Hatokufa bali ataishi

Hatokufa bali ataishi

Nakuhakikishia yupo Bay Creek Deira Dubai UAE anakula maisha. Na hiki kiitikio Cha wimbo mnachoitikia kakianzisha mwenyewe ili kupima upepo! Yupo na ni mzima wa afya hana hata mafua.
Alikuwa anaikwepa ile ripoti ya tume ya Haki za binadamu !!🤠
 
..Na yeye si inasemekana ndio amempoteza kijana wa upinzani, na kumkosakosa yule anayesemasema.
Mkuu JokaKuu, salamu zikufikie ulipo, kuna jambo ningependa unikumbushe, kipindi cha utawala wa awamu ya nne si ndiyo kipindi ambacho mzee Mizengo kayanza alikuwa PM?
OK, Sawa, je unakumbuka mgomo wa madereva wa malori uliotokea nchi nzima? Basi sawa,

sasa kama umekumbuka vyema mgomo huo nadhani utamkumbuka jamaa aliyekuwa ndiye mwenyekiti wa madereva wa malori Tanzania!
Huyo bwana nilibahatika si tu kumjua, bali niliishi naye kwa ukaribu sana, alikuwa akiitwa Swalehe Rashid,AkA Dj radi!(zamani kidogo alikuwa akijishughulisha na shughuli za u dj) bwana mmoja mtata mtata sana hasa linapokuja suala la maslahi, huyu alimsumbua sana mzee Pinda kwa kuitisha migomo ya mara kwa mara akitetea madereva wa malori kupewa heshima na haki zao kutoka kwa waajiri wao, nakumbuka mara ya mwisho Swalehe alifanya kikao na Pm akitakiwa kuacha harakati za namna hiyo, akakomaa na msimamo wake!

Kipindi hicho naweza kusema Dab hakuwa akifahamika sana kwa wengi, ila ndicho kipindi nilipopata shauku ya kumjua mtu huyu ni nani, na ana majukumu gani kwa taifa,

Unakumbuka hatma ya mwenyekiti huyo wa madereva?

Basi, Swalehe alikufa kifo cha ghafla, kwa kilichoonekana kama kawekewa sumu kwenye kinywaji,

Kwa ninavyomjua Swalehe, alikuwa mtu wa bata sana, akipenda zaidi kuwa karibu na watu wenye hadhi ya juu,

The day of his demise inasemekana alikuwa na huyo nanii sasa!! Najua nanihii hagusi pombe ila walikuwa meza moja, Swalehe akipiga kilimanjaro lager,

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa huyu nanihii alimwita ili kumpa ujumbe wa serikali dhidi ya harakati zake,

Haijulikani nini kingine kiliendelea pale, ila mara baada ya dj kutoka tu pale hotelini alianza kujisikia vibaya, akaenda moja kwa moja nyumbani kwake huku hali yake ikizidi kuwa mbaya, majirani wakamchukua na kumkimbiza hospitalini, dakika chache kabisa baada ya dj kufikishwa hospitalini baD naye aliingia, akajifanya kupush wahudumu wamuhudumie radi kwa haraka lakini sekunde chache tu baadae dj akafariki dunia,

Na ni huyo huyo baD ndiye aliyetoa taarifa za kifo cha Swalehe kwenye vyombo vya habari,

Nakumbuka vyema baada ya tangazo la kifo chenye utata cha mwenyekiti wao madereva walitishia tena kufanya mgomo usio na kikomo wakitaka waambiwe ukweli kuhusu kifo cha mwenyekiti wao,

Serikali ikaamka ghafla, ile bembeleza bembeleza ikayeyuka fasta, maderevq wakapigwa mkwara mzito uliopelekea maderee walegee miguu na Kazi ikaendelea!'
Na hata sasa kazi inaendelea,
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Anyways kufa au kuishi kwa mtu ni mapenzi ya Mungu, japo kuna vifo vingine vya kulazimishwa.

I don't like anyone to die,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom