Hatoi matumizi ya mtoto, kaomba nimkopeshe pesa

lady Jay

JF-Expert Member
May 29, 2016
526
646
Habari za weekend wapendwa,

I hope you are all doing great.Mimi ni single mum ambaye nalea mwanangu mwenyewe toka mjamzito.Babake alikataa mimba na kuomba niitoe but niligoma kuuwa kiumbe kisicho na hatia.

Nikaamua kulea mwenyewe na baada ya kujifungua, bado akakataa mtoto hivyo tukafanya DNA( kwa gharama zangu pia) na mtoto akawa ni wake.

Ilibidi aanze kutoa matumizi ya mtoto ambayo alitoa kwa miezi mitatu tu.So nikawa namkumbusha but anakwepa nikaona isiwe shida nikampotezea nikaamua kuongeza nguvu zaidi katika upambanaji.

Ndugu zake huwa wananipigia na kumjulia hali mtoto,wakiomba picha nawatumia ndo nahisi huwa wanamtumia jamaa pia.

So leo , nimekaa nawaza zangu maisha na kucheza na mrembo wangu,ghafla babake anapiga simu na kutujulia hali na kuomba nimkopeshe laki tano..Nilimjibu tu kistaarabu kuwa sina.

Na huyu jamaa anafanya kazi kwenye taasisi kubwa tu na analipwa vizuri ila amesusia matumizi ya mtoto wake na leo ana uthubutu wa kunikopa pesa. Mtoto ana miaka miwili saiv na alimhudumia kwa miezi mitatu tu baada ya DNA.

Wanaume, nimewainulia mikono.

NB:Alitumia namba ngeni so nimemblock tena.Sitaki mazoea na mtu asiyejielewa.

Jumapili njema wapenzi.
 
Habari za weekend wapendwa,

I hope you are all doing great.Mimi ni single mum ambaye nalea mwanangu mwenyewe toka mjamzito.Babake alikataa mimba na kuomba niitoe but niligoma kuuwa kiumbe kisicho na
Bravo strong youngLady !!

Kiumbe wa Mwenyezi Mungu utavuka na mambo yatanyoka... Nakuombe wepesi na faraja ktk Maisha.

Lawama na kusononeka haitasaidia kitu..
Pambana... na Life goes on..
 
Na hapo ndio kwenye ugumu sana kupima DNA. Mwanaume akilazimisha kupima hiki kipimo ni lazima uwe na uhakika silimia 80 mtoto sio wako maana majibu yakitoka ukakuta mtoto ni wako huwa ni fedhaha sana.

Dada yangu achana na hilo jamaa. Lea mtoto wako na Mungu atakuomgezea. Shida kina mama sijui mmeumbwaje asee, unaweza shangaa jamaa likalosti likajirudi ukakuta baadae mnaishi wote ukarudisha mapenzi upyaaaaaaa!
 
Habari za weekend wapendwa,

I hope you are all doing great.Mimi ni single mum ambaye nalea mwanangu mwenyewe toka mjamzito.Babake alikataa mimba na kuomba niitoe but niligoma kuuwa kiumbe kisicho na hatia. Nikaamua kulea mwenyewe na baada ya kujifungua, bado akakataa mtoto hivyo tukafanya DNA( kwa gharama zangu pia) na mtoto akawa ni wake.
Ni mtoto wa kiume au Kike?
 
i.
Zaa na mimi sitakuomba hela na ntahudumia watoto wote wawili.
 
Najua unayo Jay ila umenifanyia makusudi

Kumbuka kua ni Mbegu yangu na yai lako ndivo vimetupatia binti mrembo sana.

Maisha yanabadilika na vitu vinabadilika, mpaka imefikia wakati wa kukuomba unikopeshe utambue yakwamba nmekwama.

Mimi sio kwamba nilikua namktaa mtoto, ila kosa nipale mazingira yako ulonionyesha yakaniondolea amani,mpaka tunapima ndipo nikawa na Uhakika wa Mwanangu.

Sio kwamba sitak kuhudumia, wewe wajua kipato chang na majukum yangu nandio maana kidogo nilichopata nilikitoa, na zaidi ya yote nmekua kila siku nakuombea Wewe na Mwanangu ili muwe na maisha yenye afya njema

Nataman kuona mwanangu namsomesha naanapata huduma bora, ivo nikiwa kama mwanadam mkosaj, tambua tu ninampenda sana Mwanangu, na ninakupenda wewe nakukuheshim kwa kunizalia mtoto mzuri.

Jay, Hata ivo Adhabu yoyote utakayoamua kunipa kama hukum nitaipokea ila kumbua kua NINAKUPENDA WEWE NA MWANANGU.
 
Na hapo ndio kwenye ugumu sana kupima DNA. Mwanaume akilazimisha kupima hiki kipimo ni lazima uwe na uhakika silimia 80 mtoto sio wako maana majibu yakitoka ukakuta mtoto ni wako huwa ni fedhaha sana.

Dada yangu achana na hilo jamaa. Lea mtoto wako na Mungu atakuomgezea. Shida kina mama sijui mmeumbwaje asee, unaweza shangaa jamaa likalosti likajirudi ukakuta baadae mnaishi wote ukarudisha mapenzi upyaaaaaaa!
Asante..Ila siwezi mrudia kamwe
 
Back
Top Bottom