Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA

Kwa mh Mbowe bado humtendei haki ila kwa Mashinji huyo amepwaya sana
Mbowe anaonekana kushindwa kabisa kuhimili vitisho vya kidikteta vya mtawala John Pombe Magufuli. Pia katibu mkuu wake ameonyesha kushindwa kabisa na amebakia kama mzigo ndani ya chama! Ni bora akapisha nguvu mpya yeye pamoja na uongozi wote wa juu.
 
Wewe ulisha kuasi cdm kisa msukuma mwenzako ndani ya ccm hivyo tuwachie cdm yetu
 
Ccm haijawahi kuwa safi na haitakuwa safi milele
Wizi na umangimeza uliokuwa umeota mizizi CCM ndo uliipa boost CHADEMA na si mbowe .awamu ya tano itawarudisha huko yangu macho
 
Sababu Ambazo zitamfanya Mbowe aongoze atakavyo ndio sababu zilizo zalisha akina Mugabe, Museven, Kagame nk

Katiba ya awali ilitoa ukomo
Katiba ya sasa haina ukomo......period

Usirembe maneno eti imekaa kimya. ....
 
Uongozi wowote ule wa kidiktata, kisultani duniani huanza na kucheza na ukomo wa uongozi, Iwe mihula au miaka

Sitashangaa kabisa iwapo Magufuli atacheza huu mchezo na kuja na sababu mnazo zitoa kumteta Mbowe
 
Na nilichowaambia hapo kwamba walichofanya kina m7 na Kagame na anachofanya Mbowe n same story different versions but all are true.
Walianza na katiba na then wamekataa kutoka, sasa zito anasema maoni mapya hayakujadili kipengele hicho, nikauliza wanachama walipelekewa maoni ama walitoa maoni?
Kama walipelekewa Nani alitoa maoni hayo na hilo oni akaamua kuifanya liwe hivyo na akilifuta la zamani?
Kama waliatoa maoni wenyewe je waliamua kuupuuza ukomo na kuuweka ukomo kiini macho?
Je kwa mantiki hiyo Mh Raisi akiamua kufanya hivyo na akapitia njia hiyo hiyo hawa CHADEMA watapata wapi ujasiri wa kupinga .?
Sababu Ambazo zitamfanya Mbowe aongoze atakavyo ndio sababu zilizo zalisha akina Mugabe, Museven, Kagame nk

Katiba ya awali ilitoa ukomo
Katiba ya sasa haina ukomo......period

Usirembe maneno eti imekaa kimya. ....
 
So unaamini kuwa hata chamani hakuna uchaguzi huru na wa haki si ndio, maana Mbowe na hao ni same story different versions but all are true. Wengine n nchi na mwingne ni chama ila utaratbu n ule ule na njia n ileile.
Nachosema ni kwamba uchaguzi ukiwa huru na haki basi mbowe hawezi tawala milele

Sababu Ambazo zitamfanya Mbowe aongoze atakavyo ndio sababu zilizo zalisha akina Mugabe, Museven, Kagame nk

Katiba ya awali ilitoa ukomo
Katiba ya sasa haina ukomo......period

Usirembe maneno eti imekaa kimya. ....
Mkuu hao kina museveni wapo pale sio sababu hakuna ukomo bali chaguzi zao sio huru na haki!! Ila chaguzi zikiwa huru kama Ya kule Gambia mbona Yahya Jammeh aling'olewa ingawa naye hakua na ukomo??

Muhimu ni uchaguzi uwepo kila miaka 5 wa huru na haki kma wamemchoka atang'olewa tu haijalishi ni museveni au mbowe.

Simple and clear

Ila nchi kama Russia na Uturuki kuna ukomo wa urais ila kila ukiisha wanabadilisha vyeo ili kulinda madaraka je hyo ndio demokrasia kisa kuna ukomo?? Nadhani demokrasia kwa CHADEMA ni ile ya uchaguzi kila miaka 5 hapo ndio pa kumdhibiti Mbowe sio eti ukomo?? What is ukomo kama Mbowe hatofuata katiba??
 
Kuna ukweli kwamba mbowe kafanya mazuri chadema, lakini chondechonde walio karibu na mbowe wamshauri asigombee Mwaka huu.chadema inahitaji kupata damu mpya na nguvu mpya.Ni vizuri wakakaribishwa wanachama wengine wagombee tena kwa kushindanishwa. Nje ya hapo demokrasia mashakani
 
Mkuu get it right kina museveni hakuna chaguzi huru na haki ndio maana wapo madarakani sio eti kisa hawana ukomo!!

Ukomo is nothing kwenye demokrasia kama hakutokuwa na utawala wa sheria na chaguzi huru.....

However ngazi ya taasisi na taifa ni tofauti kidogo so tusijengee hoja kwa level ya taasisi kulinganisha na taifa.... Mbowe hata akiwa dikteta level ya chama itaathiri watu wachache tu lakini kitaifa itaathiri Vizazi vya watu million 50!! Kwahiyo impact ya madhara ni ndogo ngazi ya taasisi kuliko taifa. Ni sawa mtu aseme kama tunachagua Rais wa nchi basi na Mkuu wa Majeshi apigiwe kura na Rais utakubali?? Au mkurugenzi wa TISS igombewe kama vile jimboni??

Tusipende kurelate parameters za Taasisi na Taifa au bodies kama Jeshi/Intelligensia maana kila kitu kina mipaka yake na taratibu zake sasa mkilinganisha ili kujengea hoja mtachemka wakuu.

CHAGUZI HURU NDIO SULUHISHO KWA MADIKTETA sio UKOMO!!
 
Apumzike!Tundu lissu achukue nafasi hiyo.
Akiendelea kugombea atakuwa na tofauti gani na Mugabe?
Ruhusuni demokrasia ichukue nafasi yake,
Jisemee nafsi yako na acha kuisemea asilimia 99 ya sisi wanachama ambayo hutujui tunamtaka nani
Haahaa yaleyale ya ccm hakuna mwanachama mwingine kuchukua fomu kugombea isipokuwa magu.chadema wanawavunja moyo sana wapenda demokrasia...
 
Demokrasia inafuatwa barabara na Katiba Inaheshimiwa.Mbowe hajichagui bali anachaguliwa na wanachama na washindani wake wanakiri kushindwa
haahaa kwa kura za maruhani? Zile za huyuhuyu na hapana mwingine stail ya ccm...
 
Mbowe hakika anafaa kuendelea ila katibu mkuu wake hapana kapoa sana kama maji ya mtungi katibu awe John Mnyika
Mkuu hao wote watatu wamepoa sana, kiujumla wameishiwa pumzi.mbowe polis wanakamata wanachama wake nchi nzima wako kimya tu...
 
Una tofauti gani na Musiba, Nkamia, Mkulima.

Mbowe anabakia kwenye uenyekiti kwa mbinu zile zile alizotumia Mugabe, Museven, Kagame, Nkurunziza na huyu wa kwetu ana hivyo vidalili dalili.
Nakubaliana na we mkuu ukiona mtu anatamani mh Mbowe aondoke kwenye nafasi aliyo nayo kwa sasa ndani ya cdm huyo siyo mwana cdm bali ni mamluki na oandikizi la ccm
 
Hapo uliposema Mbowe huwashinda wenzake nimecheka sana.Mbowe huwa anawashinda akina nani?
 
Ili aendelee kuenziwa na kusifiwa na wanachama, huu ni wakati mzuri zaidi wa yeye kuachia usukani ili chama kisije mfia na lawama tele.

Mcheza ngoma hata awe mahiri vipi, lazima ajue muda wa kuacha kucheza na kupisha wenzake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…