Hatma ya Freeman Mbowe CHADEMA

KWANI HUU UWENYEKITI WA CHAMA KILICHO NJE YA MADARAKA UNAUMUHIMU GANI KUPOKEZANA WAKATI MASLAHI YAKE NI MADOGO.NGOJENI TUWE CHAMA TAWALA NDO MUDAI KUPOKEZANA VIJITI,MUKIPOKEZANA SASAHIVI MUNAUWA CHAMA,
MBOWE NI SIMBA WA UPINZANI,
 
Anajitengenezaje kuwa Sultani? Au kwa kuwa umekaririshwa na wewe unatiririka tu!!
Same story different version but all are true, niambie tofauti za Mbowe na kina Kagame na Museven kwenye kuhodhi madaraka.
Wote wanatumia njia moja mwendo mmoja ila kule n nchi na hapa n chama.
Remind me ni kina Nani wenye nguvu ndani ya chama waliowahi kugombea uenyekiti wakasurvive?
 
Ni nani aligombea Uenyekiti ndani ya CHADEMA akakataliwa?
 
Ni nani aligombea Uenyekiti ndani ya CHADEMA akakataliwa?
Hujajibu swali hapo nimekuomba unikumbushe ni kina Nani wenye nguvu kicheo CHADEMA waligombea uenyekiti wakasurvive namaanisha , makamo mwenyekiti , ama katibu and the likes ile top layer .
Hao wengine ambao waligombea ni kama alivyofanya kagema na uchaguzi wake hawana impact kubwa.
I stand to be corrected.
 
allantence hoja zangu na za zitto junior havitofautini sana.

  1. Hakuna anayekatazwa kugombea Uenyekiti ndani ya CHADEMA
  2. Ukomo wa muda wa uongozi upo ndani ya CHADEMA
  3. Mbowe hazuii wengine kugombea
  4. Uchaguzi huru na wa haki ndiyo kigezo kikuu cha Demokrasia kwenye siasa
  5. Ukomo wa uongozi pekee siyo kiashiria cha demokrasia ndani ya taasisi
Nasisitiza tena kwamba hakuna mtu anayekatazwa kugombea Uenyekiti ndani ya CHADEMA na kama wewe unaona yupo anayefaa mpendekeze!!
 
Reduced to nothing?Naamini umetumia maneno makali bila sababu.
Naaamini wanaomini katika maendeleo hawawezi kufurahishwa na kufa kwa opposition katika nchi inayojinasibu kuwa ni ya kidemokrasia.
Paskali umetumia maneno makali lakini all what is happening now yalifanyika huko nyuma tena kwa kishindo.
Pitia historia uangalie kishindo kilicholetwa na Azimio la Arusha,pitia historia uone ujenzi wa Tazara,pitia historia uone uanzishaji wa viwanda ambavyo vilitumia raw materials za kutoka hapa nchini.
Pitia historia uangalie kuanguka kwa maendeleo yote haya makubwa na ni nani waliofanikisha.
Kudumaa kwa demokrasia kutaendelea katika awamu na wawakilishi watakuwa wachache na ushindi utakuwa wa kishindo ila mitazamo tofauti haitapotea.
Raisi wetu anafanya kazi kubwa mno ila isiwe sababu ya kuona mitizamo tofauti haina nafasi tena.
 
Mkuu lazima ukubali Mikakati ya mbowe (Hata ikiwa ya siri) imetufikisha hapa tulipo, kimoja nachokumbuka nna rafiki yangu wa karibu kabisa ni viti maalum kwa sasa alikuwa na kipaji haswaa cha uongozi na hata kujenga hoja pale mzumbe nakumbuka kina Mbowe walikuja na kuidentify kipaji chake na kumuomba ajiunge CHADEMA kiufupi walifanya sourcing ya namna hiyo vyuoni enzi hizo ndio kashika uenyekiti ili kupata vijana wenye potential na hii ndio ikawa siri ya CHADEMA kuwa na loyal youth politicians waliokua msingi wa kuishusha kabisa ushawishi CCM.

Unapotafuta ukweli wa jambo kwenye process nyingi lazima utambue ni wakati gani kwenye hiyo process kuna reaction iliyochochea mabadiliko ndio utagundua kama kuna relationship ya mbowe na kukua kwa chama.

Ukiangalia wakati ambapo CHADEMA ilianza kupaa ni kuanzia 2005 wakati ambao ndio mbowe alikua mgombea wao wa kwanza wa Urais na alikua ndio fresh chairman hivyo unawezaje pinga mbowe hahusiki ilihali kabla ya hapi chadema ilikuwepo ila ya kawaida tu why mbowe??

Alibadili nembo ya chama/ Bendera, rangi, katiba, sera, mfumo wa uendeshaji siasa/kampeni, kukifanya chadema kutoka chama cha maofisini kuwa cha kuleta mabadiliko/kikamanda hata ndio wakati wake tulianza vaa Combat na misemo kama People's Powerr ilitumika zaidi wakati wake.

Hii ilikipa taswira mpya kabisa na kama kilizaliwa upya na kujenga misingi ya kuwatumia vijana kama ngazi ya kuleta mabadiliko maana aliamini wazee walishatekwa na CCM ideology ila vijana waliozaliwa miaka ya 90 huko walikulia wakati wa vyama vingi hivyo CCM haikuwa issue sana kwao. And hii strategy alone iliifuta kabisa CCM hapa nchini hasa kuanzai uchaguzi wa 2010.

2. Kuhusu kila binadamu kufikia mwisho wa uwezo wake ni kweli na ndio maana CHADEMA kuna uchaguzi kila baada ya miaka 5 hivyo akionekana kafika mwisho wa uwezo wake anachaguliwa mwingine. Sasa sielewi kivipi ukomo ndio kigezo cha uwezo wa mtu kufika mwisho wakati kuna parameters zinazopima uwezo wake zinajadiliwa huko kamati kuu.

Nachokiona hapa watu wanaongozwa na mahaba kuliko facts. Mfano timu za mpira unakuta haichukui ligi miaka na miaka ila kocha hatimuliwi sie wa nje tunaweza toka mapovu kuwa mbona kocha fulani hatimuliwi kumbe Jukumu lake analobeba timu sio makombe bali stability kwenye dressing room,nidhamu,kudhibiti fedha n.k

Same kwako na Pascal Mayalla mnapima saturation point kwa kuangalia CHADEMA haifanyi mikutano,wabunge wanaondoka n.k bila kujua kuna parameters Kamati Kuu wanatumia kumjudge Mbowe labda connection na wadhamini wa huko nje, uwezo wake wa kujenga nidhamu kwenye chama na vikao vya chama n.k sasa haya mambo kwa nje hamyaoni ila kamati kuu wanayaona.

Sasa nyie kivipi ndio mseme yupo saturation point ilihali huko ndani wanamtathmini kwa vigezo tofauti kabisa na mnavyowazia nyie hapa??

Ni hayo tu
 
Hii hoja yako ndiyo imeufunga mjadala huu kwa upande wangu!!
 
Hoja zenu kwa mtazamo wenu zipo sahihi lakini n kiini macho , ndio maana nimekuuliza hapo kuna tofauti gani Kati ya hao niliokutajia mwanzo na Mbowe?
Unadhani kama sio kiini macho n nn?

Nikaomba unitajie hao wenye nguvu kicheo chamani nawalioamua kupambania uenyekiti ni kina nan na je walisurvive?

La mwisho unadhani kukitoa kile kipengele cha ukomo, cha vipindi vya mtu kulikuwa na manufaa? Je Haya yasingeepukika? Kama kingekuwepo hadi Leo Haya yangetokea.?
 
Mbowe hakika anafaa kuendelea ila katibu mkuu wake hapana kapoa sana kama maji ya mtungi katibu awe John Mnyika
Hamjajua mpaka sasa tupo kwenye mfumo wa chama kimoja cha siasa ndani ya mfumo wa vyama vingi? Huyo Mnyika nae atapoa tu. Nasubiri siku Mbowe akituagiza tukinukishe tujue moja tunakufa, tunawekwa jela au tunafanya ukombozi
 

Kwa utawala huu umpe chama mashinji kinageuka cuf au tlp huyu jamaa kaporwa had mali zake lakin hakutetereka unataka tuwe na mtu kama slaa anamkimbia lowasa kisha wanaungana huko ccm?
 
Tundu Lissu hafai kuwa Mwenyekti wa Chadema kwa kuwa ana mpango wa kuungana na Wahaini wa Visiwan pamoja na Mbembe mmoja toka Ujiji Kigoma ili kumvunja moyo Rais wetu kukomboa Nchi

Wakina shein
 
Kwa mwana cdm wa kweli hawezi kuwa na mawazo ya kijinga na kipumbafu na kusema eti mh Mbowe awachie nafasi ya uwenyekiti.
 
Nakubaliana na we mkuu ukiona mtu anatamani mh Mbowe aondoke kwenye nafasi aliyo nayo kwa sasa ndani ya cdm huyo siyo mwana cdm bali ni mamluki na oandikizi la ccm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…