Umeamua kujipigia debe ww mwenyewe!!Wakati Freeman Aikaeli Mbowe anachukua nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa kutoka kwa mzee Bob Nyanga Makani, alikuta kuna Wabunge wa 5 na Madiwani wasiozidi 75 nchi nzima. Wabunge wasioweza hata kujaza sebule yenu hapo.
Leo tukielekea kwenye uchaguzi mkuu mwingine wa ndani wa CHADEMA, Mwezi Desemba, 2019 CHADEMA kuna Wabunge zaidi ya 65 madiwani zadi ya 1500 nchi yote, halmashauri za kutosha na wanaunda kambi ya upinzani bungeni (KUB)
Hivyo ni vyema wewe "kijana - baro baro" wa leo mwenye kuendeshwa na "mihemko" kutambua haya mafaniko makubwa kabla ya kusema "Mbowe ameiua CHADEMA", inawezekana hujui hata CHADEMA imefikaje hapa ilipo leo, sio miujiza, ni STRATEGIES!
Kuna Vijana wa leo, labda kwa mihemko na juhudi za kutumika hawajui nguvu iliyotumika, jasho lililomwagika hadi kuifanya leo CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani. Wanadhani ni kitu rahisi kama kucheza 'BIKO na TATU MZUKA'
Hatusemi kwamba Freeman Mbowe ni malaika, kwamba hakuna dosari na makosa kwenye uongozi wake, hapana, isipokuwa jasho, damu na machozi yake yamemwagika kwa ajili ya CHADEMA, tuhuma zenu zinapaswa kuwa 'Valid' wakati wa kumkosoa, tuhuma za JINAI zithibitishwe!
Freeman Aikaeli Mbowe ni mwenyekiti halali wa CHADEMA, na ataondoka madarakani siku wanachama wa CHADEMA wakisema "imetosha" kupitia mkutano mkuu, sio kwa sababu "Kuna kelele za CCM na mapandikizi" huko nje za "Mbowe ondoka! Mbowe ondoka!"
Mzee Bob Makani alikuwa na kadi namba Tatu ya CHADEMA, kadi namba Mbili ilikuwa ya Mzee Brown Ngilulupi na kadi namba moja ya Mzee Edwin Mtei, hawakukosea kamwe kumuona Freeman Mbowe na kumkabidhi CHADEMA ambayo ameifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania.
Mwisho, kimsingi, CHADEMA imebarikiwa kuwa na mwenyekiti kama Freeman Mbowe, wengine tuliopata fursa ya kufanya nae kazi au kukutana nae, tunajivunia sana, he's a man and a-half!
Stay blessed Chairman!
Mbowe Tano Tena Uchaguzi Mkuu 2019
Nani anajipigia debe?Umeamua kujipigia debe ww mwenyewe!!
Hujui usemalo kijanaMkuu iko hivii? Kupendwa kidemokrasia hutokana na kura za raia. Aanze kwanza na chaguzi zake za ndani ili tutathimini unalolisema.
Tatizo hawapewi mafunzo kwanza ya kupiga propagandaKwani kwenye chaguzi za ndani za CHADEMA kuna tatizo gani?
Asante mkuuWapatikane wabunge, wasipatikane. wanachama wanamtaka mbowe full stop.
Hivi kwa akili yako fupi unaamini tuna bunge hapa.
Hakuna mtakatifuNo matter how good one is, ukifikia point ya saturation unakuwa a saturated solution, you can take no more than you can.
One can be very good and very instrumental ukafanya a lot of good things, lakini akifikia optimum ya uwezo wako, you can do no more good than you did.
Waasisi wa Chadema walioweka kipengele cha ukomo wa uongozi ni vipindi viwili vya miaka 5 mitano, ndani ya katiba ya Chadema, walikuwa na maana yao nzuri tuu, lakini jinsi kipengele hicho kilivyo yeyuka into thin air kwa kunyofolewa kinyemela, leaves much to be desired.
Na ukiizungumzia tuu hoja ya ukomo, wanakushukia kama mwewe!.
Tuhuma Hii: CHADEMA kuendeshwa kwa Katiba "Fake" ikithibitishwa, CHADEMA inaweza kufutwa
Wanabodi, Uendeshaji wa vyama vya siasa nchini, unaongozwa na sheria, taratibu na kanuni. Ikithibitika pasipo shaka kuwa chama fulani, kinakiuka sheria, taratibu na kanuni, kinapaswa kuwajibishwa, kuadhibiwa hata kufutwa, kutegemeana na tuhuma halisi!. Miongoni mwa masharti ya usajili wa...www.jamiiforums.com
PGE2015 - CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!
Wanabodi, Preamble: Chadema ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!, hii thread ni ya swali tuu, Hivi Chadema ilivyo, bado haijakabidhiwa nchi, inatoa...www.jamiiforums.com
Mkuu sipingani na wewe wala sijasema kama yanayozungumzwa kwenye mitandao ni kweli au si kweli.Pakawa kuna hoja nyingine ni za Kihistoria na nyingine ni hisia tu za watu. Kwanza si kweli kwamba Mbowe ni lazima awepo madarakani ili CHADEMA iwepo lakini ni ukweli kwamba kwa CHADEMA Mbowe bado ni kiongozi Imara na shupavu.
Sijui ni nani anayeleta hoja kwamba kuwepo kwa Mbowe kwenye uenyekiti ni kiashiria kwamba CHADEMA inadhoofu ama itashindwa kwenye uchaguzi wa mwakani.
Kwangu mimi uimara wa Mbowe naupima kwa mashambulizi yanayofanywa na CCM kwa kutumia vyombo vya dola dhidi ya CHADEMA. Kama Mbowe si imara kwa hakika kabisa CHADEMA isingekuwa hapa ilipo na wala isingekua hivi ilivyo.
Sielewi ni kwa nini kuna watu mnaona kama vile CHADEMA haipendi kukosolewa. Tofautisheni kukosolewa na kusingiziwa. Ukisingiziwa na wewe ukakaa kimya huo ni udhaifu. Kwa nini mnataka kila baya linalosemwa dhidi ya CHADEMA liwe ni kweli?
Kulipwa mishahara kwa kodi za wananchi hakuhalalishi kujitoa mhanga. Hao wanaopora haki za walioko CHADEMA hawalipwi mishahara kwa kodi za wananchi? Kwa nini msipaze sauti kusema waache kupora haki za CHADEMA kwa kuwa wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi?
CHADEMA wanaonya, wanatoa sera mbadala, wanajenga chama chao, wanakosoa na kuonesha makosa ya CCM jinsi inavyoendesha serikali ulitaka wafanye nini tena? Wananchi wao wenyewe wanapigania haki zao zinazotajwa na CHADEMA kama zinavunjwa na CCM kwa jinsi inavyoendesha serikali?
Visasi gani?Yanayochukiza kwa rais yeye ndiyo kiongozi WA nchi lakni anaongoza kwa visasi vya kijinga.
Ni sawa lakini yawe wazi kwa kila mtu ama kwa vikao husika vya CHADEMA?Kama ni matumizi au Mapato yawe wazi.
Visasi vya kisasi!!Visasi gani?
Kuna shida ya watu kuingilia taaluma, ripoti inaposema ni hati chafu au ya mashaka haimaanishi kuna wizi ila mfano una mali kama magari au Majengo hujayathaminisha hivyo hujui value yake huo nao unarekodiwa ni ufisadi!! Hivyo utapewa hati ya mashaka/chafu. Hayo mambo yapo kiuhasibu zaidi sio necessarily wizi uwepo bali sheria za kiuhasibu/Ukaguzi zifuatwe.CDM ina Ruzuku, Hujasikia watu wakilalamima kuwa 1.2b imepigwa. hukumbuki Ripoti ya C.A.G. endelea kujitolea Bob!
Unajua pascal unanishangaza sana ni lini ukomo wa madaraka ni indicator ya demokrasia per se?? Russia na Uturuki kulikuwa na ukomo wa madaraka ila umeona watawala walivyouchezea huo mfumo hadi wanabadilisha majina ya vyeo ili waendelee kutawala!!Mkuu Zitto jnr, kwanza asante for much respect.
Utungaji katiba is a process, kila kilichokuwepo kwenye katiba ya mwanzo, kilikuwepo kwa sababu, unapotunga katiba mpya, kila kitakacho ondolewa lazima kijadiliwe with minutes written down.
Katika huo utunzi wa katiba mpya hakuna minutes zozote kuhusu kipengele hicho, as if it's an oversight, kwa taarifa kipengele hicho ni moja ya misingi mikuu kwa Chadema kuitwa Chama cha Demokrasia, how can katiba ya Chadema iwe silent?.
P
Mkuu samahani unaposema hakikujadiliwa kwenye katiba pendekezwa au Mpya si n sawa na kunyofolewa?Mkuu Pascal Mayalla huwa unaheshimika sana hapa jukwaani na muda mwingine huwa unaongea kwa mafumbo lakini hapa Sidhani kama unaongea kwa parables maana upo clear kuwa CHADEMA imefuta kipengele cha uongozi.
Hili swali aliwahi uliza Nape humu jukwaani na akajibiwa na Dr slaa pamoja na JJ Mnyika kwa hoja na nyaraka kwamba kipengele cha ukomo hakikufutwa ila katika kusaka maoni ya kutunga katiba mpya chini ya Prof Baregu suala hilo halikuwekwa na wanachama.
HIVYO BASI unapojenga hoja kuhusu suala hili usiseme kilinyofolewa bali sema katiba mpya haijazungumzia. Maana mtu anaweza dhani ilifanyiwa amendment ikafuta hiko kipengele.
Pascal upo credible so una uwezo wa kutengeneza au kuharibu so kabla hujachangia lolote keep your facts straight!!
Ni hayo tu mkuu wangu
Kwani ukomo wa uongozi kwa CHADEMA ni miaka mingapi?Mwana Taluma mwenzangu kwanza nianze kwa Kukusalimia habari za siku, sikuweza kuwepo jukwani kutokana Na masomo yanayonikabili,
Kwanza nianze kwa kukukumbusha Freeman Mbowe ataondoka pindi wanachama wakisema aondoke si kwa shinikizo kutoka kwa wanaoitakia chadema mabaya pili mbowe amekitoa chadema sehemu ambayo ccm hawakutegemea kuwa leo chadema kitafika kwahiyo freeman mbowe ndio chaguo la wana chadema na Watanzania kwa ujumla
Wasalam
Huko kupisha ndiyo kukoje?KUTOWAPISHA WENGINE
1. Mkuu katiba mpya inavyoandikwa ni kusaka maoni upya kabisa, mnakuja na framework mpya kabisa hivyo huwa vipengele vingi sana vipya vinakuja na vingi vya zamani kuondoka. Yaani mfano katiba ya warioba ilikuja na vitu vipya kabisa mfano muundo wa serikali tatu ambayo yalikuwa maaoni ya wananchi sasa kivipi mtu atokee aseme warioba alifuta serikali mbili??? Ilihali alianza kitu kipya kabisaa kwa maoni na mchakato na mfumo mpya. Kwahiyo ni kweli kipengele hicho hakipo kama ambavyo vipengele zaidi ya 100 havipo na vingine zaidi ya 100 vimeongezwa sasa sielewi kwanini hoja ijengewe kwenye kipengele cha ukomo tu na sio vingine?? Na hiyo kamati iliongozwa na Prof Baregu na katibu wake mnyika sasa kivipi tena atajwe mbowe ambaye alikua hana mizizi CHADEMA enzi hizo??Mkuu samahani unaposema hakikujadiliwa kwenye katiba pendekezwa au Mpya si n sawa na kunyofolewa?
SA hivi CHADEMA wanatumia katiba ipi?
Hiyo yenye kipengele cha ukomo au ambayo haina kipengele cha ukomo?
Kama ni hiyo yenye kipengele cha ukomo, je Mh. mwenyekiti ametimiza ukomo kikatiba ? Kama ni nyingine je ataendelea hadi lini?
Natumai utanielekeza vizuri hapo.
Wakati Freeman Aikaeli Mbowe anachukua nafasi ya uenyekiti wa CHADEMA Taifa kutoka kwa mzee Bob Nyanga Makani, alikuta kuna Wabunge wa 5 na Madiwani wasiozidi 75 nchi nzima. Wabunge wasioweza hata kujaza sebule yenu hapo.
Leo tukielekea kwenye uchaguzi mkuu mwingine wa ndani wa CHADEMA, Mwezi Desemba, 2019 CHADEMA kuna Wabunge zaidi ya 65 madiwani zadi ya 1500 nchi yote, halmashauri za kutosha na wanaunda kambi ya upinzani bungeni (KUB)
Hivyo ni vyema wewe "kijana - baro baro" wa leo mwenye kuendeshwa na "mihemko" kutambua haya mafaniko makubwa kabla ya kusema "Mbowe ameiua CHADEMA", inawezekana hujui hata CHADEMA imefikaje hapa ilipo leo, sio miujiza, ni STRATEGIES!
Kuna Vijana wa leo, labda kwa mihemko na juhudi za kutumika hawajui nguvu iliyotumika, jasho lililomwagika hadi kuifanya leo CHADEMA kuwa chama kikuu cha upinzani. Wanadhani ni kitu rahisi kama kucheza 'BIKO na TATU MZUKA'
Hatusemi kwamba Freeman Mbowe ni malaika, kwamba hakuna dosari na makosa kwenye uongozi wake, hapana, isipokuwa jasho, damu na machozi yake yamemwagika kwa ajili ya CHADEMA, tuhuma zenu zinapaswa kuwa 'Valid' wakati wa kumkosoa, tuhuma za JINAI zithibitishwe!
Freeman Aikaeli Mbowe ni mwenyekiti halali wa CHADEMA, na ataondoka madarakani siku wanachama wa CHADEMA wakisema "imetosha" kupitia mkutano mkuu, sio kwa sababu "Kuna kelele za CCM na mapandikizi" huko nje za "Mbowe ondoka! Mbowe ondoka!"
Mzee Bob Makani alikuwa na kadi namba Tatu ya CHADEMA, kadi namba Mbili ilikuwa ya Mzee Brown Ngilulupi na kadi namba moja ya Mzee Edwin Mtei, hawakukosea kamwe kumuona Freeman Mbowe na kumkabidhi CHADEMA ambayo ameifanya kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania.
Mwisho, kimsingi, CHADEMA imebarikiwa kuwa na mwenyekiti kama Freeman Mbowe, wengine tuliopata fursa ya kufanya nae kazi au kukutana nae, tunajivunia sana, he's a man and a-half!
Stay blessed Chairman!
Mbowe Tano Tena Uchaguzi Mkuu 2019