Willy, Le Mutuz, Mutu mukubwa.
Uandishi mzuri na wahaki ni kutafuta story pande zote mbili. Kwanini hujamtafuta huyo binti/mabinti uwahoji ili tujue story yao? Mbona hujamuuliza Mzee wa vibinti kuhusu polisi Osterbay?
Kauli ya kwanza ya Mzee wa Vibinti aka Akudo alikana kumjua huyo binti, na alikana namba za simu kusema alizigawa miezi sita kwanini haya maswali hayapo.
Kwa upembuzi yakinifu wa post zako zote za kumtetea Mzee wa Akudo/vibinti/ inaonyesha wazi ameafanya kosa, binti ni mdogo kama alivyosema, alibakwa kwasababu ya shida tu na utoto, MZee wa akudo ze prof alijaribu kuficha ikashindikana.
Ukimwi hauonekani machoni, na ukimwi sio kesi au shutuma ya msingi. Shutuma ya msingi ni kubaka, kudhalilisha, matumizi mabaya ya ofisi ya umma Ubunge. Then kama binti ameambukizwa ukimwa hii ni kesi ya kudhuru maisha na kukusudia kuuwa kwa makusudi.
Mpaka pale binti atakapopatikana na umri wake kuthibitika, na wote waliotajwa kukiri au kukataa, katibu wa Mzee wa Vibinti, polisi binti alipopeleka kesi, Kinana aliyemuona binti, bunge , Gazeti la Tanzania Daima, kikundi cha haki za binadamu ambacho nao wamemwona na kuchukua maelezo, Waalimu wa shule wa Turiani, chuo cha tumaini wote hawa lazima waseme kama hii story ya Prof Kapuya mzee wa vibinti ni ya kweli au ya binti.
Mpaka sasa naona unajitajihidi kumuogesha Prof Kapuya kwa jiki-hawezi kutakata.