Hatimaye pepsi wamvua ubalozi Diamond Platnumz

Hatimaye pepsi wamvua ubalozi Diamond Platnumz

Lilikuwa ni suala la muda tu. Hatimaye imetiki. Pepsi imemvua ubalozi diamond , hivyo diamond ameondoa utambulisho rasmi wa yeye kama balozi wa pepsi Tanzania.
Wayatoe sasa na yale mapichapicha yake ya mabango huku anakunywa bia huku anakunywa soda anatuchukuliaje kwa mfano?
 
Lilikuwa ni suala la muda tu. Hatimaye imetiki. Pepsi imemvua ubalozi diamond , hivyo diamond ameondoa utambulisho rasmi wa yeye kama balozi wa pepsi Tanzania.

Sasa hapa inabidi nguvu nyingine itumike kuwashawishi serengeti nao wamtose ubalozi



Pia jambo lingine Diamond amefuta picha ya Samuya iliyobaki kwenye account yake.

Ikumbukwe diamond ilibidi aje apafomu siku Samia anaapishwa ila walimtosa kwa sababu alifuta picha za kampeni .

Kingine cha mwisho diamond followers wake wanazidi kupungua , mpaka sasa wapo milioni moja laki saba na elfu 20 ,hivyo mpaka kufikia jumanne atakuwa na followers 1.6M kushuka chini.


Kikubwa zaidi kama ulim follow hakikisha una m unfollow kisha una ripoti akaunti yake.
Nimeanini ukizaliwa maskini si ajabu ukaendelea kuwa maskini........kwa mawazo haya diamond ataendelea kuwatia vidole
 
IMG_1524.jpeg

Mbona bado ipo?
 
Watoto wajinga wa kiafrika aisee inatafakarisha sana. Kwahiyo akianguka wewe ndio utainuka? Masikini ni mtu mjinga kabisa duniani
 
Hatuwezi kujitenga na mziki babu, akili yangu imekaa sawa baada ya kusikiliza amapiano na nyimbo za hawa wasanii..

Wana makosa yao lakini mziki ni dawa.
 
Back
Top Bottom