Hatimaye nimeweza,ila kuna jipya...

noella

Senior Member
Mar 21, 2011
101
46
Wandugu natumai mu wazima.

Ni mwezi mmoja na nusu umepita tangu nifanye maamuzi magumu ya kuachana na baba mtoto wangu.
Ila pia ni mwezi mmoja na nusu wa machungu ya moyo maana nilifanya maamuzi hayo nikiwa bado nampenda ila sikuwa na jinsi kwa maana nilikuwa kwenye mahusiano yenye mateso.
Baada ya kumwambia maamuzi yangu jamaa alikasirika sana na kutishia kutotaka kujua lolote la kuhusu mtoto.cha kushangaza alirudi tena na kuanza kunitishia maisha yangu na ya mwanangu kama tu ataona mimi nina mtu mwingine, na story haikuishia hapo alidiriki kutuma msg kwa mama yangu mzazi kumwambia maneno hayo ya kutisha pamoja na kwamba mama yangu ndio chanzo cha mimi kumuacha kwasababu hakuwahi kumshauri yeye wala mimi.na pia alinitumia msg nyingi za matusi ambayo siwezi kuyaandika hapa.
Hatimaye juzi kanitumia msg kuwa na yeye anamove on hajali kama huyo mtu anampenda au la na tuone mwisho wangu.

kwa kipindi chote hiko sio kama ninaona raha yeye kuhangaika ila na mimi pia nilikuwa naumia na mpaka sasa hivi i wish kungekuwa na miujiza ya kumbadilisha tabia zake. namshukuru Mungu sasa hivi nimezoea na pia cha kushangaza leo katuma fees ya mtoto from nowhere.

Sasa basi, kisa cha mimi kuandika hapa leo ni kwambaa,wakati huo wote kwa muda wa kama miaka miwili kuna kijana ambaye nilikuwa nikimuhadithi matatizo yangu ananishauri na vitu kama hivyo ni rafiki tu wa kawaida na tunaelewana sana, bila kujua yule kijana ananipenda. baada ya kujua tumeachana huyu kijana kazidisha kuwa karibu na anadiriki kunambia mimi ndo mke wake siku zote alikuwa anajua sitolast na baba watoto wangu. afu kaniintroduce kwa kaka zake na sister zake na marafiki, na anapenda kuongelea mambo ya ndoa na jinsi tutakavyoishi pamoja na mwanangu etc, nikisema mi sipo tayari na mahusiano anakasirika mbaya hatoongea siku nzima.

tatizo ni kuwa naona kama yuko too fast na pia ni mdogo kwangu kwa miaka miwili. ni kijana mwenye hekima na busara na mwenye sifa zote za kuitwa baba na mume bora.

naombeni mawazo yenu ya busara wanaMMU
 
hizo side effects za kutosana! unafanya upate pa kuegemea, ila sio kwamba unampenda!
 
hebu subiri kwanza bana sasa ukisema hauko tayari ananuna siku nzima huoni hiyo ni tabia ya ubabe na kutojali.vuta subira ubongo upate utulivu wa fikra mama.
 
Bado akili haijatulia na kovu bichi kabisa unajitwisha mzigo mwingine..........

sasa nimekuelewa....sina uhusiano nae wa kimapenzi ni rafiki tu wa muda mrefu, yeye ndo anakuja speed na gia za mahusiano na kunitambulisha kwa watu wake but huwa anasema "she is my best friend"..i told him mi sipo tayari na mahusiano kwa sasa.
 
dah japo mie sijaolewa ila nakushauri utulie tuli , wahenga wanasema kwenye ndoa kuna wakati wa masika na kiangazi .ila usikurupuke piga maombi kwanza manake wanaume wenyewe sharobizo usije umia mammy
 
tuliza akili walau mwaka mmoja huku ukimchunguza huyo kijana kabla hauajaamua lolote.
Moyo wa mtu ni msitu mnene, usiusemee moyo wake tena mapema hivyo.
be careful to whom you give your heart, coz when you give your heart to some1....you are not only giving that person the right to love you! but also... the power to hurt you.
 
Mwambie akupe muda ni mapema sana sasa kufanya maamuzi

Fuata ushauri wa FL1 lakini usimpotezee na pia usithubutu kuingia kwenye ndoa haraka haraka, vuta subira kwa miaka kama miwili hivi kuona pumzi yake kama kweli ana mapenzi ya kweli au ni msanii tu. Kama kweli anakupenda kiasi cha kutaka uwe mkewe basi miaka miwili hataiona mingi hata kidogo.
 
noella kwanza kabisa pole na hongera kwa ujasiri wa kuamua kuendelea na maisha yako ni wachache sana wenye ujasiri kama huo.
Pili, mtoto wako ana umri gani? Umesema una mwezi na nusu toka umesitisha uhusiano na baba mtoto, wewe binafsi huoni kuwa ni mapema sana kujiingiza kwenye mahusiano mengine licha hata ya kuwauliza wanaJF kwa ushauri?!unataka kuniambia wote hapa tukikwambia umkubali huyo jamaa wewe utaona ni sawa na utakubali kwasababu ya wengi wape???!!!

Nisamehe kama nitakua nimekukwaza lakini kwa jinsi nilivyokusoma ni kama na wewe umeanza kumfeel jamaa......kila la kheri mwaya.
 
Last edited by a moderator:
Yaani ukikosea tena maisha yako yatakuwa valuvalu, pumzika kwanza, angalia Elimu yako, Kama unaweza fanya kitu kingine mbali na kazi unayofanya, yaani biashara hivi, jijengee uwezo zaidi kifedha na kielimu, mapenzi ya ukweli yape muda, muda utafika tu.Kama yeye ndio Mr RIGHT atakuwa tu, usifanye haraka.
 
Fuata ushauri wa FL1 lakini usimpotezee na pia usithubutu kuingia kwenye ndoa haraka haraka, vuta subira kwa miaka kama miwili hivi kuona pumzi yake kama kweli ana mapenzi ya kweli au ni msanii tu. Kama kweli anakupenda kiasi cha kutaka uwe mkewe basi miaka miwili hataiona mingi hata kidogo.

Wel said BAK asijejuta kwa kutoa maamuzi ya haraka.....itasaidia kujipanga na kuendelea kusikiliza moyo wake unamwambia nini
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukiachana na mwenzio wa ndoa usingie mara moja kwenye ndoa nyingine kama sehemu ya kumkomoa mtu na kumwonyesha kuwa bado uko kwenye chati, maana watu wengine waliokuwa wakikumezea mate wanaweza kuchukulia nafasi hiyo kukupata na baadaye kukuacha, hapo utaona dunia chungu !!!! Chukua muda, tafakari yaliyotokea na kumpima kwa kina kila anayetangaza nia.
 
jamani ulikuwa kwenye mahusiano ya mateso haujapumzika unataka kuanzisha mengine???? Mhhh mi napata doubt na maamuzi yako yote kuanzia kuachana na huyo wa kwanza na huyu aliyekuwa mshauri wako ambaye anataka kubadilika na kuwa mumeo... Jipe muda bana pumzika ili hata kama ikiwa ni yaleyale uloyakimbia yasiwe yameungana... Ni hayo tu.
 
noella kwanza kabisa pole na hongera kwa ujasiri wa kuamua kuendelea na maisha yako ni wachache sana wenye ujasiri kama huo.
Pili, mtoto wako ana umri gani? Umesema una mwezi na nusu toka umesitisha uhusiano na baba mtoto, wewe binafsi huoni kuwa ni mapema sana kujiingiza kwenye mahusiano mengine licha hata ya kuwauliza wanaJF kwa ushauri?!unataka kuniambia wote hapa tukikwambia umkubali huyo jamaa wewe utaona ni sawa na utakubali kwasababu ya wengi wape???!!!

Nisamehe kama nitakua nimekukwaza lakini kwa jinsi nilivyokusoma ni kama na wewe umeanza kumfeel jamaa......kila la kheri mwaya.

Hujanikwaza Yummy ucjali.

Mwanangu ana miaka miaka mitatu. Kwakweli sijaingia kwenye mahusiano na sipo tayari kwa sasa, nimeomba mawazo yenu kwani mi naona hii situation imekaa strange kidogo kwangu.kwanza ni rafiki ambaye sijawahi kumuwazia hayo mambo, pili ni mdogo kwangu tatu yeye mawazo yake yako mbaali kwenye ndo nikimjibu vinginevyo baasi nimenuniwa for that day.
 
jamani ulikuwa kwenye mahusiano ya mateso haujapumzika unataka kuanzisha mengine???? Mhhh mi napata doubt na maamuzi yako yote kuanzia kuachana na huyo wa kwanza na huyu aliyekuwa mshauri wako ambaye anataka kubadilika na kuwa mumeo... Jipe muda bana pumzika ili hata kama ikiwa ni yaleyale uloyakimbia yasiwe yameungana... Ni hayo tu.

Maege hujanielewa, hapa nilipo nina furaha na amani na sihitaji mtu kwa sasa. ni maoni tu nahitaji nyie mwaionaje hii?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom