Hatimaye nimeweza,ila kuna jipya...

Pole dada kwa yaliyokukuta na hongera kwa kuepusha msongamano na kuamua kujiweka pembeni. Huyo side B naomba muendelee kuwa marafiki tu, hata kama yeye anazungumzia masuala ya ndoa, wewe ni mwanamke bado unaweza kumpa majibu mazuri tu amabyo hayatamkwaza. Naungana na member wengine wote waliosema utulie kwanza, jipe muda atleast hata mwaka hivi ndo uanze kuangalia masuala ya mahusiano tena, sawa mwanangu? (Mwanangu coz unajina kama la mwanangu) Mungu akutangulie ma babygirl
 
Hujanikwaza Yummy ucjali.

Mwanangu ana miaka miaka mitatu. Kwakweli sijaingia kwenye mahusiano na sipo tayari kwa sasa, nimeomba mawazo yenu kwani mi naona hii situation imekaa strange kidogo kwangu.kwanza ni rafiki ambaye sijawahi kumuwazia hayo mambo, pili ni mdogo kwangu tatu yeye mawazo yake yako mbaali kwenye ndo nikimjibu vinginevyo baasi nimenuniwa for that day.

Ok, ushauri wangu ni kuwa mlee kwanza mwanao hakikisha mapenzi yako yoote na jitihada zako zooote ni kwaajili ya mwanao hayo mengine yatafuata baadae sana. Kaa na huyo kijana mueleze kwa upendo kuwa kwa sasa hauko tayari kuingia kwenye mahusiano ya aina yoyote ile hivyo basi unamuomba muendelee na urafiki wenu lakaini kama hawezi kufanya hivyo basi na huo urafiki ufe maana hauko tayari kununiwa nuniwa kama watoto wadogo bana.
Kuhusu umri wake wala usikutie wasiwasi, hebu jaribu kufikiria huyo uliyekua nae mwanzo alikua na umri gani na alikutenda kiasi gani???!!! Unaweza kuwa na zeee zima lakini akili kama mtoto wa miaka saba:puke:
 
Asante kwa ushauri ila hata iweje na Mungu aniepushie siwezi kumrudia jamani duuh huwezi jua what i went through. for now nina concentrate na maisha yangu na mwanangu tu.

Kami ni hivyo basi ngoja tumwachie Allah asimame katikati yako na akuepushe na maswaibu ya mapenzi.
 
boys are opportunist ameona upo kwny broken heart anataka kutumia nafasi hiyo....,tuliza akili mama naniii bado mapema sana.....by da way pole sana
 
what if akibadirika na ukaona kabisa kabadirika, kuna tatizo gani la kurudiana nae mzazi mwenzako? Au usikute kijana rafiki yako alitia sumu kali hadi huwezi kusamahe. Ni vizuri sana kukaa na baba wa mtoto wako.. huwezi jua huyu jamaa atakuja kukaa vipi na mwanao.. sasa hivi anaweza ku act akitaka tunda, akikutia mikononi ndo utajua haswa yuko vipi.Tumia muda huu kumsoma na uwe makini sana.Mimi mwanaume najua tunapotaka kuua tuna fanya nini.. we can do anything... na kwa wewe sasa hivi uko vulnerable kwani umetoka kwenye maumivu moyo wako unahitaji pumziko, na pia mwili wako soon utahitaji kupozwa kama bado.

kubadilika kwake kunahitaji maombi aisee maana mh iko kwenye damu.akibadilika niko tayari kumrudia
 
Pole dada kwa yaliyokukuta na hongera kwa kuepusha msongamano na kuamua kujiweka pembeni. Huyo side B naomba muendelee kuwa marafiki tu, hata kama yeye anazungumzia masuala ya ndoa, wewe ni mwanamke bado unaweza kumpa majibu mazuri tu amabyo hayatamkwaza. Naungana na member wengine wote waliosema utulie kwanza, jipe muda atleast hata mwaka hivi ndo uanze kuangalia masuala ya mahusiano tena, sawa mwanangu? (Mwanangu coz unajina kama la mwanangu) Mungu akutangulie ma babygirl

sawa mummy asante sana kwa ushauri
 
Asanteni wote kwa michango yenu, inanisaidia kwa namna moja au nyingine.mbarikiwe
 
noella pole kwa hii situation,

Pamoja na kwamba ndio inabidi ujipe muda of which I agree completely, sikubaloiani na wazo la kwamba huyo rafiki yako wa sasa eti ni ka boy tu, ana ajenda ya siri, anataka kuku do tu baasi...inawezekana pia kuwa anakupenda. Nimependa kuna sehem umesema huwezi kupredict your future....so huwezi kupredict pia ur love....
 
Last edited by a moderator:
kubadilika kwake kunahitaji maombi aisee maana mh iko kwenye damu.akibadilika niko tayari kumrudia

nini nini hicho kilico kwenye damu, noella weka wazi hapa kuna watu wengi engine wamewahi kuwa na issue kama yako na wameweza kutatua, sidhani kama kuna tatizo ambalo ni wewe wakwanza kulipata.. na hamna anayekujua weka wazi feel free.
 
kwanza kabisa hatukuwa tumeoana, tulizaa na kila mmoja aliishi kivyake, kila siku ni ahadi tuu mwakani mwakani nikiaccomplish hiki nikiaccomplish kile.tatizo ni kwamba yeye ni mtu wa kugomba tuu for no good reason,hata ufanye nini kizuri ye anagomba, ni mtu anagombana mpaka na ndugu zake na anaweza asiongee nao hata mwaka mzima, ni mtu anaweka kinyongo for years, ni mtu muongo anapenda kuishi maisha artificial na kudanganya marafiki sometimes hata ndugu so siku akisahau kuniambia ni kwamba ninapata aibu kwa maana nitasema vinginevyo.ni mtu wa kusikiliza maneno ya kijiweni then ana apply kwangu, kwa mfano alianzisha tabia ya kunipiga then baadae akaconfess kwamba alisikiliza maneno ya kijiweni wakisema mwanamke usipompiga hatokuheshimu.ni mtu ambaye haoni tofauti ya mkwe na rafiki anadiriki kutuma msg za ajabu ajabu kwa mama yangu mzazi na ndugu zangu pale tunapokuwa tumehitilafiana mpaka nikaambiwa "huyu mtu hakufai" wakati angekaa kimya hakuna mtu angejua weakness zake zaidi yangu mimi. Ndo maana nikasema labda kwa maombi.
 
Subiri,Usifikiri una bahati na huyo kijana... Mwambie akupe muda tnx mrefu kutafakari yaliyotokea. na ndio uwaze chungu kipya... Angelia unaweza kurudi hapo hapo kwa zamani. Mapenzi ni ajabu sana..
 
Du pole sana.... Mungu akusaidie... kwani mpk karne hii kuna. mtu anapiga Mke..... lol.
 
kwanza kabisa hatukuwa tumeoana, tulizaa na kila mmoja aliishi kivyake, kila siku ni ahadi tuu mwakani mwakani nikiaccomplish hiki nikiaccomplish kile.tatizo ni kwamba yeye ni mtu wa kugomba tuu for no good reason,hata ufanye nini kizuri ye anagomba, ni mtu anagombana mpaka na ndugu zake na anaweza asiongee nao hata mwaka mzima, ni mtu anaweka kinyongo for years, ni mtu muongo anapenda kuishi maisha artificial na kudanganya marafiki sometimes hata ndugu so siku akisahau kuniambia ni kwamba ninapata aibu kwa maana nitasema vinginevyo.ni mtu wa kusikiliza maneno ya kijiweni then ana apply kwangu, kwa mfano alianzisha tabia ya kunipiga then baadae akaconfess kwamba alisikiliza maneno ya kijiweni wakisema mwanamke usipompiga hatokuheshimu.ni mtu ambaye haoni tofauti ya mkwe na rafiki anadiriki kutuma msg za ajabu ajabu kwa mama yangu mzazi na ndugu zangu pale tunapokuwa tumehitilafiana mpaka nikaambiwa "huyu mtu hakufai" wakati angekaa kimya hakuna mtu angejua weakness zake zaidi yangu mimi. Ndo maana nikasema labda kwa maombi.

i see, OK basi mbona hapo mimi sioni shida, nilidhani mlikuwa mume na mke.. Kwa hapo na namna ulivyoeleza kama ni hivyo huyo jamaa inaonekana ana matatizo. Ushauri wangu ni kuwa wewe tulia kwa muda, jaribu kupunguza ukaribu sana na huyo kijana mpya, ukiwa unamsoma kama utaona yuko OK, then muoane. Ila chukua muda kumsoma ili ujuridhishe usije kuumia tena.
 
We dada kama nimkubwa kama unavyodai hebu tumia ukubwa wako hapo.usikurupuke wala usiharakie maisha,huyo jamaa yako atawachinja.tuliza jazba muda ukifika kaeni chin na baba mtoto myajenge upya.
 
Angalia asijkuwa mbwa mwitu aliyejivisha ngozi ya kondoo! Maana naona unampa misifa kibao shauri yako, yametukuta hayooo
 
Kumbuka una mtoto mtafute mume wako acha tamaa utakuja kujuta tamaa mbaya.
 
katika safari wengi ni rahisi kuona mwanzo, lakini hakuna ajuaye mwisho. tungekuwa na uwezo wa kuona mwisho hakuna ambaye angeanza safari."
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom