Hatimaye nimepanda daraja kazini

Huyu mama ni muungwana sana, watumishi wameteseka sana miaka kibao bila kupanda madaraja, ilifika hatua suala la madaraja ikawa kama ni hisani tu na ni utashi wa mtawala, mwanzoni mwa mwaka jana niliongea na Afisa mmoja kuhusu suala la madaraja alichokisema ni kwamba kwa miaka ya hivi karibuni usitarajie mtumishi chini ya miaka 7/8 kupanda daraja, kauli hii ilikuwa ngumu sana kuiamini lakini hali ilikuwa hivyo.... ghafla upepo umebadilika ndani ya miezi 4 tu maumivu yamebaki historia
 
Mkuu kwani huu uzi utakuwa wa walimu siyo!....... Maana unauliza anafundisha wapi ikiwa hakuna mahali ameandika kama yeye ni Mchezea vumbi la chaki.
Anajua kila mtumishi wa serikali n Mwalimu.
 
Mnavyoshukuru utadhani ni hisani mmefanyiwa kumbe ni haki yenu ya kikatiba.
 
Haunishindi mimi kwa kupanda madaraka, daraja la mfugale nimepanda,daraja la kijazi nimepanda,na hata la kigamboni nimepanda
 
Back
Top Bottom