Mkuu shetani kanikamata nikiruka mkojo nakanyaga mavi. Bora ninywe niangalie plan B ya uhakika nikipata niache maana pombe inanigarimu nilienda kwenye kikao.cha harusi Ndugu wa mfanyabiashara mwenzangu baada ya kunywa nikaidi 500,000 mchango baada ya mwenzangu kuahidi 1,500,000 hasara nikubwa nikiandika Ni kitabu.
Kuna siku naanza biashara Kuna mtu nilikuwa namdai mda mrefu ile amenilipa nikafrai nikasema acha nitumie 50,000 maana alitoa 450,000 matokea yake nikaichoma yote saa nne usiku mpaka saa tano asubui.
Siku ingine nimetoka kwenye msiba nikatoa usafiri zile kurupushani maana usiku ulikuwa Kama.wangu Ni mtu nilikuwa nafanya nae kazi na kwao hamna hela nikatoa gari mbili ili zishughulikie msiba nikawa sijala hiyoo Ni saa Saba nikaenda kusaka msosi msosi unachelewa nikapiga vyombo mpaka naondoka saa 9 nikakamatwa na maaskari nikawatukana nikalala ndani. Yani pombe inanitesa lakina Bado sijapata mbadala