ndugu hivi karibuni nilikuja na nyuzi za kulalamika kuhusu matatizo yalionikumba.
ISSUE ILIKUA HIVI
nilikua kwenye gari binafsi natoka arusha kwenda iringa.nilikua na kiasi cha pesa kwenye gari kama 45 million kwa ajili ya shamba na kununua gari mtu anayeniuzia yupo iringa na ndiye aliyenichezea mchezo.
baada ya kufika iringa tuliuziana gari nilimpa million 12 nkabakiwa na33 million.usiku huo nililala kwa huyo jamaa aliyeniuzia gari nkaamka na kuanza safari nikiwa na gari niliyoinunua kwenda kununua drip pipe za shambani nikiwa njiani kwanza nilikamatwa kwa kosa la gari kuwa na spotlight.pili nilikuwa sina leseni(umri wangu mdogo ulichangia mimi kusumbuliwa zaidi).nililipa faini na kuondoka kwa speed kali nikiwa na hasira.kufika eneo la tanangozi mbele yangu kulikuwa na gari kubwa na kuna njiapanda inapandisha juu mkono wa kulia kuna jamaa alikuwa na noah ghafla baada ya gari kubwa kupita akaingia barabarani kwa kuwa nilikua kasi sana nikamgonga ubavuni gari yake ikarushwa ng'ambo ya barabara.yangu ikachomoka tyre la upande wa kulia na ikaendelea kwenda na mbele kuna basi la New force limesimama.gari ilikuwa inavutia barabara nikajtahidi kuitoa ikaenda kupindukia kwenye kabonde kushoto .nliumia uti wa mgongo nikachubuka na mkononi kidogo.basi maaskari wakaja kupima pale wakakuta mi sina leseni na yule jamaa wa kwenye noah hana leseni mi nkapelekwa hospitali.matatizo yalianza kwani niliibiwa pesa zangu zote pale kwenye ajali.lakini cha kushangaza yule jamaa aliyeniuzia gari alichukua gari lile na kwenda kulitengeneza huku akiwaambia watu sikumpa hela yote hivyo bado ananidai.wiki mwanamke wangu(sijamuoa ni msichana nilikuwa naishi nae tu kishkaji)eti akauza baadhi ya vitu na kurudi kwao bukoba.kwa kweli nilichanganyikiwa pesa niliyoitafta kwa shida leo narudi kuwa fukara.
baada ya kuandika uzi hapa nikiomba msaada kuna jamaa ni wakili.alinisaidia kunihamisha hospital na nilivyoruhusiwa baada ya kutoka alinipa pesa za kuanzia upya maisha kama laki tatu hivi.
Namshukuru mungu nipo mtaani napambana upya ila Koku bado nakupenda Mumy uje tuishi pamoja.
Raymond gari nilikumalizia hela yote sikutaka tuandikishane sababu nakujua ila nakudai unasema nikupe million saba,ya nini bro? ntakachokufanyia hutonisahau bado napambana na maisha upya ila kaa ukijua ntapambana na wewe hata ukiwa maiti.kitu ntakachokufanyia itabaki historia kwa kizazi chako chote sitakuacha Salama,nakuahidi ukoo wako wote watanilaumu kwa ntakachokifanya