Hatimaye na Mimi yamenikuta

Hujawahi kusikia mtoto wa tajiri ni mwizi?
 
Mbona hivo mnatukatisha tamaa sisi ambao hatujaoa, sometime muwe mnatupa mambo mazuri yanayopatikana kwenye ndoa na sio story ya kukatishana tamaa,
Mkuu ndoa ni tamu Sana. Ila Uvumilivu, maarifa na busara inatakiwa sababu changamoto ni nyingi. Hapa tunaelimishana na kupeana uzoefu. Na changamoto kubwa ya ndoa nyingi Kwa sasa ni michepuko. Hivyo Kama umeamua kuingia kwenye ndoa changa karata zako vizuri.
 
Kupitia mawasiliano yake ( texts na voice calls) Mkuu sadly I was too late
 
Unaona wife wako kama umemuonea kumpuga kwa uzinzi, hata mimi ninakiri umemuonea.

Ndiyo maana umemuacha kishingo upande huku unajilaumu, roho inakusuta.

Ujue wengi wanaingia kwenye ndoa kwa madhumuni zaidi ya upendo ama ngono pekee.

Manufaa ya ndoa ni pamoja na kusaidiana mambo makubwa na madogo ya kimaisha, kupanuana akili na kushauriana, pamoja na kulindana nk nk.

Sasa mmoja wenu akikengeuka jambo flani mojawapo katika muunganiko wenu, yakupasa kurudi nyuma na kukaa naye chini kurekebisha dosari hiyo.

Mke ama mume haachwi kwa kosa moja, kama niivyo pasingekuwepo na ndoa za watu hadi kuzeeshana sasa!

Tayari hapo ulishauvaa uhakimu, umemuhukumu mwenzako saazingine kwa makosa yale yale unayopenda wewe kuyafanya.

Fikiria mara mbilimbili mrudie mkeo, kwa misukusuko ulompatia bila shaka atajirekebisha.
 
Nimekaa kwenye ndoa muda sasa nilichojifunza ni kuwa mke hukinaisha, na mume huchokwa, au kwa ufupi binadamu tunakinai.

Watoto, Busara, hofu ya MUNGU, hofu ya taswira yako katika jamii, upendo uliopo sababu ya kuzoeana baada ya kuishi miaka mingi pamoja na ukomavu wa akili ndio hushikilia ndoa.

Haya mambo ni nadra sana kuyapata kwa binadamu mwenye age ya 20's ndio maana haishauriwi kuwahi kuoa.
 
Mwanamke akishazini ukathibitisha hafai tena kuwa mke. HUYU HAFAI TENA, HAKUNA NDOA HAPO HATA AKIMSAMEHE.

Wanawake waliopitia mafunzo kutoka kwa mabibi na mashangazi wanaelewa akili ya mwanaume linapokuja suala la fumanizi na ndio maana hata akichepuka hawezi ruhusu ijulikane kizembe.

Mwanamke yoyote mwenye akili na mkomavu wa nyonga na fikra, aliyepitia mafunzo ya matunzo ya mume hawezi kamatwa akizini.

Ikitokea akakamatwa kwenye hayo mazingira yanayopelekea kuhisi labda amezini huwezi thibitisha alikuwa akizini hata ww uliyelala naye huwezi thibitisha kirahisi kuwa umemlala.

Huyo ndo mwanamke aliyekuzwa akijua kuilinda ndoa yake na kulinda heshima ya mume wake, wana akili kubwa sana ya kupanga kuchepuka. Mazingira yote anaandaa yeye na huwezi mshika kizembe.

Hawa wa siku hizi hawakai na shangazi zao wanajifunza kwenye matv tu ndio maana wanafumaniwa fumaniwa tu. Siku hizi kutembea na mke wa mtu ukafumaniwa imekuwa rahisi sana.
 
Aliokwambia hela ni kama Solex kwenye chupi ya mkeo ni nani? Ukitaka usichapiwe tengeneza selo umfungie mkeo asitoke nje mpaka unaporudi toka mihangaikoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…