sasa hebu fafanua vizuri ni ipi njia sahihi kuitumia ili tuepukane na kuibiwa kupitia njia hii uliyoeleza?Hapo nyuma kidogo Wakili Msomi Bashir Yakub alileta uzi wake akitujulisha anapanga kuishtaki mitandao ya simu hapa nchini kwa mada zake kubwa tano (5) alizoziainisha. Hakusita kutoa mrejesho wa kila hatua ya shauri lake ulivyokuwa unaendelea.
Naona moja ya shauri lake limefanyiwa kazi. Jana nimepokea sms toka mtandao wa Vodacom Tanzania ukinitaka nikasitishe matumizi ya muda wa maongezi kwenye kupiga simu, internet na sms. Sikuhitaji degree 4 kufanya hivyo, nikaenda menu yao na kufuata muongozo walionipa. Matokeo yake sasa hivi sina hofu ya kutumia/kukomba kasalio kangu ili wasije kakata nikimaliza bando!.
Hatua nilizopewa ni:-
> *149*01#
> 11 (Huduma Xtra)
> 09 (Matumizi bila bando)
> 02 (Sitisha matumizi bila bando).
Ni kwamba sasa hivi ukiwa na vocha kwenye simu halafu hujajiunga kifurushi, basi hautaweza piga simu, tumia internet wala tuma sms mpaka ujiunge bando unalotaka!. Hii ni hatua nzuri sana, binafsi nakushukuru Wakili Msomi Bashir Yakub!. Heri yako kuliko wale bush lawyers wanaotusainisha mikataba ya Mangungo!.
Nasubiri na lile shtaka la bando kutoexpire!.
(kwa mathomaso hakuna screenshot sms ipo kwenye kitochi!.)
wako consumer right lakini utawasikia labda kama kuna maonyesho vinginevyo wamekaa tu bila kufanya chochote sasa hivi airtel wanatufungia huduma huwezi kupiga simu pamoja naa kwamba kila kitu kiko sawa customer care yao haipatikani ni shida tuUshindi mkubwa sana huu. Consumer protection groups and activism ni muhimu sana.
Mara nyingine hili ni muhimu kuliko siasa za vyama vya upinzani.
Bila ya grassroots organization kwenye hili, huko kwingine kwenye siasa na vigumu kujipanga.