Hatimaye moja ya shtaka la Wakili Msomi Bashir Yakub limefanyiwa kazi na mtandao wa Vodacom!.

Wick

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
8,313
12,123
Hapo nyuma kidogo Wakili Msomi Bashir Yakub alileta uzi wake akitujulisha anapanga kuishtaki mitandao ya simu hapa nchini kwa mada zake kubwa tano (5) alizoziainisha. Hakusita kutoa mrejesho wa kila hatua ya shauri lake ulivyokuwa unaendelea.
Naona moja ya shauri lake limefanyiwa kazi. Jana nimepokea sms toka mtandao wa Vodacom Tanzania ukinitaka nikasitishe matumizi ya muda wa maongezi kwenye kupiga simu, internet na sms. Sikuhitaji degree 4 kufanya hivyo, nikaenda menu yao na kufuata muongozo walionipa. Matokeo yake sasa hivi sina hofu ya kutumia/kukomba kasalio kangu ili wasije kakata nikimaliza bando!.
Hatua nilizopewa ni:-
> *149*01#
> 11 (Huduma Xtra)
> 09 (Matumizi bila bando)
> 02 (Sitisha matumizi bila bando).
Ni kwamba sasa hivi ukiwa na vocha kwenye simu halafu hujajiunga kifurushi, basi hautaweza piga simu, tumia internet wala tuma sms mpaka ujiunge bando unalotaka!. Hii ni hatua nzuri sana, binafsi nakushukuru Wakili Msomi Bashir Yakub!. Heri yako kuliko wale bush lawyers wanaotusainisha mikataba ya Mangungo!.
Nasubiri na lile shtaka la bando kutoexpire!.

(kwa mathomaso hakuna screenshot sms ipo kwenye kitochi!.)
 
Mimi kilio changu hiki hapa... Je hizi msg naweza kuzibadili kwa internet bundle...
Hapo nyuma kidogo Wakili Msomi Bashir Yakub alileta uzi wake akitujulisha anapanga kuishtaki mitandao ya simu hapa nchini kwa mada zake kubwa tano (5) alizoziainisha. Hakusita kutoa mrejesho wa kila hatua ya shauri lake ulivyokuwa unaendelea.
Naona moja ya shauri lake limefanyiwa kazi. Jana nimepokea sms toka mtandao wa Vodacom ukinitaka nikasitishe matumizi ya muda wa maongezi kwenye kupiga simu, internet na sms. Sikuhitaji degree 4 kufanya hivyo, nikaenda menu yao na kufuata muongozo walionipa. Matokeo yake sasa hivi sina hofu ya kutumia/kukomba kasalio kangu ili wasije kakata nikimaliza bando!.
Hatua nilizopewa ni:-
> *149*01#
> 11 (Huduma Xtra)
> 09 (Matumizi bila bando)
> 02 (Sitisha matumizi bila bando).
Ni kwamba sasa hivi ukiwa na vocha kwenye simu halafu hujajiunga kifurushi, basi hautaweza piga simu, tumia internet wala tuma sms mpaka ujiunge bando unalotaka!. Hii ni hatua nzuri sana, binafsi nakushukuru Wakili Msomi Bashir Yakub!. Heri yako kuliko wale bush lawyers wanaotusainisha mikataba ya Mangungo!.
Nasubiri na lile shtaka la bando kutoexpire!.

(kwa mathomaso hakuna screenshot sms ipo kwenye kitochi!.)
Msg million sita kasoro
Screenshot_20191215-103925.jpeg

Jr
 
Safi sana kwa wakili na vodacom kusikiliza malalamiko na kuyafanyia kazi.
 
Back
Top Bottom