Hatimaye moja ya shtaka la Wakili Msomi Bashir Yakub limefanyiwa kazi na mtandao wa Vodacom!.

Ushindi mkubwa sana huu. Consumer protection groups and activism ni muhimu sana.

Mara nyingine hili ni muhimu kuliko siasa za vyama vya upinzani.

Bila ya grassroots organization kwenye hili, huko kwingine kwenye siasa na vigumu kujipanga.
 
Yani umeshidwa kuelewa maeleza rahisi namna hiyo sasa utaelewa nini.

Hahahahaa!

Fahamu kuwa kila mtu ana kiwango chake cha kuchanganua mambo na kuelewa pia. Hatuwezi kufanana. Kuna pia utofauti katika kuzingatia wakati wa kusoma. Kuna watu hawana uwezo mzuri wa ku concentrate wakati wa kusoma. Na kuna sababu nyingine pia zinaweza kuathiri uwezo wa mtu kuelewa kwa wakati flani. Mfano, unaweza kukuta mtu ana jambo limemsonga kichwani halafu anasoma hapa, inaweza kuwa ni kitu rahisi lakini asielewe pia.

Yote kwa yote, tambua walioweka mipaka kitaaluma na katika elimu walifanya tafiti na kugundua kuwa binadamu wanatofautiana sana katika uwezo wa kufikiri kutokana na sababu mbalimbali. Kwahiyo usishangae.
 
Hapo nyuma kidogo Wakili Msomi Bashir Yakub alileta uzi wake akitujulisha anapanga kuishtaki mitandao ya simu hapa nchini kwa mada zake kubwa tano (5) alizoziainisha. Hakusita kutoa mrejesho wa kila hatua ya shauri lake ulivyokuwa unaendelea.
Naona moja ya shauri lake limefanyiwa kazi. Jana nimepokea sms toka mtandao wa Vodacom Tanzania ukinitaka nikasitishe matumizi ya muda wa maongezi kwenye kupiga simu, internet na sms. Sikuhitaji degree 4 kufanya hivyo, nikaenda menu yao na kufuata muongozo walionipa. Matokeo yake sasa hivi sina hofu ya kutumia/kukomba kasalio kangu ili wasije kakata nikimaliza bando!.
Hatua nilizopewa ni:-
> *149*01#
> 11 (Huduma Xtra)
> 09 (Matumizi bila bando)
> 02 (Sitisha matumizi bila bando).
Ni kwamba sasa hivi ukiwa na vocha kwenye simu halafu hujajiunga kifurushi, basi hautaweza piga simu, tumia internet wala tuma sms mpaka ujiunge bando unalotaka!. Hii ni hatua nzuri sana, binafsi nakushukuru Wakili Msomi Bashir Yakub!. Heri yako kuliko wale bush lawyers wanaotusainisha mikataba ya Mangungo!.
Nasubiri na lile shtaka la bando kutoexpire!.



(kwa mathomaso hakuna screenshot sms ipo kwenye kitochi!.)
sasa hebu fafanua vizuri ni ipi njia sahihi kuitumia ili tuepukane na kuibiwa kupitia njia hii uliyoeleza?
hii matumizi bila bando inamaanisha nini na inasaidiaje ukiitumia?
 
Hili tuzidi kuwamini watoke hadharani watangaze hivyo na watoto kwenye uwo mfumo wa zamani tuanze upya,sio wote wanaoweza kaolewa hayo maelezo yao hasa wazee
 
Ushindi mkubwa sana huu. Consumer protection groups and activism ni muhimu sana.

Mara nyingine hili ni muhimu kuliko siasa za vyama vya upinzani.

Bila ya grassroots organization kwenye hili, huko kwingine kwenye siasa na vigumu kujipanga.
wako consumer right lakini utawasikia labda kama kuna maonyesho vinginevyo wamekaa tu bila kufanya chochote sasa hivi airtel wanatufungia huduma huwezi kupiga simu pamoja naa kwamba kila kitu kiko sawa customer care yao haipatikani ni shida tu
 
46 Reactions
Reply
Back
Top Bottom