Cicadulina
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 1,006
- 2,431
“Nilikwenda Nairobi, nikamuita Halima Mdee, akasafiri na Ester Bulaya. Nimekuwa nao siku 7 nikimshawishi Halima anieleze nini kilitokea, aligoma. Nikamuomba aache huo ubunge, nimemtafutia kazi Nairobi na RSA na atalipwa US$15,000 (Shs. 34.9M), Halima akagoma”.
“Halima ananiuma kwa sababu nyingi. Halima nimemtoa chuo kikuu akiwa msichana. Nimempika kwa gharama sana. Ndiyo maana nilitumia juhudi zangu zote hata kuwaita wazazi wake, wamshawishi aachane na ubunge wa damu wa Magufuli, anaharibu career yake, hakunielewa”.
“Nairobi nilipowaita Halima na Bulaya nilikuwa nakutana nao kila siku. Tunakula na kunywa pamoja. Nikimbembeleza Halima aachane na ubunge wa damu, mtetezi ni Magufuli, hayupo. Nikamuomba anieleze nini kilitokea, Hawakuwahi kunieleza hadi naondoka kwenda Dubai”.
“Kama haya nayoeleza hapa kuhusu Halima nadanganya, Halima yupo hapa asimame na aseme kama ni uongo. Akanushe kuwa sikumtafutia kazi NRB na RSA alipwe Shs. 34.9M, au kama sikuzungumza na wazazi wake, au sikumuita NRB kumshawishi aachane na ubunge wa Magufuli”.
“Siyo kazi rahisi kufukuza wanawake 19 ambao umewajenga kwa gharama, wapo wote mbele ya baraza kuu, nitawaomba sasa dada zangu hawa, aliye na jambo la kuzungumza asogee mbele asemee”.
Baada ya hapo mwenyekiti Freeman Mbowe akawaambia wajumbe “nadhani dada zangu wameona hawana kitu cha kuongea na wajumbe wa baraza kuu, mheshimiwa katibu mkuu, sasa nikuombee tuendelee na taratibu za kitaasisi, tusikilize rufaa zao na tufikie maamuzi” Wajumbe wakapiga kura!