Hatimaye Mbowe atoa ya moyoni kuhusu Halima Mdee

images (46).jpeg
WAHUNI wanajuana.
 
“Nilikwenda Nairobi, nikamuita Halima Mdee, akasafiri na Ester Bulaya. Nimekuwa nao siku 7 nikimshawishi Halima anieleze nini kilitokea, aligoma. Nikamuomba aache huo ubunge, nimemtafutia kazi Nairobi na RSA na atalipwa US$15,000 (Shs. 34.9M), Halima akagoma”.

“Halima ananiuma kwa sababu nyingi. Halima nimemtoa chuo kikuu akiwa msichana. Nimempika kwa gharama sana. Ndiyo maana nilitumia juhudi zangu zote hata kuwaita wazazi wake, wamshawishi aachane na ubunge wa damu wa Magufuli, anaharibu career yake, hakunielewa”.

“Nairobi nilipowaita Halima na Bulaya nilikuwa nakutana nao kila siku. Tunakula na kunywa pamoja. Nikimbembeleza Halima aachane na ubunge wa damu, mtetezi ni Magufuli, hayupo. Nikamuomba anieleze nini kilitokea, Hawakuwahi kunieleza hadi naondoka kwenda Dubai”.

“Kama haya nayoeleza hapa kuhusu Halima nadanganya, Halima yupo hapa asimame na aseme kama ni uongo. Akanushe kuwa sikumtafutia kazi NRB na RSA alipwe Shs. 34.9M, au kama sikuzungumza na wazazi wake, au sikumuita NRB kumshawishi aachane na ubunge wa Magufuli”.

“Siyo kazi rahisi kufukuza wanawake 19 ambao umewajenga kwa gharama, wapo wote mbele ya baraza kuu, nitawaomba sasa dada zangu hawa, aliye na jambo la kuzungumza asogee mbele asemee”.

Baada ya hapo mwenyekiti Freeman Mbowe akawaambia wajumbe “nadhani dada zangu wameona hawana kitu cha kuongea na wajumbe wa baraza kuu, mheshimiwa katibu mkuu, sasa nikuombee tuendelee na taratibu za kitaasisi, tusikilize rufaa zao na tufikie maamuzi” Wajumbe wakapiga kura!
Eti nitatafuta kazi ulipwe usd 15,ooommh labda kama kwenye kampuni yake
 
Kwanini wameshindwa kuomba msamaha yakaisha? Mbona kiburi sana ?

Wajifunze kwa wanasiasa wakongwe
 
alimtoa akiwa mwanafunzi au ana fundisha? huyu kaingia Chadema akitokea ofisi za umma kama mtumishi... wazazi wake ndio walikuwa chuo wakipiga vipindi (Nazani ni mzee mdee ndio alikuwa ana fundisha)

aweke wazi...
Yeye kasema alimtoa chuo na Halima hakutoa pingamizi
Wewe unataka unachowaza wewe ndo kiwe na sivyo alivosema ama?
Hivi watu wengine mnakulaga nini? Maana vichwa vyenu sijui vipoje khaaa
 
angekuwepo hayati mpendwa baba yetu makufuli yote haya yasingetokea jpm sasa hivi anakaa na yesu mbinguni
 
Mwendakuzimu alituharibia sana hawa dada zetu wapambanaji.

Tulipenda lile bunge liwe na chama kimoja tu
 
Yeye kasema alimtoa chuo na Halima hakutoa pingamizi
Wewe unataka unachowaza wewe ndo kiwe na sivyo alivosema ama?
Hivi watu wengine mnakulaga nini? Maana vichwa vyenu sijui vipoje khaaa
ukweli... msiwe mna danganywa...

Mh mbowe wewe yawezekana una msikia, mimi namfahamu tuna fahamiana... niishie hapo ndg mfuasi...
 
Halima alisafiri na Ester Bulaya hadi Nairobi. wakala bata wiki nzima na Mwenyekiti wao.
Kumbe kuna mengine yalifanyika nyuma ya pazia Ndio maana Halima anasema wahuni hao
 
Mbowe its a kind of a leader...more than a father & guardian achana na huo uenyekiti.

Namhurumia dogo aliyetolewa usiku gelezani Singida kwenda kupewa ubunge feki maskini.
 
Back
Top Bottom