Hatimaye Mbowe atoa ya moyoni kuhusu Halima Mdee

Hatimaye Mbowe atoa ya moyoni kuhusu Halima Mdee

Hata mi nimewaza sana hili
Kwanini baraza kuu halijaangalia kua tulikua kwwnye kupindi cha mpito
Maana mtawala likua ni herode
Nadhani wawasamehe tu bure na mambo mengine yaendelee..!

Ukisoma kwa makini bila kukurupuka ni kwamba ushauri huo wa mbowe alimpa halima baada ya magufuli kufa,

“Nairobi nilipowaita Halima na Bulaya nilikuwa nakutana nao kila siku. Tunakula na kunywa pamoja. Nikimbembeleza Halima aachane na ubunge wa damu, mtetezi ni Magufuli, hayupo."
 
Mbowe its a kind of a leader...more than a father & guardian achana na huo uenyekiti.

Namhurumia dogo aliyetolewa usiku gelezani Singida kwenda kupewa ubunge feki maskini.
Yaan yule saiz Angeula kirahis kutokana na hussle alizopitia. Lkn hkn ajuaye kësho. Walijua Magu ataendelea kuwepo so. Ndo hivyo Tena.
 
Mbowe anabusara sana.@pascal mayala unamaoni gani?
Mwanasheria na mwandishi wamchongo atasema nn atakachokwambia chadema imekosea kwani akina covid 19 walijenga chama kwajasho nadamu hatazami kwamba nguvu walizotumia kujenga chama ndonguvu zilezile zimetumika kusaliti chama
 
"Halima akasafiri na Ester Bulaya"....nimeelewa hapo tu, mengine hata sina muda nayo maana najua kila mwanasiasa ana dau lake la kununuliwa! Tukifukua makaburi ya pesa aliyopewa Mbowe na kubadiri gea angani Lowassa kubwa la mafisadi akawa msafi na kugombea urais asilalamike
Kwenye siasa hakuna adui wa kudumu ila kuna rafiki wa kumtengeneza ili malengo yatimie.
Nenda Kenya hapo... coalitions zinatengenezwa kila siku na watu wana defect kila siku kwenda wanapohisi kuna wafaa.
Tatizo Watanzania mnajenga urafiki au uadui na majina ya watu badala ya hoja zao!
Lowassa angetusaidia sana kuisambaratisha ccm.
Na itachukua muda sana kufika momentum tuliyokuwa nayo 2015.
 
Yaan yule saiz Angeula kirahis kutokana na hussle alizopitia. Lkn hkn ajuaye kësho. Walijua Magu ataendelea kuwepo so. Ndo hivyo Tena.
Hapa duniani huwezi kuishi muda mrefu ukiwa katili hivyo..kuua na kutesa watu kama Sauli.

.enzi za kale wafalme wakifanya makosa walimlilia Mungu sana ili waishi...mfano ni mfalme Daud wa Islael ambaye aliandika Zaburi huku akimlilia Mungu.
 
“Nilikwenda Nairobi, nikamuita Halima Mdee, akasafiri na Ester Bulaya. Nimekuwa nao siku 7 nikimshawishi Halima anieleze nini kilitokea, aligoma. Nikamuomba aache huo ubunge, nimemtafutia kazi Nairobi na RSA na atalipwa US$15,000 (Shs. 34.9M), Halima akagoma”.

“Halima ananiuma kwa sababu nyingi. Halima nimemtoa chuo kikuu akiwa msichana. Nimempika kwa gharama sana. Ndiyo maana nilitumia juhudi zangu zote hata kuwaita wazazi wake, wamshawishi aachane na ubunge wa damu wa Magufuli, anaharibu career yake, hakunielewa”.

“Nairobi nilipowaita Halima na Bulaya nilikuwa nakutana nao kila siku. Tunakula na kunywa pamoja. Nikimbembeleza Halima aachane na ubunge wa damu, mtetezi ni Magufuli, hayupo. Nikamuomba anieleze nini kilitokea, Hawakuwahi kunieleza hadi naondoka kwenda Dubai”.

“Kama haya nayoeleza hapa kuhusu Halima nadanganya, Halima yupo hapa asimame na aseme kama ni uongo. Akanushe kuwa sikumtafutia kazi NRB na RSA alipwe Shs. 34.9M, au kama sikuzungumza na wazazi wake, au sikumuita NRB kumshawishi aachane na ubunge wa Magufuli”.

“Siyo kazi rahisi kufukuza wanawake 19 ambao umewajenga kwa gharama, wapo wote mbele ya baraza kuu, nitawaomba sasa dada zangu hawa, aliye na jambo la kuzungumza asogee mbele asemee”.

Baada ya hapo mwenyekiti Freeman Mbowe akawaambia wajumbe “nadhani dada zangu wameona hawana kitu cha kuongea na wajumbe wa baraza kuu, mheshimiwa katibu mkuu, sasa nikuombee tuendelee na taratibu za kitaasisi, tusikilize rufaa zao na tufikie maamuzi” Wajumbe wakapiga kura!
Kumbe huko NRB ndiko mikakati ya kigaidi ilikofanyika?? Kuwashawishi vijana wa kitz kuacha kutumikia taifa lao, na kwenda kuwa wakimbizi nje ya nchi, huo si ugaidi jamani?
Kama kweli anahuruma basi awatafutien kazi watakapovuliwa ubunge!

Sent from my TECNO CA6 using JamiiForums mobile app
 
“Nilikwenda Nairobi, nikamuita Halima Mdee, akasafiri na Ester Bulaya. Nimekuwa nao siku 7 nikimshawishi Halima anieleze nini kilitokea, aligoma. Nikamuomba aache huo ubunge, nimemtafutia kazi Nairobi na RSA na atalipwa US$15,000 (Shs. 34.9M), Halima akagoma”.

“Halima ananiuma kwa sababu nyingi. Halima nimemtoa chuo kikuu akiwa msichana. Nimempika kwa gharama sana. Ndiyo maana nilitumia juhudi zangu zote hata kuwaita wazazi wake, wamshawishi aachane na ubunge wa damu wa Magufuli, anaharibu career yake, hakunielewa”.

“Nairobi nilipowaita Halima na Bulaya nilikuwa nakutana nao kila siku. Tunakula na kunywa pamoja. Nikimbembeleza Halima aachane na ubunge wa damu, mtetezi ni Magufuli, hayupo. Nikamuomba anieleze nini kilitokea, Hawakuwahi kunieleza hadi naondoka kwenda Dubai”.

“Kama haya nayoeleza hapa kuhusu Halima nadanganya, Halima yupo hapa asimame na aseme kama ni uongo. Akanushe kuwa sikumtafutia kazi NRB na RSA alipwe Shs. 34.9M, au kama sikuzungumza na wazazi wake, au sikumuita NRB kumshawishi aachane na ubunge wa Magufuli”.

“Siyo kazi rahisi kufukuza wanawake 19 ambao umewajenga kwa gharama, wapo wote mbele ya baraza kuu, nitawaomba sasa dada zangu hawa, aliye na jambo la kuzungumza asogee mbele asemee”.

Baada ya hapo mwenyekiti Freeman Mbowe akawaambia wajumbe “nadhani dada zangu wameona hawana kitu cha kuongea na wajumbe wa baraza kuu, mheshimiwa katibu mkuu, sasa nikuombee tuendelee na taratibu za kitaasisi, tusikilize rufaa zao na tufikie maamuzi” Wajumbe wakapiga kura!
Kwa hili Halima na wenzake watakuwa walionunuliwa kwa bei kubwa mno. Yaani Yule Dictator alichezea Kodi zetu mno katika kuua upinzani. Yaani mtoa hongo na Rushwa mkubwa Yule. Sasa nchi haina hela tinatembeza mabakuli na kuomba mikopo. Kweli Mungu ni fundi Sana. Asante Baba Mungu kwa kutuheshimisha March 2021.
 
Mbowe muungwana sn
Yaani ukweli sijawahi kuona kiongozi mwenye Busara kama Mbowe. Yaani kumbe nyuma ya pazia alifanya jitihada Sana kuwarudisha. Inaelekea walipewa pesa nyingi Sana na ahadi kibao pia nahisi walisaini mkataba wa kuwatisha wakijiuzulu au kukimbia nchi. Kweli pesa ina nguvu. Yaani Halima akakubali kupoteza sifa na nguvu kubwa ya Kisiasa aliyoipata kupitia Chadema? Poleni Sana CHADEMA. Ila malipo ni hapa hapa duniani.
 
alimtoa akiwa mwanafunzi au ana fundisha? huyu kaingia Chadema akitokea ofisi za umma kama mtumishi... wazazi wake ndio walikuwa chuo wakipiga vipindi (Nazani ni mzee mdee ndio alikuwa ana fundisha)

aweke wazi...
Mwanafunzi wa Sheria UDSM. Mdee ni Mwanasheria Mwanasiasa. Chadema walikuwa Makini Ku target vijana wenye brain na political aspiration then wakawajenga. Walikuwa wanapitia Vyuo vya Elimu ya Juu Ku target huko. Kama kina Zito na wengine wengi tu. Ndiyo maana unaona kama Chadema ina wasomi Fulani hivi.
 
Wameondoka. Sheria, kanuni, na taratibu za chama zimewabana.

Ila tumepoteza majembe aisee. Halima & CO mmetuangusha sana wafuasi wenu. Rudini mkaombe msamaha kwa umma wa chadema muwe wanachama wa kawaida.
Kweli kabisa. Wajishushe na nina Uhakika watasamehewa na maisha yataendekea na 2025 wangesimamishwa majimboni au viti maalum. Na uchaguzi utakuwa siyo uchafuzi na watashinda.
 
Mnyika,zitto,mdee

Recruit wa mbowe tangu wakiwa udsm

Zitto huko nyuma akishawahi sema hivi

Ni recruits wa mbowe yeye mwenyewe sababu kwanza walikuwaga viongozi DARUSO

zitto alikuwa PM na halima spika kama sikosei na kina mtatiro akiwa Rais sema mtatiro akakimbilia cuf.

So dogo nyamaza
Uko sahihi kabisa. Big up
 
Back
Top Bottom