Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 242
Naona kuna utata katika habari ya kwenye gazeti la mwananchi (hard paper vc online). ninaomba kunukuu sentensi zifuatazo kisha tujiulize ukweli ni upi:
Mwananchi online: "Habari zinasema kuwa Masauni alitakiwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake, lakini aligoma na kujitetea dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008"
Mwananchi hard Paper lililo mtaani: "Habari zinasema kuwa Masauni alijiuzulu saa mbili usiku baada ya kubanwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.
Swali: ukweli ni upi?
Shyrose ni mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM akitokea UWT(umoja wa wanawake tz),UVCCM pia wana mjumbe wao kwenye baraza kuu la UWT,ni utaratibu wao CCM.Mie nimeshangaa haswa,nakumbuka back 1997 nikiwa Ngaza Secondary huyu mdada alikuwa pale Nyegezi Social (SAUTI) akisoma na alikuwa kama kwenye mid 20's,kama mpaka sasa bado ni kijana,basi tena.
Mie nimeshangaa haswa,nakumbuka back 1997 nikiwa Ngaza Secondary huyu mdada alikuwa pale Nyegezi Social (SAUTI) akisoma na alikuwa kama kwenye mid 20's,kama mpaka sasa bado ni kijana,basi tena.
Ridhiwani uko wapi hebu chukua mikoba ya Masauni......!
ANOTHER BLUNDER YA JK.
Kuna blunders nyingi zilitajwa katika thread fulani, napenda na hii iongezwe kwani JK ndiye alimkingia kifua Masauni
Vyombo vya ushauri vinafanya kazi kweli? au JK ndiye hashauriki.
Kuna siku tutaamka na kuambiwa tuondoke TZ maana imeshauzwa sisi bila kujua!
Nikivaa hayo maguo ya kijani,MUNGU atanilaani !
Kwa hiyo Malisa atakaimu uenyekiti? Nasikia wazee wao wa CC wanakutana leo pamoja na mengine ku-deliberate juu ya hali hii. FMES uko wapi? Tunakumiss sana kwenye suala hili.
Haya ni makubwa sasa, Ningependa kuwaambieni kitu, wanompiga vita masauni na kumnyooshea vidole ningependa kuwauliza ndani ya UVCCM je kila mmoja wenu nae atupe umri wake wa kweli basi maaana najua fika ndani ya UVCCM ni wachache sana wenye umri mdogo kwani hii sheria nayo hajazingatiwa ukitizama ni vijana wachache sana katika nchi hii ndio wako UVCCM na wenye umri mdogo na wengi wao ni umri mkubwa sasa pia UVCCM nanyi hili mkalijadiri na umri uwe mwisho 35.
nimeona matukio mengi ya viongozi wa UVCCM ndio wanao jiuzulu lakin cha ajabu Masaun anachia ngazi kwa kosa la Umri je hao Viongozi wakuuwa CCM wano kutwa na kashafa nyingi na bado wako wanang'ang;ania madaraka ndani ya CCM au NEC je mbona hawaachii ngazi?
CCM kuna tatizo na inapaswa wakaechini wajichunguze sana na kwa makini wasije jisahau wakadhani hao viongozi wao ndio CCM hata kidogo wasije jidanganya yatakuja wakuta tu huko mbeleni.
Nilisha wambieni UVCCM ni hawana hata kauli mbiu NAPE alisema saaana na waka mdharau hao hao UVCCM hata kumuunga mkono wao wakapiga kimya hizo pesa za mafisadi na zinawachanganya sana na hamtokuja iongoza hii nchi amini nawambieni ninyi viongozi wa UVCCM mliopo kwasasa simameni na mjisimamie msingojee kuambiwa na mfanye jinsi hao wakubwa zenu watakavyo mtaburuzwa mpaka lini
Naomba kuuliza tu kwani kijana kwa mujibu wa UV SISI M ni miaka mingapi? na huyo Shy rose ni kijana? Ni swali tu!