Naomba kuuliza tu kwani kijana kwa mujibu wa UV SISI M ni miaka mingapi? na huyo Shy rose ni kijana? Ni swali tu!
Hapa tunajifunza nini?
Hapa tunajifunza nini?
Nikiangalia hizi picha sura zote zimekomaa? Hawa ni wazee au vijeba? Kiumbo wengi naona wana umri karibu sawa na Masauni
Mkuu niliguswa sana. Ila pia ukweli uko pale pale kwamba hata hili dude (linalojiita chama) limeua watu wengi sana wasio na hatia makusudi au kwa sera zake za kinyang'au.
Poa mkuu, tuko pamoja.
Hapa tunajifunza nini?
Umenena Mkuu, wengi hapo ni wangangaji wa njaa tu, we miaka 42 (Kijeba)unajiita UVCCM? teh teh teh. Siasa si mahala pa kukupa hela ya kula na familia yako - siasa ni wito.
Naona kuna utata katika habari ya kwenye gazeti la mwananchi (hard paper vc online). ninaomba kunukuu sentensi zifuatazo kisha tujiulize ukweli ni upi:
Mwananchi online: "Habari zinasema kuwa Masauni alitakiwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake, lakini aligoma na kujitetea dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008"
Mwananchi hard Paper lililo mtaani: "Habari zinasema kuwa Masauni alijiuzulu saa mbili usiku baada ya kubanwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.
Swali: ukweli ni upi?
Masauni anasema wanampinga kwa sababu ya msimamo wake wa kusimamia rasilimali za umoja. Kwa kauli hiyo utagundua ugomvi huu ni kwa sababu ya hela. Ufisadi unaanzia awali kabisa!
Ni tafsiri tu, nadhani sahihi ni kuwa awali Mwaka 2008 Masauni aliwahi kutakiwa kujiuzulu kutokana na Kashfa ya umri akagoma kujiuzulu, lakini leo amejiuzulu saa usiku kutokana na kashfa hiyo inayomkabili ambayo makamba aliwahi kumtaka ajiuzulu na kukataa. Nadhahi sahihi ni hivi kwa mawazo yangu.