Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

huyo ndo JK a.k.a KING'OTA, kutoka kijiwe cha SAIGON K.KOO, kama hamuelewi waulizen MBAYUWAYU (TUCTA) walipodai maslahi akawaahidi NGEU ZA POLISI.
 

Halafu wale wengine wale nani tena wale. Wale kule segerea wale nani tena waliimba ule wimbo "baba na mwana wanaimba na kucheza" walipofanya fyoko tu kifungo na hawa nao wafanyweje?
 
Douglas ndio tatizo la kutawaliwa na Wanajeshi, kila kitu kwao ni amri. Na always maneno yanakuwa mbele kabla ya kufikiri cha kusema. Najua mengi uliyasikia kwenye hotuba yake na wazee wa Dar (CCM). Ukiwa kama Rais huwezi kutushia watu eti mkiandamana polisi itawashughulikia, hiyo imeonyesha udhaifu mkubwa aliokuwa nao au wakuongozwa na Mjeshi.
 

Ha ha haaaaaaaaaaaa hii nimependa mkuu. Kweli ni full Rose Mhando mwanangu.
 
Hii nchi itaingia vitani,unless haya mambo mnayoyaleta humu ni uongo.
 
Kaburunye said:
Hata hivyo, Rais Kikwete alimfariji kijana huyo mpole na mzito kufanya maamuzi magumu na haraka, akisema kwakuwa ni makakamavu na mchapakazi atapangiwa kazi nyingine hapo baadaye. mwisho wa kunukuu (Source: Gazeti la mwananchi la leo 20 May 2010)

Kwani ni uzito wa kufanya maamuzi magumu ya haraka ndilo tatizo ama ni kughushi?hii ina justify ukweli kwamba walishapanga,na mwananchi ni la nani vile?Inawezekana walikuwa wamemweka hapo and they fell out,walimweka hapo mwanzoni wakidhani ni mjinga walipogundua sivyo wakamchomea mambo ya kughushi,na sasa pia hana akili na ni mzito kufanya maamuzi magumu,ila bado atapatiwa kazi ambayo ni ya kuwatumikia wananchi bila kutumia akili?
Haya mambo nshasema kama siamini vile,maana hakuna binadamu mwenye akili timamu ata comprehend,kama haya si ya uongo,machafuko ni very likely,unless ni kweli kila mtz ni mjinga?
 
Jamani,kwani mtu akikosea upande mmoja hawezi kufanya upande mwingine?Mimi sioni tatizo kama atapewa majukumu mengine lakini sio ya vijana...
 
GS: Usiniambie ndio unagundua leo!? Pole sana

Kitilla Mkuu,heshima mbele..Ndio nimegundua leo nini?mimi nashangaa tunavyojipa tabu kwa kumshangaa Rais kwa kusema kuwa Masauni atapewa makukumu mengine,mimi bainfasi sioni tatizo,kama amedanganya umri sio kigezo cha kufanya ashindwe kufanya majukumu mengine ilimradi tu awe na uwezo..Ingawa natambua suala la kughushi umri ni kosa na ni kweli amepoteza credibility lakini haamanishi hawezi kufanya kazi za chama chao tena..Huu ndio mtazamo wangu..
 
yaani wewe unadhani mtu mwongo ndio hana nafasi kwa CCM huyo ndio anawafaa zaidi,na ndio maana rais kakwambia atampangia kazi ingine.anajua pa kumuweka we ulie tu.yana mwisho haya:angry:

Hahahaa Mkuu unataka kusema hii ndiyo SIFA MAMA KWA MWANA CCM?
 
Baada ya tuhuma za Masaury.....
Then GS.....
Gender Sensitive said:
Jamani,kwani mtu akikosea upande mmoja hawezi kufanya upande mwingine?Mimi sioni tatizo kama atapewa majukumu mengine lakini sio ya vijana...
Kitila Mkumbo akaja.....
GS: Usiniambie ndio unagundua leo!? Pole sana

Kwahiyo chadema mtafanya the same?Poleni chadema
 
Kwahiyo chadema mtafanya the same?

Mkuu huu ni mtazamo wangu na sio wa chama,tafadhali usiingize chama hapa...msipende sana kuhukumu wenzenu wakatyi hata nyie mnadhambi kibao,hebu kuweni wa kweli kidogo..
 

Kwenye uchaguzi wa UWT Janeth Kahama alilalama weeee kwamba Sofi anatumia rushwa na kwamba anawaambia wagombea yeye Sifi alitumwa na Mwenye Kaya lakini nini kilijiri?

Lakini kumbukeni kuna mheshimiwa mmoja nadhani atakuwa Ziro aliwahi kuwaambia wafanyabiashara ukitaka biashara zako zisiwe na usumbufu wewe jiunge na SISI wa Me, lakini kuna watu walishawahi kusumbuliwa na TRA na kudaiwa kodi lukuki kwa sababu tu waliunga mkono vyama vya upinzani.

Kwa hiyo Masaunyi yuku nyumbani kwao sana tu.
 
Mkuu huu ni mtazamo wangu na sio wa chama,tafadhali usiingize chama hapa...msipende sana kuhukumu wenzenu wakatyi hata nyie mnadhambi kibao,hebu kuweni wa kweli kidogo..
Wakina nani wana madhambi yepi?Can yu plz be a little more specific on dat?issue hii inahusu masuala ya chama,sasa ona unatapa tapa na kudai eti ooh ni msimamo binafsi,yes ni misimamo binafsi ya kina JK lakini si ya chama?Ama unaleta zile za Zitto na Dowans eti msimamo binafsi,misimamo yenu binafasi ita aafect maamuzi be it ya kichama ama Taifa...Duh!
Haya shuhudia chadema mtakavyonishukia,na huku ccm wakidai mimi chadema,haya!
 
Jamani,kwani mtu akikosea upande mmoja hawezi kufanya upande mwingine?Mimi sioni tatizo kama atapewa majukumu mengine lakini sio ya vijana...
Mkuu nakubaliana na wewe. Lakini hatua ya kwanza apitie mchakato wa jinai na mahakama imsafishe (au imfunge) kwanza, haya yakiisha apewe hicho kibarua kingine.
 
[/COLOR][/I]
Hakuna Mkuu. Na ndiyo sababu tunahitaji kubadili hali hii kwa bidii zote!

Mara nyingi huwa najiuliza hivi nchi hii hakuna wanaume wemye uchungu nayo? wanangojea mpaka nchi ifikishwe mahala gani ndio waamke waseme sasa basi inatosha? Maisha ya wananchi yamefika mahali ambapo hayana maana tena na ndio maana ushirikina umekithiri kwani watu wamekata tamaa inabidi waamini nguvu za giza!!
 
Hii nchi itaingia vitani,unless haya mambo mnayoyaleta humu ni uongo.
Mkuu,Kama tunashindwa kuwaadhibu kwa kalamu na karatasi(kura) kubeba machete ndiyo tutaweza.We have to reach rock bottom and possibly we start thinking like thai people.
 

Mkuu hapo wenye highlights una uhakika?
 
Atapangiwa kazi ya ukuu wa wilaya (DC) period.
Natanguliza pole zangu kwa watakaopangiwa DC ambaye amedanganya kuhusu umri wake. Sijui atawadanganya mambo mangapi mengine hao atakaokabidhiwa dhamana ya kuwadanganya... no I mean kuwaongoza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…