Mwanzo tulisema hapa si waziri wala wananchi wanaoelewe hili jambo!
Swala hapa ni television husika yani FTA kuwa bure haijalishi una kifurushi au huna kifurushi ,kimekwisha au hakijakwisha!
Sasa kurudi lakini kifurushi kikiisha zinakata hii bado haina maana ya hoja na kusudi la waziri na wananchi kama waziri alielewe kile kilichokuwa kilio cha wananchi!
DSTV walikuwa nazo hizo channel na waliziondoa baada ya serikali kuwalazimisha kuwa channel ten,Clouds Tv,ITV,EATV na TBC 1 zioneshwe bure yani hata kama kifurushi kikikata basi hizo zibaki zinaonekana ndio maana wakaziondoa!
DSTV wamezitaka hizo kibiashara maana wateja wao nikiwemo mimi nilikuwa naziangalia japo kwa kulipia lakini serikali walitaka ziwe bure kabisa na wao DSTV wanazifanyia biashara na kwa hiyo hapa tukubali DSTV wameshinda na channel zitarudi lakini watazionesha kwa kulipia kupitia kifurushi lakini sio bure...
Hapa bado Nape hajafanikisha alicho kitaka na kupitia channel hizi DSTV atajizolea wateja wengi sana na bahati mbaya washindani wake walilalamika kuwa wao wamewekeza sana hivyo DSTV hana haki ya kuonesha FTA...hapo sasa
Ukweli ni kwamba DSTV hawatokubali kuonesha bure channel husika!