Hatimaye Kiwia afanyiwa upasuaji India

Imany John

JF-Expert Member
Jul 30, 2011
2,930
1,165
MBUNGE wa Jimbo la Ilemela,
Highness Kiwia
(CHADEMA),amefanyiwa
upasuaji mkubwa wa kichwa
katika Hospitali ya Apollo
nchini India, Alhamisi iliyopita.

Akizungumza na Tanzania
Daima jana, Mkurugenzi wa
Masuala ya Bunge wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), John Mrema,
alisema kutokana na upasuaji huo, hali ya mbunge huyo
inaendelea vizuri.
“Mheshimiwa Kiwia
alishafanyiwa upasuaji
mkubwa wa kichwa tangu
Alhamisi ya wiki iliyopita na
kwa sasa anaendelea vizuri,”
alisema Mrema. Alipoulizwa kuhusu kurejea
nchini Mrema alisema ni
mapema mno kueleza kwani
hivi sasa anaendelea kuwa
chini ya uangalizi wa
madaktari. “Kuhusu kurejea lini nchini
madaktari ndio watakaojua
kwani kwa sasa anaendelea
kuangaliwa pamoja na
kufanyishwa mazoezi,”
alisema Mrema.

Kiwia na mbunge mwenzake
wa chama hicho, Salvatory
Machemuli wa Jimbo la
Ukerewe walijeruhiwa vibaya
kwa mapanga na shoka na
watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha
Mapinduzi(CCM) katika eneo la
Ibanda, Kabuhoro mjini
Mwanza.

Tukio hilo lilitokea usiku wa
kuamkia Aprili mosi mwaka
huu baada ya wabunge hao
kudaiwa kuvamiwa na watu
hao.
Akizungumzia tukio hilo
Kamanda wa Polisi wa Mkoa
wa Mwanza, Liberatus Barlow,
aliwataja wengine
walioshambuliwa kuwa ni
Ahmed Waziri ambaye inasemekana kuwa ni kada
wa UVCCM aliyekatwa kiganja
chake cha mkono wa kulia.

Wengine ni Haji Mkweda (21),
ambaye alijeruhiwa mguu wa
kulia, Judhith Madaraka (26),
aliyechomwa kisu kwenye titi
lake la kushoto na mkono wa
kushoto, Ivory Mchimba (26), aliyejeruhiwa kichwani na
mdomoni. Majeruhi wote ukiondoa
wabunge hao na waziri,
wamelazwa katika Hospitali
ya Mkoa ya Sekou Toure.

Awali, wabunge hao
walilazwa katika Hospitali ya
Rufaa Bugando lakini baadaye
walisafirishwa kwa ndege
kupelekwa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam na baada ya siku
kadhaa mbunge Kiwia
alihamishiwa katika Hospitali
ya Appolo, India.

Source:Tanzania daima.
 
Pole kamanda!!Inasikitisha kuona waliofanya huu unyama bado hawajashughulikiwa!!
 
Tumesha usoma mchezo,tumejiaa vya kutosha tunasubiri maelekezo.zamu yao inanukia sana.
 
Hizi damu zinazomwagwa na hawa CCM zinatuletea laana nchini mwetu, inashangaza haya mambo ya kumwaga damu kwa malengo ya kisiasa yanaanza kuwa ya kawaida. God forbid.
 
Pole sana mkuu...I remember such a bad night was arounr too...nikanusurika.CCM=Chama Cha Mauaji
 
ivi kwa nini tunasomesha madaktari? bora tusomeshe manesi tu basi

ili wawatibu watanzania maskini. Njoo moi uone kina prof kahamba wanavyofanya kazi ndipo utakapojua tz kuna madaktari wazuri. Kina jk wamewastarv vifaa wamebaki kuwa waganga wa kienyeji. Hao wabunge wanalazimisha waende nje kutokana na ile sera yao ya kuifirisi nji hii.
 
ili wawatibu watanzania maskini. Njoo moi uone kina prof kahamba wanavyofanya kazi ndipo utakapojua tz kuna madaktari wazuri. Kina jk wamewastarv vifaa wamebaki kuwa waganga wa kienyeji. Hao wabunge wanalazimisha waende nje kutokana na ile sera yao ya kuifirisi nji hii.
Kama yeye keshazoea Waganga wa kienyeji, unategemea vipi awathamini modern doctors!
Hivi waliowapiga mapanga walishakamatwa? Au walifanya hiyo kazi kwa Maagizo? Je na upande wa pili nao ukiamua "kama n' mbwai, mbwai!" Watalaumiwa!
 
mungu awajaze nguvu waweze kupona haraka warejee kwenye harati za kutukomboa tulio gizani.
 
..kama wale waliOfanya vurugu kujeruhi watu hivi karibuni pale katika mkutano wa Mbunge wa CDM na wananchi wa Nduli wamekwishafikishwa mahakamani, Iweje hili la wabunge wa Mwanza? Ninaona kuna JAMBO HAPO! au ndio nimepitwa na taarifa ya maendeleo ya sakata hili la MWANZA??
 
Mkakati wa kuwaua baadhi ya viongozi makini wa chadema hautafanikiwa kwa sababu wananchi wamejenga imani katika falsafa ya chama na hivyo yeyote akipendekezwa na chama kugombea kwenye nafasi fulani ni lazima atakuwa mwiba mchungu kwa magamba.BIBLIA IMFANDIKA "Msiogope aharibuye mwili bali mwogopeni yeye awezaye kuharibu mwili na roho".CCM wajue hatutarudi nyuma kwa sababu hatuwaogopi kwani vita ya haki ni ya Mungu na ndiye tunayesimama naye,tutamwogopa na kumheshim yeye peke yake katika hili. KIWIA pona kamanda uje tupambane ukombozi uko karibu.
 
Back
Top Bottom