Hatimaye fedha kurudi mitaani

Sijui itaanza lini,mfukoni jua kali balaaa!!!
Day light dreaming (Hawa wasomi hawashauri?) wakiona mambo yana kwenda mrama wanajitokeza ila inawezekana serikali hii pia haishauriki hawa wasomi pengine hawapati nafasi ya kushauri (Let us not beat about the bush by calling a spade a spade not a big spoon) kupata ushauri wa kitaalamu ni muhimu kwa uendeshaji nchi biila kusahu utawala wa sheria
 
Wasomi wanapaswa kupingana hivi.
 
Huyo anayesema hela itakuja mitaani kwa serikali kukopa toka mabenki ya ndani huyo siyo tu hastahili kuitwa msomi bali ni mtu ambaye amekosa hata ule uelewa wa kawaida. Na kama anafundisha University, anatakiwa kufukuzwa.
Haya bwana. Nenda ukachukuwe hiyo nafasi yake ya kufundisha uchumi huko University, kawaonyeshe hako ka certificate kako ka economics watakupa tu huo u professa.
 
Haya bwana. Nenda ukachukuwe hiyo nafasi yake ya kufundisha uchumi huko University, kawaonyeshe hako ka certificate kako ka economics watakupa tu huo u professa.
Nani kakuambia nina certificate ya Economics. Mimi sina hata certificate ya Economics. Nilimaliza pale UD nikiwa second best science student. Nikasonga mbele lakini siyo kwenye Economics. Na baadaye sikutaka kufundisha. Kwanza kinachojadiliwa hapa siyo Academic Economics ni Reasoning Economics ambayo huhitaji hata diploma kuelewa.

Unachotakiwa kujua ni kuwa serikali inapokopa kwenye mabenki ya ndani inasababisha inflation. Serikali inapokopa kwenye mabenki ya ndani hufifisha mzunguko wa pesa kwa sababu inakopa pesa nyingi kwaajili ya kugharamia miradi mikubwa inayotekelezwa na makampuni mengi ya kigeni, na miradi hiyo huwa eneo fulani tu la nchi na hivyo kusababisha uhuisho mdogo kwenye mzunguko wa fedha (sehemu kubwa ya pesa inaenda ambako makampuni yanatoka) ukilinganisha na ukopaji wa fedha unaofanywa na watu binafsi. Pesa inayokopwa na serikali mara moja wanaweza kukopeshwa watu binafsi hata zaidi ya 50 wanaotoka maeneo mbalimbali ya nchì. Hivyo inasaidia kukuza mzunguko wa pesa maeneo mengi kwa muda mfupi.
 
Inflation (bei ya vitu kupanda) maana yake kuna pesa nyingi mitaani kuliko idadi ya vitu (supplies). Kama umekubali kuwa serikali kukopa benki za biashara kunaweza kuleta inflation, maana yake ni hiyo hiyo kwamba kutasababisha fedha mitaani kuwa nyingi zaidi kuliko idadi ya vitu. Hivyo serikali kukopa benki hizi kutasababisha wingi wa fedha mitaani na kama uzalishaji wa vitu hautaongezeka kutatokea inflation. Ili inflation isitokee ni muhimu kuwa kiasi kikubwa kitakachokopwa toka benki hizi zielekezwe kwenye miradi ya uzalishaji wa vitu mhimu. Hili linaweza kufanywa vizuri zaidi na serikali badala ya mtu mmoja mmoja.

Haizalishi mzunguko wa pesa mitaani umeanzia wapi. Pesa ikishaingia tu mtaani huzunguka haraka sana na kuenea nchi nzima. Wewe tuseme uko Dar jaribu ku trace fedha zako ulizotumia leo uone kesho zitakuwa wapi? Utakuta zingine zilifika Mwanza siku hiyo hiyo kupitia Msukuma mmoja aliyekuja kuuza ng'ombe wake Dar. Pesa haikai eneo moja inasambaa kwa wachapa kazi halali na wasio halali. Hela ikishaingia mitaani hata majambazi, machagudoa na wauza unga inawafikia! Huu ndyo ukweli.
 
Ila kweli trip hii ndio wapo kutukana watanzani.
 
Njaa haina baunsa .
 
Mhmh! ya kweli hayo, zitazidi kukauka mifukoni
 
Mkuu umeandika kisomi mno !
 
Mkuu, mbona unapenda maneno meeengi, sentensi yako ya kwanza ndio imebeba mambo yote. Hayo mengine unachosha tu vidole kwenye keyboard.
 
Hivi kukitokea financial meltdown kama iliyotokea ulaya mwaka 2008, ni nani atam'bale out' mwenzie? Nakumbuka srikal za ulaya na marekani ilibidi ziya'bale out' mabank. Sasa ikitokea hapa kwetu ambapo serikali ndio inakuwa bailed out sijui itakuwaje?
 
Unaambiwa hata ule uongo wa mapato ya TRA ya kila mwezi kimyaaaaaa !!!!
Sometimes kuna watu wandanganya bila kuwa na uwezo wa kujua wanachoongea ni uongo.Ndio maana wengine hata kuapa kwa jina la Muumba sio shida.
 
Hiyo ni fyokofyoko mkuu .
Wanahitajis ababu za msingi.Hapa wanaweza kuwa na roho mbaya ile ile, waliyoitumia kutoa hela, km hizo bank zilienda kopa dollar nje,hii roho mbaya yao itarudi kuzipora hizo hela kwa nguvu km mkopo.Kisha waanze wazungusha kuwarudishia na hao jamaa washindwe lipa Tena.
 
Naona bwana Ngosha ameshaishiwa sasa ...!!! Makusanyo yote hayo ya TRA..?! Kubana kote matumizi..?!

Nasikia BOT inawahudumia watu wa Chato pekee, mpaka waseme poo...!!

Kweli nyumban ni nyumban mtan wangu, Chato oyeeeeeee......!!
Mkuu kuna ubahili wa kuua kampuni.Ukiwa mbahili jitibu ipo siku utajitibu kwa hela ya kutosha maliza akiba yote.Ukiwa mbahili ktk ujinga ujinga km kununua engine oil.Utanunua engine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…