Hatimaye Damu yetu haikumwagika Bure Uganda, Tunalipwa!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Raisi Museveni wa Uganda amesema sababu za nchi yake kuamua kupitisha bomba la mafuta nchini mwetu ktk Tanga mpaka Uganda badala ya nchi ya Kenya ni kulipa fadhila kwetu kwa kazi kubwa na isiyo ya kibinafsi tulioifanya huko Uganda ya kumtoa Idi Amini!

Leo hii Uganda ni nchi nzuri inayostawi kwenye ngazi zote, uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa na hii yote ni kwa sababu tulijitoa mhanga kwa ajili yao, hivyo kama tusemavyo Waswahili wema hauozi, hatimaye Raisi Museveni amelitambua hilo!

Hili Bomba kwa mujibu wa Raisi Magufuli lina thamani ya 4 bilion US dollars na litazalisha ajira kwa watu zaidi ya elfu 15! TanZania ya viwanda hiiyo inajongea kwa kasi kabisa!

Sasa Bandari yetu ya Tanga itapata kazi na kuwa busy na hii ni neema kubwa kwa Mji na Mkoa wa Tanga!

Come babe come!!!!!

HAPA KAZI TU!
 
Huu Ni Ujinga Wa hali Ya Juu, Rais Mseven ameona kwamba Kenya tayari imegundua Mafuta yake ardhini, hivyo akapiga hesabu za haraka akaona aweke Bomba hili kuanzia Tanzania-Tanga kama danganya toto, kumbuka Uganda nayo imegundua mafuta, sasa mahesabu ya Mseven ni kwamba, mara tu uzalishaji utakapoanza Uganda, bomba hilo hilo pia litumike kusambaza mafuta yake Tanzania na kutuuzia, hivyo Uganda ndo itapata faida, maana Tutanunua mafuta kutoka kwake, vile vile Tutalipia hilo Bomba lake, hivyo wataalamu wa Uganda, kimahesabu ni kwamba watakuwa wameipiku Kenya au kuiwahi kwa kuteka soko la Tanzania.
 
Wanaoyatazama mambo kwa mtazamo wa karibu kama taa ya baiskeli inayokatiza gizani, hawawezi kuelewa maana pana ya kilichoandikwa kwenye uzi huu. Habari iliyoandikwa haina mipasho, ni mambo makubwa ya kiuchumi. Bandari ya Tanga baada ya kupoteza ile tenda ya makontena ya KMCL, ni kama ilikuwa ikitegemea mizigo michache. Nadhani hili bomba litaifanya bandari ifufuke upya. Afrika ya mashariki yenye maendeleo inaanza kuonyesha dalili ya kuja kuwa hai.
 
Huu Ni Ujinga Wa hali Ya Juu, Rais Mseven ameona kwamba Kenya tayari imegundua Mafuta yake ardhini, hivyo akapiga hesabu za haraka akaona aweke Bomba hili kuanzia Tanzania-Tanga kama danganya toto, kumbuka Uganda nayo imegundua mafuta, sasa mahesabu ya Mseven ni kwamba, mara tu uzalishaji utakapoanza Uganda, bomba hilo hilo pia litumike kusambaza mafuta yake Tanzania na kutuuzia, hivyo Uganda ndo itapata faida, maana Tutanunua mafuta kutoka kwake, vile vile Tutalipia hilo Bomba lake, hivyo wataalamu wa Uganda, kimahesabu ni kwamba watakuwa wameipiku Kenya au kuiwahi kwa kuteka soko la Tanzania.

Sasa kama ni kweli unavyosema huwo Ujinga uko wapi? Au ndiyo staili ile ile ya kutokuelewa maana ya upinzani kwamba ni kupinga kila kitu hata kama hakuna sababu ya kufanya hivyo?

Haijalishi sababu ni ipi ile tu kwamba nchi ya Uganda itatumia Bandari yetu ya Tanga ni sababu tosha ya sisi kusherehekea kwani Bandari yetu itapata kazi ya uhakika!
Hili Bomba litagharimu dola Bilion 4 za Kimarekani ina maana sehemu ya hii fedha itawekezwa Tanzania yetu, hapo ni win win situation kwetu kuanzia mafundi wa ujenzi wa bomba mpaka mama lishe wa kuuza vyakula site kuendelea mpaka kwa wahandisi
watu wetu watapata ajira za moja kwa moja na zingine zisio za moja kwa moja!

Na hata kama Uganda wakiuza mafuta kwetu hauoni kwamba watakuwa wametusaidia sana badala ya sisi kuimport? tena hili Bomba litakuwa limejengwa siyo kwa fedha zetu ina maana litatuletea mafuta nyumbani!
 
hehehe....nataka niendew nikajibu ile thread yako naona jamaa zako wananishambulia hatari....by the way how is your campaign? to turn every one at JF a Demon,Devil,Satanic,Masonic,Illuminati and Evil Sorcerer and Worshiper? @mshanajr
 
Doing wonderful...!!! By the way learn to defend your point of view. ...ukiwa bondia usiogope za uso
 
Ni rahisi kudefend vitu ambavyo viko kwenye akili ya mtu...lkn ww umewashibisha imani....they dont understand...they feel it..
 
Huu Ni Ujinga Wa hali Ya Juu, Rais Mseven ameona kwamba Kenya tayari imegundua Mafuta yake ardhini, hivyo akapiga hesabu za haraka akaona aweke Bomba hili kuanzia Tanzania-Tanga kama danganya toto, kumbuka Uganda nayo imegundua mafuta, sasa mahesabu ya Mseven ni kwamba, mara tu uzalishaji utakapoanza Uganda, bomba hilo hilo pia litumike kusambaza mafuta yake Tanzania na kutuuzia, hivyo Uganda ndo itapata faida, maana Tutanunua mafuta kutoka kwake, vile vile Tutalipia hilo Bomba lake, hivyo wataalamu wa Uganda, kimahesabu ni kwamba watakuwa wameipiku Kenya au kuiwahi kwa kuteka soko la Tanzania.
duhh!! Huyu ndugu haoni faida ya bomba la mafuta kupita nchini kwetu kweli? Siamini ninachokisoma. Tuwe tunafanya tafiti kabla ya kujirusha hewani. Wengine tunachafukwa roho haraka, tusaidiane kwani hatupendi kurusha makombora.
 
Magufuli amekurupuka..bomba la mafuta litawanufaisha waganda..tumekula hasara
 
Magufuli amekurupuka..bomba la mafuta litawanufaisha waganda. Watanzania tumekula hasara
 
Structured conversation is based on ....
What...?--->So What...?--->Now What...?
=====================
Tukirudi kwenye mada. Tunahitaji justification ya utengenezwaji wa ajira...na tujue hizo ajira zitakuwa za kudumu ama za muda mfupi?
 
Raisi Museveni wa Uganda amesema sababu za nchi yake kuamua kupitisha bomba la mafuta nchini mwetu ktk Tanga mpaka Uganda badala ya nchi ya Kenya ni kulipa fadhila kwetu kwa kazi kubwa na isiyo ya kibinafsi tulioifanya huko Uganda ya kumtoa Idi Amini!

Leo hii Uganda ni nchi nzuri inayostawi kwenye ngazi zote, uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa na hii yote ni kwa sababu tulijitoa mhanga kwa ajili yao, hivyo kama tusemavyo Waswahili wema hauozi, hatimaye Raisi Museveni amelitambua hilo!

Hili Bomba kwa mujibu wa Raisi Magufuli lina thamani ya 4 bilion US dollars na litazalisha ajira kwa watu zaidi ya elfu 15! TanZania ya viwanda hiiyo inajongea kwa kasi kabisa!

Sasa Bandari yetu ya Tanga itapata kazi na kuwa busy na hii ni neema kubwa kwa Mji na Mkoa wa Tanga!

Come babe come!!!!!

HAPA KAZI TU!
Hawa jamaa si wamegundua mafuta kule kwao? sasa wanataka mafuta mengine ya nini? Hapa kutakuwa na jipu kwenye hili bomba
 
Back
Top Bottom