Hatimaye Aggrey Mwanri awa Mchungaji rasmi. Sasa ukisikia soma hiyoo! Ujue ni somo la Injili

Aseew ana stress vibaya mno...hivi huwa hawatoshekwi?

Mavyeo yote ambayo alishapata ila bado tuu anasumbua

Nakumbuka alivyostaafishwa uRC aliamua kuwapigia CCM wenzake kampeni akidhani mzee Baba atampa tena teuzi..kumbe Holla
Ni makosa yeye kumtumikia Mungu?
 
mzee alitupa furaha sana enzi za utawala wa jiwe.

kauli zake na namna alivyokuwa anakemea watendaji wa chini yake, ziligeuka kuwa burudani badala ya kero.

Mungu amsimamie na kumuongoza ktk majukumu yake nje ya siasa.
I love him very much
Mungu azidi mtunza huyu baba.
 
SIHA :- MWANRI AWA MUINJILISTI

Aliyepata kuwa mtumishi wa Serikali akihudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ya Unaibu Waziri na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri (Pichani: Katikati) amethibitisha kuingia rasmi katika utumishi wa Mungu kama Mwinjilisti katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Uthibitisho huo umekuja siku chache baada ya kusambaa kwa uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba Mkuu huyo wa Mkoa Mstaafu Aggrey Mwanri ameanzisha kanisa.

Habari hiyo ilisambaa kwa wingi na kasi mitandaoni ukimwonyesha Mwanri akiubiri huku akiwa amevalia joho la utumishi wa kiroho ndani ya moja ya kanisa katika wilaya Siha mkoa wa Kilimanjaro

Katika kuondoa utata huo na kuweka bayana kinachoendelea kwa sasa Mwanri mwenyewe anafanua kwamba alitunukiwa Uinjilisti wa kanisa la KKKT kwa kupata baraka zote za viongozi wa dhehebu hilo

Mkuu wa Mkoa mstaafu Mwanri katika utumishi wake serikalini amekuwa maarufu sana katika matumizi ya misemo mbalimbali ambayo aliitumia kama msisitizo wa jambo wa jambo fulani kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa urahisi katika jamii.

Sasa ameingia katika kuwatumikia wananchi kiroho anazungumziaje, Je ataendelea kutumia misemo hiyo katika kufikisha neno la Mungu kwa urahisi kwa waumini?

Licha ya kuwa mkuu wa Mkoa Mwanri amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ambazo ni pamoja na Naibu waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu-Tamisemi, Mkuu wa wilaya ya Arusha, mbunge wa Siha na pia Katibu wa Itikadi na uenezi wa taifa wa CCM.

SUKUMANDANI...
https://m.youtube.com/channel/UCUzK7v2L8t7qH0mDQ_7CuWg

Login • Instagram

Kasomi
 
Ni jambo jema sana,ameishaitumikia nchi,sasa ni wakati wa kumtumikia Mungu.Muumba wa Mbingu na nchi
 
Mzee ameamua.
IMG-20210418-WA0001.jpg
 
Back
Top Bottom