UKITAKA KUJUA ATHARI ZA SINEMA ZA KIHINDI KURATIBIWA NA UONGOZI WA KI-CHINA BASI KAMUULIZE ALHAJI AFANDE SELE PALE 'MAMBO YA NDANI' NA JINSI GANI ALIVYOLITIA KOVU LA KUDUMU JESHI LA POLISI
Kwa akili tu ya kawaida, busara zinatuamrisha ya kwamba pindi tunapoinuia kutengeneza sinema ama yaa Kihindi, Kimang'ati au hata ya Kichina, ni vema tukawapa nafasi watu wenye ufahamu mzuri na tamaduni za mahali husika wakatusaidia kuratibu mambo.
Ajabu na kweli ni kwamba katika jaribio la kumchukua uhai Dk Ulimboka, majina ambayo yatokea kutajwatajwa yametokea kuwa ni wa upande fulani tu. Madai ya Uhalifu huo ni wao, Uchunguzi ni wao, Usemaji ni wao, na hata Uratibu mzima bado ni wao tu.
Hakika hili kidogo linatatiza kwa kuwa jeshi letu la polisi sote tunajua halina dini lakini kwa mwenendo huu wa mara Abeid wa Ikulu, Ahmed Msangi wa Kanda Maalum, Selemani Kova kubwa lao, Saed Mwema ambaye ndiye Back-stopper hapo -- mmmmmmhhhh!!!
Japo ni jambo ambalo halisemwi wazi wazi na wengi LAKINI mmmhhhhh!!! Kwa nini na kwani kuna nini??? Siku zote Matokeo ya mambo kama haya, pengine ni ajali tu imetokea hadi hapo, mwisho wa siku huleta taswira kama vile ya Picha ya KIHINDI kuratibiwa vile na WACHINA.
Mtu akiangalia ki-undani, pale kwenye ONYESHO LA PILI, jinsi gani ka-Gwajima (Mkristo) na Joshua (nalo jina la kikristo ila mbebaji wa jina hilo HATUNA UHAKIKA na dini yake mpaka atakapotuthibitishia kwa kinywa chake mwenyewe) wanavyovutwa kwa nguvu zote kuwa sehemu ya mchezo katika filamu hii - yote yanayojitokeza ni VITUKO VYA KARNE katika historia ya mambo ya kipolisi duniani kote.
Kwa watazamaji wapya wa picha hii ya 'KOVA KATIKA MABAWA YA MABADILIKO YA NGUVU YA UMMA NCHINI TANZANIA', kwa kukumbushia tu, ONYESHO LA KWANZA ilianzia pale Leaders' Club na kuishia Mabwepande Tegeta na walioonekana mwishoni mwa picha ile ni Mama Kijo Bishimba, Mzee Mwanakijiji, Mjeruhiwa Dk Ulimboka pamoja na wanakijiji katika yale mandhari asili ya MabwePande.
Sababu ya kusema hivyo ni kwamba Alhaji Afande Sele (Kanda Maalum Jijini Dar), kwa kosa moja tu la kutokufahamu desturi na taratibu za madhehebu ya ki-Kristo ki-ajali kabisa kajikuta AMEUNGUZA PICHA ZIMA kwa kudai kwamba mgeni wake Joshua Muyungi alienda na AKATUBU katika kanisa la Nabii Mkuu na Askofu Gwajima juu ya uhusika wake kwenye jaribio la kumua Dr Ulimboka. Hii ndio maana kila wanapojaribu kuunganisha picha hizo mbili hali inaendelea tu kuwa kama mafuta ya taa na maji kwenye maabara zetu za kibongo hizi.
Ukweli wa mambo ni kwamba mbali na Kanisa Katoliki ambako watu hujichagulia kwenda kwa Padre na kutubu dhambi zao, madhehebu mengine yote ya ki-Kristo hayana utaratibu huo. Lakini kwa kuwa Alhaji alikua anatafuta MNOGO WA PICHA YENYEWE ndio hapo maini yakaingia nyongo.
Kama bado tu mtu hajashtuka kitu hdi hapo, hivi watu bado tu hamjiulizi kwa nini ONYESHO LA TATU (linalotegemewa kuwa ndefu sana mpaka hadhira kujikuta wachapa tu usingizi badala ya kuendelea kufwatilia picha) la filamu ilivyoanza kwaa usiri mkubwa katika mahakama ya Kisutu na kwamba wahusika wote huko wakawa ni WATU WA KUFIKIRIKA tu huku wengine wakidaiwa kuwasili tu kutoka katika taifa la KUSADIKIKA ('nimewasili na bado ninaendelea kuwazoea').
Mpaka hapa wala mtu hahitaji kutngaziwa kwamba kwele Alhaj Afande Kova kalitia kovu chombo hiki, tulichopata kukiamini na kukithamini sana miaka hiyo, kwa namna ambayo itachukua miaka kuturudisha imani sisi Umma wa Tanzania.
Sasa kilichobaki pengine ni wahusika wkuu wa filamu hii warudi tena mezani ili waje na ubunifu mwingine maana huu wa sasa ndio kama hivo umekwishagonga mwamba.