Hatimaye afande Kova ajibu shutuma juu yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye afande Kova ajibu shutuma juu yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by motema yapembe, Jul 16, 2012.

 1. m

  motema yapembe Member

  #1
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Leo kamanda. wa police wa Dar es salaam Amevieleza vyombo vya habari kuwa alie mkamata ndie mtuhumiwa na alikuwa Kwenye ibada ya three 13/07 2012. hivyo sijui mchungaji kasema nn!, amesha pelekwa mahakamani hivyo hairuhusiwi kuhoji jambo lolote lililo mahakamani!
  his ndo bongo bana!

  source, channel 5
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo hakukamatwa tarehe 29 kama alivyosema mwanzoni?
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  UKITAKA KUJUA ATHARI ZA SINEMA ZA KIHINDI KURATIBIWA NA UONGOZI WA KI-CHINA BASI KAMUULIZE ALHAJI AFANDE SELE PALE 'MAMBO YA NDANI' NA JINSI GANI ALIVYOLITIA KOVU LA KUDUMU JESHI LA POLISI

  Kwa akili tu ya kawaida, busara zinatuamrisha ya kwamba pindi tunapoinuia kutengeneza sinema ama yaa Kihindi, Kimang'ati au hata ya Kichina, ni vema tukawapa nafasi watu wenye ufahamu mzuri na tamaduni za mahali husika wakatusaidia kuratibu mambo.

  Ajabu na kweli ni kwamba katika jaribio la kumchukua uhai Dk Ulimboka, majina ambayo yatokea kutajwatajwa yametokea kuwa ni wa upande fulani tu. Madai ya Uhalifu huo ni wao, Uchunguzi ni wao, Usemaji ni wao, na hata Uratibu mzima bado ni wao tu.

  Hakika hili kidogo linatatiza kwa kuwa jeshi letu la polisi sote tunajua halina dini lakini kwa mwenendo huu wa mara Abeid wa Ikulu, Ahmed Msangi wa Kanda Maalum, Selemani Kova kubwa lao, Saed Mwema ambaye ndiye Back-stopper hapo -- mmmmmmhhhh!!!

  Japo ni jambo ambalo halisemwi wazi wazi na wengi LAKINI mmmhhhhh!!! Kwa nini na kwani kuna nini??? Siku zote Matokeo ya mambo kama haya, pengine ni ajali tu imetokea hadi hapo, mwisho wa siku huleta taswira kama vile ya Picha ya KIHINDI kuratibiwa vile na WACHINA.

  Mtu akiangalia ki-undani,
  pale kwenye ONYESHO LA PILI, jinsi gani ka-Gwajima (Mkristo) na Joshua (nalo jina la kikristo ila mbebaji wa jina hilo HATUNA UHAKIKA na dini yake mpaka atakapotuthibitishia kwa kinywa chake mwenyewe) wanavyovutwa kwa nguvu zote kuwa sehemu ya mchezo katika filamu hii - yote yanayojitokeza ni VITUKO VYA KARNE katika historia ya mambo ya kipolisi duniani kote.

  Kwa watazamaji wapya wa picha hii ya '
  KOVA KATIKA MABAWA YA MABADILIKO YA NGUVU YA UMMA NCHINI TANZANIA', kwa kukumbushia tu, ONYESHO LA KWANZA ilianzia pale Leaders' Club na kuishia Mabwepande Tegeta na walioonekana mwishoni mwa picha ile ni Mama Kijo Bishimba, Mzee Mwanakijiji, Mjeruhiwa Dk Ulimboka pamoja na wanakijiji katika yale mandhari asili ya MabwePande.

  Sababu ya kusema hivyo ni kwamba Alhaji Afande Sele (Kanda Maalum Jijini Dar), kwa kosa moja tu la kutokufahamu desturi na taratibu za madhehebu ya ki-Kristo ki-ajali kabisa kajikuta AMEUNGUZA PICHA ZIMA kwa kudai kwamba mgeni wake Joshua Muyungi alienda na AKATUBU katika kanisa la Nabii Mkuu na Askofu Gwajima juu ya uhusika wake kwenye jaribio la kumua Dr Ulimboka. Hii ndio maana kila wanapojaribu kuunganisha picha hizo mbili hali inaendelea tu kuwa kama mafuta ya taa na maji kwenye maabara zetu za kibongo hizi.

  Ukweli wa mambo ni kwamba mbali na Kanisa Katoliki ambako watu hujichagulia kwenda kwa Padre na kutubu dhambi zao, madhehebu mengine yote ya ki-Kristo hayana utaratibu huo. Lakini kwa kuwa Alhaji alikua anatafuta MNOGO WA PICHA YENYEWE ndio hapo maini yakaingia nyongo.

  Kama bado tu mtu hajashtuka kitu hdi hapo, hivi watu bado tu hamjiulizi kwa nini
  ONYESHO LA TATU (linalotegemewa kuwa ndefu sana mpaka hadhira kujikuta wachapa tu usingizi badala ya kuendelea kufwatilia picha) la filamu ilivyoanza kwaa usiri mkubwa katika mahakama ya Kisutu na kwamba wahusika wote huko wakawa ni WATU WA KUFIKIRIKA tu huku wengine wakidaiwa kuwasili tu kutoka katika taifa la KUSADIKIKA ('nimewasili na bado ninaendelea kuwazoea').

  Mpaka hapa wala mtu hahitaji kutngaziwa kwamba kwele Alhaj Afande Kova kalitia kovu chombo hiki, tulichopata kukiamini na kukithamini sana miaka hiyo, kwa namna ambayo itachukua miaka kuturudisha imani sisi Umma wa Tanzania.

  Sasa kilichobaki pengine ni wahusika wkuu wa filamu hii warudi tena mezani ili waje na ubunifu mwingine maana huu wa sasa ndio kama hivo umekwishagonga mwamba.

   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jul 16, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hawa watu hawajui hata kudanganya.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  CCM walianza kwa kucafua BOT, wakachafua Police, TISS na sasa Mahakama! Wanapataje usingizi hawa wakubwa?
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  "Naogopa kuzungumza coz hili swala lipo mahakamani" hii statement kwa kova ni kumuogopa gwajima maana kashaaribu picha la kihindi.
   
 7. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,798
  Likes Received: 36,823
  Trophy Points: 280
  paranawee inaendelea
   
 8. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #8
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,341
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  Mahakama siku hizi imekuwa kama FFU. Yaani kitu kikija moto wanakipeleka mahakamani afu hakuna kuhoji. Kama kweli mahakamani wangekuwepo majaji wenye weredi na kazi zao wangeisha piga stop hali hiyo. Naweza kukubaliana na Mh Lissu kuwa na majaji wa fasta fasta.
   
 9. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #9
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,033
  Likes Received: 8,521
  Trophy Points: 280
  Hivi kwanini lakini serikali haitaki kuwaruhusu Chadema waunde tume huru ya uchunguzi wa hii issue?
   
 10. F

  Fringe Senior Member

  #10
  Jul 16, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Serikali inatengeneza kaburi lake lenyewe,watatuzuia kwa fitna kulijadili suala hili kwa hila zao za kichaka cha mahakama,watafanikisha...ila trust me kumziba mtu mdomo ni kumuongezea chuki,heri mtu asemeee anyamazee...serikali haiaminiki,polisi hawaaminiki,mahakama hazina mvuto kwa wanyonge,viongozi hawana touch ya wananchi,hawapendwi.

  kinacho tokea Ngado-singida ni kielelezo cha chuki ambayo ipo juu ya serikali na watu wanao i support serikali hiyo,chuki hii watawala wanaijenga kwa wananchi,chuki hii inaanza kukua,itahamia kwa akina Nappe,mwigulu,wasira et el..ipo siku watapigwa kama wezi na wananchi...!

  Ukiwashitaki polisi wataachiwa,ukiwapeleka mahakamani watashinda....lakini nikirusha jiwe,panga,au mkoki siwezi kuwakosa....They will feel the pinch that i always feel,the pains caused by them to me shall be paid as permanent torture to them..
  make my word
   
 11. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #11
  Jul 16, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mi ninachoamini Kamanda Kova hakusema Gwajima alimkamata na kumpeleka polisi. pili Mch. Gwajima alisema walizi wake ndiyo walimkamata huyo jamaa je walimpeleka wapi? je walimkamata kwasababu zipi? Nani waliwataarifu polisi? Sawa tuseme katengenezwa je huyu jamaa ilikuwaje aseme aliyemtuma ni mtu wa serikalini? kwanini Kova asilifiche hilo akaliweka wazi? Mch. Gwajima anasema kwake watu hawaungami lakini akumbuke kuwa Kova alisema huyo mtu ndiye aliye sema hayo na si Gwajima. Nadhani Gwajima anajaribu kutafuta umaarufu baada ya umaarufu huo kupotea aweke wazi aache kubwabwaja, kwanini nasema hivi? kwasababu Gwajima alitamka kuwa huyu mtu atakuwa hana akili timamu au ametumwa mimi siyo wa kudanganywa na vipesa sasa aseme alipewa pesa na nani? Naamini huyu bwana Gwajima ana siri nzito anapaswa kuhojiwa maana kanena mwenyewe. Huyo Msangi anayemsema inajulikana wazi kuwa ilikua propaganda ili iundwe tume huru. Mchungaji na Nabii Gwajima namkumbuka sana alivyosema anaweza kumfufua Amina Chifupa na sakata lake na Mchungaji na Nabii Geor Davie. Bwana tunachezewa akili na hao jamaa wote siwaelewi kabisa. Nadhani nahitaji kuanza kazi ya uandishi wa uchunguzi zadi
   
 12. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #12
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama kova alikua amechagua kamati yakuchunguza hiki kitu kwanini yeye atangaze na si kamati alio ichagua
  Inaonyesha kua ile kamati haina chakufanya

  Kuna maswali mengi ambayo hayana majibu
   
 13. mikonomiwili

  mikonomiwili JF-Expert Member

  #13
  Jul 16, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Weeee tangulini ukaona baba anakubalikuaibishwa na mtotowake? Ndo hivyo hivyo kwa serikali na hata sikumoja wala msiote haitakaa itokee wakubali kilichotokea its not easy
   
 14. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #14
  Jul 16, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi hawa wanashauriwa na nani?Mambo yapoleta mkorogano hivi ni bora usiongee,sasa wanazidi kulikoroga.
   
 15. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mbona yeye laiitisha press conference wakati tayari mtuhumiwa alishapelekwa mahakamani? mwaka huu hawachomoki ngoja ulimboka arudi
   
 16. Mystery

  Mystery JF Gold Member

  #16
  Jul 16, 2012
  Joined: Mar 8, 2012
  Messages: 7,956
  Likes Received: 6,719
  Trophy Points: 280
  Huyu Kova asiwafanye wa-TZ wa sasa kuwa ni wa mwaka 47, ambao wanaweza kuogopa mkwala wowote wa Polisi, yeye anasema kwa kuwa suala la huyo mtuhumiwa "feki" mkenya lipo mahakamani kwa hiyo haruhusiwi mwananchi yeyote kulijadili hilo, kwa kile anachokiita itakuwa uvunjaji wa katiba, sasa tunamuomba Kova kama kweli anasimamia kikamilifu sheria za nchi yetu, aanze kwanza kumkamata Kikwete, ambaye katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi uliopita aliongelea kwa kirefu sana suala la madaktari, wakati anafanya hivyo, spika wa bunge naye alikuwa ametumia staili hii hii ya Kova kuwaziba mdomo wabunge, wakati wote 2 wakijua kuwa suala hilo lipo mahakamani!! Kwanza hata hivyo inabidi tumfundishe sheria Kova kuwa watu kutoa maoni kuwa mkenya wake ni mtuhumiwa feki au kutaka kuundwe Tume huru ya uchunguzi siyo kuvunja Katiba ya nchi, bali ni kutekeleza kikamilifu wajibu wa kila mwananchi kuongelea kwa uhuru masuala ya nchi yake, kama yanavyoainishwa kwenye katiba iliyopo sasa, ibara ya 18, au kimemuuma sana kurukwa futi 100 na mtumishi wa Mungu Gwajima? ambaye amekanusha kuwa mkenya wa Kova hakuwahi kufanya sala ya toba kwenye kanisa la ufufuo kama alivyodai Kova? au yeye Kova alidhani mtumishi wa Mungu ataingia kwenye dhambi kubwa ya jeshi lake, la kupenda kuongea uwongo kwa asilimia 99.9? Hili limemkuta, kama anataka kulinda heshima yake ni vyema akaandika barua yake ya kujiuzulu fasta na kuikabidhi kwa JK kabla hajarejea kutoka kwenye safari zake alizozizoea nje ya nchi safari hii akiwa anatoka Addis. kwenye mkutano wa AU!!!!
   
 17. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna kautamaduni kameanza kujitokeza juu ya seriakli yetu eti kila kitu sasa kinapelekwa mahakamani kwa makusudi ili watu wasizungumzie. Mahakama sasa naona yataka tumiwa kama chaka la kufichia maovu. Kwa mfumo huu kazi tunayo
   
 18. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #18
  Jul 16, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hii nchi kungekuwa kunauwezekano ni kuhiama kabisa maana viongozi wetu ni waongo na wanafiki ipo siku tuta tutawang'oa meno na kucha na wao
   
 19. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #19
  Jul 16, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,706
  Likes Received: 17,754
  Trophy Points: 280
  165978_327048354049715_1823400543_n.jpg

  Huyu candidates hakujiandaaaa kabisa na pepa
   
 20. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #20
  Jul 16, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Japokuwa mimi si mtaalam wa kudanganya, ningeweza kufanya zaidi ya walichofanya hawa jamaa katika suala hili...
   
Loading...