Hatimae Polepole awaangukia Maaskofu

Hatimae Polepole awaangukia Maaskofu

Aaache upuuzi wake huyu Chakubanga. Hakuna mahali popote pale ambapo katiba imesema Rais akosolewe kwa siri. Yeye kuwadhalilisha Watanzania na kuwateka, kuwatesa na kuwaua sawa lakini yeye akikosolewa hadharani KOSA.

  • Akatubu mara moja na aachane na sheria zake kandamizi zote zifutwe mara moja. Sheria kandamizi kuhusu habari na mtandao zifutwe. Magazeti yaliyofungiwa yafunguliwe mara moja
  • Watwambie Watanzania alipo Ben Saanane na Mwandishi wa Mwananchi. Kama wako hai waachiwe mara moja na kama wamewaua maiti zao wakabidhiwe familia zao au waonyeshe makaburi yao.
  • Majina ya Watanzania ambao miili yao iliokotwa ufukweni yatangazwe hadharani haraka sana na tuambiwe sababu za kuuwa kwao.
  • Vyama vya siasa viruhusiwe mara moja kufanya shughuli zake za kisiasa nchini na kutoingiliwa na yeyote yule iwe wakuu wa mikoa, wilaya au polisiccm

Akatubu tu mara moja hakuna jinsi.

Baada ya maaskofu kuliamsha dude kuanzia kipindi cha Salam za krismasi na salam za mwaka Mpya, hatimae katibu mwenezi CCM ndugu Humphrey polepole amejitokeza na kuwaomba maaskofu waishauri serikali sirini kwani kwa hali ilivyo sasa ni kama wanaidhalilisha, Rais yuko tayari kupokea ushauri na kuufanyia kazi.

My take
Kila shetani ana mbuyu wake ukimya wa maaskofu na mashehe umetuumiza sana kama taifa na sina shaka wameamuka usingizini baada ya Askofu niwemugizi kuelekezewa bomba la moshi, pia salam zangu za pole ziwafikie Clouds Media
 
Polepole, mchungaji akienda kuombea Mkutano wa Chadema tayari ni Chadema? Kwahiyo Shekh wa Mkoa wa dar es Salaam ni CCM? Pengo ni CCM?

Haya turudi kwa aliyo yasema, nini kakobe katereza, Katiba inaruhusu Vyama kufanya Siasa, kwanini imezuiliwa? watu kupotea na Kupigwa Risasi, hilo nalo ni kawaida kwa CCM? kwahiyo sasahivi wakosoaji dawa yao ni risasi?

Polepole, Ubabe haujawahi kujenga taifa lolote, mmeambiwa kukaa kimya kwa Watanzania msitafsiri Amani, msilewe mpaka Watanzania wakajua mmelewa.
Kuna chama kimezuiwa kufanya siasa?
 
maaskofu vidume ni wale wa congo.wametangano maandamano nnchi nzima.Hawa wakwetu wakiongozwa na yule mwenye sauti ya kinaa....! mda wote,duu mtasubiri sanaa!.
 
Yaani iwe siri sirini tu?
Mbona sielewi miye?
Kwani mahubiri huwaje?
Huwa chumbani jamani?
Sielewi kitu jamani miye
Muumini wa kawaida akizini na kuzaa nje ya ndoa hutubu mbele ya kanisa, yaani waumini wote... Kiongozi huongozwa sala ya toba ofisini kwa mchungaji
 
Sirini ndiyo wapi huko,mambo ya sirini yanafanywa na madc na marc wanapowanunua wapinzani na wanapofanya mipango ya kuiba kura na maaskofu nao wafanye mambo sirini kama wezi?.
Watumishi wa Mungu hawatakiwi kuwa wanafiki. Wanatakiwa wapaaze sauti zao zisimike. Kama za mtu aliyeko nyikani kunyoosha mapito ya Bwana. Hizi siri ndizo zilimfanya Yuda akamsaliti Yesu.
 
Je, Polepole anakumbuka kuwa serikali yake ilikataa ombi la viongozi wa dini kuzungumzia 'operation ukuta'? Njia pekee ya kusonga mbele kama taifa ni kuheshimu katiba, kuheshimiana na kuthaminiana kama raia na kuweka mbele maslahi ya taifa. Kujua tatizo ni nusu ya ufumbuzi. Methinks 'root cause' ya tatizo letu ni hofu ya kupoteza nguvu za kisiasa. Dalili zilianza wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010. Kutokana na ushindani ghafla siasa iligeuka uadui na baada ya uchaguzi wanasiasa wetu wakawa kama nyati aliyejeruhiwa. Hali hii imeendelea kushika kasi; siasa sasa ni vita ya kufa au kupona. Utaifa wetu uko mashakani. Binafsi tangu wakati huo nimetokea kuamini kuwa watu pekee watakaoweza kulinusuru taifa hili na janga hili la uroho wa wanasiasa ni viongozi wa dini. Tunamshukuru Mungu kuwa miaka 2 tu baadaye, aliwainua viongozi hao na kulinusuru taifa na janga la katiba ya watawala badala ya ile ya wananchi. Tuwaombee viongozi wetu wa dini, Mungu azidi kuwainua na kuwatia nguvu.
 
Kuombewa muombewe hadharani, ila kukosolewa iwe sirini??
Bush it ...!!
 
Mkuu swala la ukuta ni la kikatiba na mambo ya kikatiba yanapelekwa mahakamani sio kuandamana.Katiba ibara ya 30 imeweka wazi,kama magufuli afuati katiba hujaambiwa uandamane umeambiwa uende mahakamani.sasa mahakamani hamjaenda mnataka kuandamana kweli?Na ule ukuta ungekula vichwa ving sana
 
Polepole na huyo mkuu wake wameshasoma upepo baada ya kuona hali ya uchumi inazidi kudorora. Wamenunua wapinzani ili wapate mvuto hawajafanikiwa, juzi kwenye uchaguzi ndio wakafanya ukatili wa kishenzi watu wakasema enough is enough. Sasa viongozi wa dini wamejua ukimya wao ni sawa na kumchekea kima kwenye shamba la mahindi.

Maaskofu wameamua kuwaambia waumini waamke kwani hapa hakuna utawala wa sheria bali kuna sheria za kikatili. Zile mbwembwe ccm walizoleta kwamba wanakubalika wamegundua walikiwa wanajilisha upepo ila hawakubaliki. Hizi kampeni wanazoendesha kwa kiburi kwenye uchaguzi uliosusiwa na wapinzani wakuu pia zimechangia sana viongozi wa dini kuamka huko walipokuwa wametulia.
 
Sasa ushauri ukiwa ni wa siri ni nani atajua kuwa watu wa dini wameishauri serikali!?🙂)
 
Huyu polepole nadhani harakaharaka linamfaa sana
Contradictions nyiiiingi
Mwambieni mtu wenu atubu acha hizi porojoporojo zake
Msilipangie Kanisa namna ya kuendesha shughuli zake jipangieni humo humo na ccm yenu dhalimu
Unakera sana wewe kijakazi
Muombewe hadharani Mkosolewe Gizani Why?
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuna chama kimezuiwa kufanya siasa?

Ndio, vyote visivyo na muwakilishi wa kuchaguliwa eneo husika. Tuume maneno tupendavyo ili kuhalalisha utashi wa rais lakini hii kusema eti ufanye siasa mahali ulipochaguliwa tu na siyo nchi nzima hiyo ni sheria ya mfukoni ya rais. Huu ni utashi wake na hakuna sheria ya hivyo.

Kama hufanyi siasa nchi nzima, unapataje wanachama wapya? Sera na ajenda zako zitafahamikaje kwa wananchi ili uwavutie. Katika vitu vinanifanya nisimuunge mkono Magufuli hata kwa hayo machache mazuri ni hii tabia yake ya kutuongoza kama watoto wa chekechea. Ni bora angeweka utaratibu wa kwamba mikutano ya siasa iwe mara moja au mbili kila mwezi. Sio yeye afanye siku yoyote atakayo ba popote yeye na chama chake kisha apangie wengine anavyotaka yeye.
 
Wapumbavu sana hawa kama ni sifa wamwagiwe hadharani ila kukosolewa hadharani hawataki ni makosa makubwa sana.

Huyu polepole nadhani harakaharaka linamfaa sana
Contradictions nyiiiingi
Mwambieni mtu wenu atubu acha hizi porojoporojo zake
Msilipangie Kanisa namna ya kuendesha shughuli zake jipangieni humo humo na ccm yenu dhalimu
Unakera sana wewe kijakazi
Muombewe hadharani Mkosolewe Gizani Why?
 
Kibanga ampiga mkoloni,mkoloni mweusi aliyewageuza waafrika wenzie kutoka nchi ya kusadikika DANGANYIKENI kuwa mabwege,tena mabwege kweli kweli.
 
Back
Top Bottom