Polepole anazidi kuwagombanisha watu badala ya kuwafanye wawe kitukimoja kupitia itikadi za dini,kwani anasema kwamba kiongozi wa dini akiwa na mwelekeo wa chama Fulani mtu wa chama kingine hawezi kwenda kwake kwa maana ya kwamba wana ccm wawe na maaskofu wao na wana chadema wawe na maaskofu wao kwa maana tu,wote ni wanachama wa chama husika,ameshindwa kuelewa kwamba askofu anaweza kuwa na itikadi ya chama Fulani lakini kwa upande wa dini akawa anawaudumia watu wa vyama vyote,hilo yeye Polepole halioni na kama ameshindwa kuliona hilo vipi ataona ualali wa mwana ccm kumuudumia mwana chadema katika hali ya kawaida? watu wenye mawazo kama ya Polepole hawatufai kabisa katika nchi hii ndio maana sasa hivi inaanza kujitokeza kwamba mwana chadema akipata tatizo kama alivyopata Lisu mwana ccm anashindwa kwenda kumuona na akienda anafikiriwa vibaya, hivyo polepole lazima aonywe mapema kwa huo mtazamo wake