Baada ya maaskofu kuliamsha dude kuanzia kipindi cha Salam za krismasi na salam za mwaka Mpya, hatimae katibu mwenezi CCM ndugu Humphrey polepole amejitokeza na kuwaomba maaskofu waishauri serikali sirini kwani kwa hali ilivyo sasa ni kama wanaidhalilisha, Rais yuko tayari kupokea ushauri na kuufanyia kazi.
My take
Kila shetani ana mbuyu wake ukimya wa maaskofu na mashehe umetuumiza sana kama taifa na sina shaka wameamuka usingizini baada ya Askofu niwemugizi kuelekezewa bomba la moshi, pia salam zangu za pole ziwafikie Clouds Media
Hivi wale viongozi wa Dini walioomba kukutana na Rais JPM toka mwaka juzi walishajibiwa? Nakumbuka ilikuwa kipindi cha sekeseke la operesheni UKUTA.
Nakumbuka wakati huo JPM alikuwa amepania kweli kweli kumwaga damu ya watanzania wanachama na wapenzi wa CHADEMA. Viongozi wa Dini walijitokeza kutaka kuweka mambo sawa, wakawaomba CHADEMA watulie, na wakaomba kukutana na JPM. Mpaka leo hilo halijafanyika, na ilibidi CHADEMA watumie busara tu kubadili gia ili UKUTA uendelee kwa njia nyingine. na kweli. mpamabano kati ya CHADEMA na serikali ya JPM umeendelea kwa namna mbalimbali na sura mbalimbali.
Imefikia wakati Viongozi wa dini wameona kwamba mambo hayaendi sawa. Alijitokeza Askofu NiweMugizi, akatoa rai yake. Serikali ikagadhabika na kumtisha kwa kumhoji uraia wake. alipoanza kujibu kwa kutumia Zaburi, na kusisitiza msimamo wake, JPM akajifanya yeye msanii, akampigia simu huku akijifanya kwamba wale waliomhoji uraia wamekosea. Thubutu yake! nani anaweza kujaribu kuhoji uraia wa Askofu, tena wa Kanisa Katoliki, ambaye husimikwa kwa uwakilishi wa Serikali Kuu, ni nani anayeweza kuthubutu kumhoji uraia bila taa ya kijani kutoka juu kabisa?
Maaskofu walipozidisha mashambulizi kipindi cha Krismasi, Serikali ikawatisha tena kwa kutishia kufuta makanisa. yule Katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani alifikia hatua kusema ni marufuku viongozi wa dini hata kusifia Serikali! Naona ikaonekana sasa wale Maaskofu makada wa CCM watafanyaje kazi zao? ikabidi jamaa arekebishe kauli. kusifia ni sawa. kukosoa hapana! Ni uchochezi!!
Ilipokuja nyundo ya Kakobe, Serikali ikakunja ndita. Je, Kakobe afunguliwe mashitaka ya uchochezi? Mmmhhh... hiyo haitalipa in the long run. hebu TRA jaribuni kumdhibiti kwanza. hapo hapo, wakati tunajipanga, hebu wewe Babu Seya njoo kwanza Ikulu unywe Juice na kupiga picha na JPM. hiyo ni kubadili ukurasa ili watu waongelee mengine kwanza.
Ni upuuzi tu. Haiwezekani kukiuka haki za raia wako halafu ukategemea kustawi, ukategemea Amani iwepo. Amani ni tunda la Haki. ni Haki tu ndio itaiokoa Serikali ya JPM kutoka minyukano kama hii. ukandamizaji kama huu wa kuvipiga faini vyombo vya habari, ni mbinu za KIFASHISTI ambazo hazitafualu asilani.
Maaskofu waongee sirini? upuuzi gani huu? na mpaka maaskofu wanaongea, ujue kuna mengi wamevumilia. lakini umefika wakati sasa imetosha. Enough!
DAWA NI KUTUBU!!