Hatimae nimeanza maisha ya geto

Bin Shaib

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
1,315
1,186
Bwana Yesu asifiwe,, Assaalam alykum wapendwa,,natumai hamjambo nyote kama kuna wenye udhaifu Mungu Baba atawarehemu.

Maada :
Hatimae nimejitegemea kigeto kama nilivyo waambia kwenye uzi niliouleta kipindi cha nyuma @Nimekukuwa, nataka kujitegemea.

Nimeishi kwa mjomba kwa mwaka na miezi kadhaa siku moja nikamwambia anko nataka nipange chumba akanizuia subiri kwanza usiwe na haraka ile pesa niliyo kuwa nayo akanikopa ..

Amekuwa akinikopa pesa hata hanirudishii, akanambia ntakupatia siku ukipanga chumba,, lakini wapi.
Namimi sitaki kumuomba hata senti maana fikira zangu nawaza labda kwa vile nilikuwa kwake ndo maana hataki kunirudishia .

Kuna baadhi ya ndugu kumkopesha ni shida na wakati huo pesa anapata zaidi ya ninazo pata lakini hulipwi.
Nikasema powa isiwe tabu.

Nikaendelea kupambana nikapata 150000/=
Nikaenda kuchukua godoro la 100000, nikalipia chumba miezi mitatu 30000 na iliyobaki nikachukua vyombo na sasa nimeyaanza maisha ya peke yangu ambayo ntapambana mimi kama mimi ,,toka nimehamia magetoni najiona niwa tofauti sana kuliko nilipo kuwa kwa anko,,.

Kwasasa naishi kwa uhuru sana,,najiongoza mimi mwenyewe na kuhusu swala la kula nalipangilia mimi ni muda gani nile ,, sio kama kupindi nipo kwa anko muda wa misele inatakiwa uwe home kwa ajili ya msosi..

Akili yangu inawaza mbali tofauti na zamani,, na nilikuwa nikipata pesa aslimia kubwa nilikuwa naitapanya tofauti na sasa mambo yalivyo..

Kila nikiwa nipo geto naangalia kipi kinahitajika getoni,, nikifanya hiki naona bado kuna kitu kingine kinahitajika magetoni.

Nimeamini ukiishi kwa mtu hutokuwa na malengo yoyote na mawazo kupanuka ni nadura sana..

Na sitaki kurudisha mpira kwa kipa hata siku moja.

Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kujitambua na kunijalia mipango yangu kwenda sawa.
©Bin Shaib Classic 2020.
 
Safi sana don’t look back, na usitishike na lolote hapo ndo utakuw mwanaume. Jitahid uwe na asset muhimu taratibu utafika.
 

Similar Discussions

17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom