Magnificient
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 1,177
- 734
Natumai ndugu zangu nyote wa MMU ni wazima, nami namshukuru MUNGU.
Baada ya kuwa na mpenzi wangu kwa muda kila mtu akiishi kwao kwa wazazi wake (takribani miezi 6 sasa) tumeridhia kuwa tunaendana na sasa tunaweza tukaoana na kuishi pamoja. Hapa nina amani kiasi na utulivu wa moyo sasa, isipokuwa tu sijajua muundo wa barua ya posa; anayejua tafadhali anisaidie mapemaaa tusije tukaandika barua ya kiofisi au ya kirafiki kama hizi tulizozoea kuombea kazi.
Pia nakaribisha maoni na ushauri juu ya mchakato mzima wa kuchumbia na kuoa, nikiwa na imani kuwa hapa MMU ndipo penyewe, kila kitu ni live bila chenga.
Natarajia kupeleka barua tarehe 10.05.2014, ingawa mshenga sijaconfirm kati ya rafiki yangu au kaka yangu kama hakuna tatizo.
Au hadi nimpate mzee? Kila kitu kinakaribishwa. Nawatakieni siku njema!