Hatimae Msanii R.Kelly ajisalimisha Polisi Mjini Chicago

Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,520
2,000
Mkongwe wa muziki wa RnB nchini Marekani, R.kelly amejisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi mjini Chicago baada ya kushtakiwa kwa tuhuma kadhaa dhidi yake.

Staa huyo ambaye jina lake kamili ni Robert Sylvester Kelly (52) alifanya hivyo baada mashitaka ya makosa 10 dhidi yake juu ya unyanyasaji wa kijinsia kwa wasichana wenye umri mdogo.

R.kelly aliondoka kwenye studio yake mjini Chicago na kuelekea moja kwa moja kwenye kituo cha polisi ambapo atashikiliwa kwa hatua za kisheria pamoja na kufikishwa mahakamani.

Hata hivyo R Kelly aliingia tena kwenye kashfa mpya ya wanawake wawili, Bi Rochelle Washington na Bi.Latresa Scaff ambao hivi karibuni walijitokeza mbele ya waandishi wa habari wakidai kuwa walishanyanyaswa kijinsia na mwanamuziki huyo miaka ya 1990.
Screenshot_20190223-120125.png
cdc25d300df6030bb530f4cfa0975277.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom