Hatimae Baba Mdogo wa Mwigizaji wa Filamu Marehemu John Maganga Aeleza Mkasa Mzima toka Alipoanza ku

Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,093
Points
1,500
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,093 1,500
Muigizaji wa tasnia ya Bongo Movie John Stephan Maganga ambaye filamu yake ya mwisho inayoweza kuwakumbusha watu wengi taswira yake, kwa wale wanaotaka kumjua ni “BAR AHMED” iliywashirikisha Nice na Irene Uwoya, ambapo Marehemu Stephano ali act kama Boss wa bar ambaye alimwambukiza gonjwa la ukimwi Irene Uwoya.
Baba yake mdogo na marehemu, ambaye pia naye ni mwigizaji, ameelezea mkasa mzima toka Stephan alipoanza kuumwa mpaka siku ya kifo chake jumamosi asubui ya wikiendi iliyopita.
Baba mdogo wa Stephano anasema, kabla ya kufikwa na umauti mwigizaji John alikuwa akisumbuliwa na homa ambapo alimpigia simu na kumweleza jinsi anavyojisikia ndipo akamwambia amngojee, kisha alimfuata na kumpeleka Hospitali ya Mwananyamala.
Aidha anaendelea na kusema siku ya pili yake John alimpigia simu na kumwambia bado anaumwa na wala hajisikii vizuri, kuona hivyo, baba yake mdogo akaenda nyumbani kwake na kumkuta amelala kwenye kochi anatoka jasho sana, akamuuliza, John vipi tena?, John akamjibu, tumbo linamuuma sana, ikabidi nimpigie simu Baba yake mzazi nimwambie tumpeleke Hospital Mwananyamala.
Tulipofika pale hospitali, kutokana na maelezo ya Stephano, madaktari wakaamua wampige X Ray na Utra Sound kwa sababu alikuwa na maumivu makali sana tumboni mwake. Baada ya majibu ya vipimo kutoka, madaktari, wakasema ana matatizo kwenye utumbo hivyo wanatakiwa wamfanyie upasuaji wa haraka.
Stephano aliingizwa chumba cha upasuaji, wakati sisi kwa maana ya mimi na baba yake tukiwa tumekaa, dokta alitoka na kutuambia mashine za kupumulia zina matatizo kwa hiyo tunafanya transfer ya kwenda Muhimbili kwa matibabu zaidi, hivyo zilifanyika taratibu na Stephano aliingizwa kwenye gari la wagojwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.
Baada ya kufika Muhimbili, Stephano aliingizwa chumba cha dharura (emergence room), na baada ya dakika kama 10 hivi, alitoka Doctor ambaye tunafaamiana naye na kusema kuwa, kwa tatizo alilonalo John, hatakiwi kufanyiwa upasuaji kama walivyofikiria madaktari wa Mwananyamala ambapo walidhani kuna utumbo umekatika.
Daktari huyo wa Muhimbili aliendelea kutuambia sehemu ambayo inaonekana kuleta matatizo ni sehemu ya kongosho ambapo vipimo vinaonesha ina matatizo, ime fell kwa hiyo ina mwaga maji kwenye tumbo ndiyo maana anapata maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa.
Baada ya maelezo hayo Dokta tunayejuana naye alitueleza kwamba mtaalamu wa tatizo hili hayupo na kwamba anategemewa kuja kesho yake asubuhi na kutuasa tuende nyumbani na kwamba watammwekea mashine ya kupumua na sisi turudi kesho.
Kesho yake asubuhi, ilikuwa ni siku ya jumamosi nilifika Muhimbili na kuonana na yule Dokta kama tulivyokubaliana usiku wa jana yake. Nilipokutana naye akaniambia nisubiri atanijulisha kinachoendelea. Nafikiri wakati huo ndipo mambo yaliharibika, kwa sababu yule daktari ambaye alimtaja kutokuwepo jana, alikuwa ndani anamshughulikia hivyo alikuwa anajaribu achomwe sindano ambayo ingeweza punguza makali ya sumu iliovuja toka kwenye kongosho au angewekewa drip ya maji lakini inaonekana jambo hili lilichelewa kufanyika.
Muda mchache baadae Dokta alitoka na kuniambia John hatuko nae tena, amefariki. Hicho ndicho kilichomtokea John kuelekea kifo chake. Mazishi yamepangwa kufanyika makaburi ya kinondoni kesho. Alisema baba mdogo wa muigizaji Stephano.
Bongo5 Tutaendelea kukupa update kadri tutakavyozipata. [h=3][/h]
 
lutayega

lutayega

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Messages
1,254
Points
1,225
lutayega

lutayega

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2012
1,254 1,225
inasikitisha sana yani tunatembea na magonjwa bila ya kufaham. R.i.p john
 
cacico

cacico

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
8,388
Points
1,250
cacico

cacico

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
8,388 1,250
Ndiyo maana kikwete and co wanakwenda apollo, germany na france! Ila sisi wakina kajamba nani ndiyo tunaishia mwananyamala, amana, temeke na muhimbili! Hakika dhambi hizi za hawa wachumia tumbo, watazilipa tu siku moja!! Imeniuma sana!

Halafu ulimboka akianzisha mapambano kudai vifaa na wataalamu anatupwa mabwepande, anang'olewa kucha na meno!!

Wote tutakufa, wote tutalipa kulingana na matendo yetu! Rip john! Mimi, kikwete, zoka, msangi na wote tu!! Tupo nyuma yako twaja!
 
Angel Msoffe

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Messages
6,796
Points
1,225
Angel Msoffe

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2011
6,796 1,225
R.i.p John & Sharobaro
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,093
Points
1,500
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,093 1,500
kifo chake ukisoma apo kilitokana na madaktari wazembe,na huduma mbovu ambazo zipo hospital za serikali na kutokujali,mtu amezidiwa unamwambia aje kesho!!! wala kifo chake siyo mipango ya mungu,tuamke tanzania siyo kila kifo mungu amepanga,mbona japan,na scandnavia countries watu wengi wanakufa kuanzia miaka 80,ina maana mungu amependa africa zaidi,wake up nigga
 
A

Anne deo

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2011
Messages
485
Points
225
A

Anne deo

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2011
485 225
mhh r.i.p john....yupo kwenye movie ya Mrembo kikojozi pia??? au nimechanganya majina?? duh ndo mwisho wa mwaka huu...tuombeane uzima!!
 
cacico

cacico

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Messages
8,388
Points
1,250
cacico

cacico

JF-Expert Member
Joined Mar 27, 2012
8,388 1,250
kifo chake ukisoma apo kilitokana na madaktari wazembe,na huduma mbovu ambazo zipo hospital za serikali na kutokujali,mtu amezidiwa unamwambia aje kesho!!! wala kifo chake siyo mipango ya mungu,tuamke tanzania siyo kila kifo mungu amepanga,mbona japan,na scandnavia countries watu wengi wanakufa kuanzia miaka 80,ina maana mungu amependa africa zaidi,wake up nigga
i second you my dear! yaani wapo radhi waendeshe mashangingi na kuruka kwenda nje kila kukicha badala ya kununua vifaa na kuboresha huduma za hospitali kwanza!! waweke madr kwenye mazingira mazuri ya kufanyia kazi, vifaa viwe modern etc!! NAICHUKIA CCM NA VIONGOZI WAKE WOTEEEEEEEE! NATAMANI KILA MWANANCHI ANGEVAA NGUO NYEUSI AU NYEUPE KULIKO KIJANI NA NJANO, ILI KUKAA MATANGA KWA MSIBA TULIO NAO WA KUTAWALIWA NA WATU WA-BINAFSI, PAMOJA NA TUFUNGE NA KUMUOMBA MUNGU PIA ATUPE KIONGOZI ATAKAYEWEKA MATAKWA YA WANANCHI HASAAAA AFYA MBELE! silly and corrupt government of ccm!
 
A

Anne deo

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2011
Messages
485
Points
225
A

Anne deo

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2011
485 225
kifo chake ukisoma apo kilitokana na madaktari wazembe,na huduma mbovu ambazo zipo hospital za serikali na kutokujali,mtu amezidiwa unamwambia aje kesho!!! wala kifo chake siyo mipango ya mungu,tuamke tanzania siyo kila kifo mungu amepanga,mbona japan,na scandnavia countries watu wengi wanakufa kuanzia miaka 80,ina maana mungu amependa africa zaidi,wake up nigga
apo umenena mkuu.angekuwa kizito au mtoto wa vizito wa nchi hii ndege ya emergency ingetua india baada ya dkka chache tu.Ndo ivyo watu hatufanani kiuwezo
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,093
Points
1,500
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,093 1,500
i second you my dear! yaani wapo radhi waendeshe mashangingi na kuruka kwenda nje kila kukicha badala ya kununua vifaa na kuboresha huduma za hospitali kwanza!! waweke madr kwenye mazingira mazuri ya kufanyia kazi, vifaa viwe modern etc!! NAICHUKIA CCM NA VIONGOZI WAKE WOTEEEEEEEE! NATAMANI KILA MWANANCHI ANGEVAA NGUO NYEUSI AU NYEUPE KULIKO KIJANI NA NJANO, ILI KUKAA MATANGA KWA MSIBA TULIO NAO WA KUTAWALIWA NA WATU WA-BINAFSI, PAMOJA NA TUFUNGE NA KUMUOMBA MUNGU PIA ATUPE KIONGOZI ATAKAYEWEKA MATAKWA YA WANANCHI HASAAAA AFYA MBELE! silly and corrupt government of ccm!
wabunge wana mkataba na hospital ya appolo uko india,wakitaka kuchek afya wanapanda ndege kwenda india,awajali raia waliopo nchini na ndio maana wanashindwa kuborosha huduma sababu wao awatibiwi tanzania,harafu mtu akifarik kutoka na uzembe uliopo wao ndio wa kwanza kusema sisi tulimpenda ila mungu kampenda zaidi,hakuna kitu kama icho,huduma mbovu za afya ndio zinachangia vifo kwa umri wa mtu ambaye ni kijana,watu wamezidi msingizia mungu kwa africa,mbona nchi ambazo zimeboresha huduma za afya watu awafi hovyo,inauma sana kuona raia masikin wa nchi wanataabika wakat nchi imebarikiwa rasilimali,ata mungu atatushangaa na ni dhambi kumsingizia kwa kila kitu
 
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
29,448
Points
2,000
Mamndenyi

Mamndenyi

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
29,448 2,000
Madaktari wakigoma kutaka vitendea kazi mnawapa mathusi matokeo ndo haya tutakwisha.
 
T-1000

T-1000

Senior Member
Joined
Feb 21, 2011
Messages
143
Points
195
T-1000

T-1000

Senior Member
Joined Feb 21, 2011
143 195
Madaktari wakigoma kutaka vitendea kazi mnawapa mathusi matokeo ndo haya tutakwisha.
nimemuona mpuuzi vuvuzela wa magamba kwenye msiba wa John, kwa kweli alinichafulia hali ya hewa na kuniharibia siku yangu, liserikali lake ndo source ya haya yote mpaka huduma mbovu kwenye afya wakati wenyewe wanatibiwa nje, nilitamani nimfanyie kitu mbaya sana we subiri tu... ipo siku
 
L

Leornado

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
1,533
Points
0
L

Leornado

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
1,533 0
jamaa amekufa kwa ukosefu wahuduma navitendea kazi kwenye hospitali zetu, eti mashine ya kupumulia mbovu?? rip john,so sad
 
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,019
Points
2,000
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,019 2,000
Ndiyo maana kikwete and co wanakwenda apollo, germany na france! Ila sisi wakina kajamba nani ndiyo tunaishia mwananyamala, amana, temeke na muhimbili! Hakika dhambi hizi za hawa wachumia tumbo, watazilipa tu siku moja!! Imeniuma sana!

Halafu ulimboka akianzisha mapambano kudai vifaa na wataalamu anatupwa mabwepande, anang'olewa kucha na meno!!

Wote tutakufa, wote tutalipa kulingana na matendo yetu! Rip john! Mimi, kikwete, zoka, msangi na wote tu!! Tupo nyuma yako twaja!

umeona eeh? Ccm haikubaliki
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
31,229
Points
2,000
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
31,229 2,000
apo umenena mkuu.angekuwa kizito au mtoto wa vizito wa nchi hii ndege ya emergency ingetua india baada ya dkka chache tu.Ndo ivyo watu hatufanani kiuwezo
mmh...kila nafsi itaonja kifo,tunatofautiana mda tu.
Hata ulalamike haisaidii..watu wanapelekwa st thomas na wanarudi ndani ya jeneza itakua apollo?.
Kampeni kwenye misiba HATUZITAKI.
 
G

gugu

Member
Joined
Nov 14, 2008
Messages
69
Points
95
G

gugu

Member
Joined Nov 14, 2008
69 95
Nimeuliza kwa sababu nilikuwa na raptured *Appendicitis* ambayo ilikua iniue. Ilirapture tumboni na kusababisha maumivu makali na tumbo kuvimba. Nilivyo enda hospitali ya TMJ walifanya ultra sound na scan wakasema ni uvimbe unatakiwa utolewe upelekwe ocean road. Nadhani wote mnajua mtu ukiwa referred ocean road ina maana moja tu kwamba ni cancer. Nililia sana lakini kwa bahati nilikua na ndugu yangu mmojs daktari aliichukua case yangu na kunifanyia operation walikuta ni Appendix iliyo raputure nakuenea tumbo zima. Nilisafishwa na mpaka sasa bado naugulia. Its not a joke. Kijana wa watu didnt have to. RIP
 
LiverpoolFC

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2011
Messages
11,021
Points
1,250
LiverpoolFC

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2011
11,021 1,250
Alale kwa Amani yake Bwana wetu!

Na ni wazi kabisa serikali yetu haiko makini na raia wake!
Serikali tawala inajijali wao kwa wao tu na kutusahau wanainchi!

MUNGU YUPO!
 
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Messages
13,093
Points
1,500
Money Stunna

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2011
13,093 1,500
jamaa amekufa kwa ukosefu wahuduma navitendea kazi kwenye hospitali zetu, eti mashine ya kupumulia mbovu?? rip john,so sad
kweli kabisa,inauma kumuwaisha kijana wa watu kabla siku yake ajafika
 
Forum statistics

Threads 1,295,830
Members 498,409
Posts 31,224,656
Top