Hatima ya walimu

Emmy Bonny

Member
Sep 24, 2016
16
45
Ndalichako mbona mawazo watutia,
Elimu tuliyo tuliyoIpata ajira twangoja,
Kila siku matamuko sisi wapi tupo tena,
Elimu tuliyo pewa ajira kuzingoja.

Angalia hali zetu uduni umetawala,
Bahati kuipata chuoni kutinga mrua,
Tukasoma kwa shida mpaka kung'amua,
Leo tena kwetu laana ajira kuzipata.

Tanzania gani ya viwanda sisi twaumia,
Ndege mwanunua sisi twashinda njaa, Elimu yetu tegemezi sisi tujiajiri da,
Elimu tuliyopewa ajira kuzingoja.

Ningekuwa msituni panga ningelishika,
Watu kuwapora nami kutangazwa kila,
Mawazo niliyonayo mola anijua mama,
Elimu tuliyopewa ajira kuzingoja.

Nilianza umachinga kibanda kutupiliwa,
Nikaenda mgodini mabomu nikapigwa,
Viongozi wapi wanyonge tupate raha,
Elimu tuliyopewa ajira kuzingojea.

Shairi la maumivu ya walimu wa
Mtaani
2015&2016
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom