Nimeangalia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nimeona hivi kuhusiana na hali inayofanana na hii aliyo nayo Mh. Chenge.
Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
Chenge amekutwa na hatia na amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja au faini 700,000Sh.
Sasa hatima ya Chenge inakuwaje baada ya hukumu hiyo?
Naomba wataalamu wa Sheria na katiba mtufafanulie vizuri.
ukisoma vema kifungu ulichonukuu kinasema mtu hatakuwa na sifa ya kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa mbunge.KIko wazi hakizungumzii mtu ambe ni mbunge tayari hivo kinawahusu wanaotaka kugombea au kuteuliwa kuwa wabunge. Kwa kifungu hiki Chenge tayari ni mbunge hivo hakiwezi kumbana labda kama kuna kifungu kinachosema mtu akishakuwa mbunge na akipataikana na hatia.Spika hawezi kutangaza jimbo lake wazi au vinginevyo.La pili Traffic offence ni tofauti na makosa mengineyo ndo maana hata kama ukigonga mtu akafa sio murder labda kuwe na vielelezo va kuonyesha umekusudia kuuwa.Kwa Chenge imeoneka ni kosa ndio aambalo imeanishwa ktk mojawapo ya Traffic offence na kapatikana na hatia ktk traffic offence na sio criminal offence ambayo iko ndani ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(criminal Procedure Act).Chenge bado ataendelea kutamba na vijisent vyake bungeni kama kawa. Ndo hivo nijuavo
KWA SHERIA NA KATIBa hii...the man hana hatia (YA KUNGOLEWA UBUNGE)
KWA SHERIA NA KATIBa hii...the man hana hatia (YA KUNGOLEWA UBUNGE)
@ mahesabu....another Kinyaa.....!
Katiba inasema:
No. 67 (2)
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
KWA SHERIA NA KATIBa hii...the man hana hatia (YA KUNGOLEWA UBUNGE)
Hapa nina pata kizunguzungu, Mi nadhani faini ni sawa na kifungo kile kile ila badala ya kufungwa unatoa pesa "yenyewe ndo inafungwa badala yako" Sasa kama angekosa faini akafungwa jela, je, angeendelea kuitwa Mh. Mbunge na akawa anahudhulia vikao vya Bunge? Mshahara, Posho na marupurupu mengine angeendelea kuyapata akiwa gerezani? Hapa napata kizunguzungu kwa sheria za bongo-ziko double standard!
Ukisoma vema kifungu ulichonukuu kinasema mtu hatakuwa na sifa ya kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa mbunge. Kiko wazi hakizungumzii mtu ambe ni mbunge tayari hivo kinawahusu wanaotaka kugombea au kuteuliwa kuwa wabunge. Kwa kifungu hiki Chenge tayari ni mbunge hivo hakiwezi kumbana labda kama kuna kifungu kinachosema mtu akishakuwa mbunge na akipataikana na hatia. Spika hawezi kutangaza jimbo lake wazi au vinginevyo. La pili Traffic offence ni tofauti na makosa mengineyo ndo maana hata kama ukigonga mtu akafa sio murder labda kuwe na vielelezo va kuonyesha umekusudia kuuwa. Kwa Chenge imeoneka ni kosa ndio aambalo imeanishwa ktk mojawapo ya Traffic offence na kapatikana na hatia ktk traffic offence na sio criminal offence ambayo iko ndani ya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai(criminal Procedure Act). Chenge bado ataendelea kutamba na vijisent vyake bungeni kama kawa. Ndo hivo nijuavo
KWA SHERIA NA KATIBa hii...the man hana hatia (YA KUNGOLEWA UBUNGE)
Hata kama hukumu imetolewa tayari akiwa mbunge,kosa alifanya kabla ya kuwa mbunge wa bunge la sasa,na kama hukumu ingetolewa mapema ina maana asingegombea ubunge,pamoja na huvyo suppose asingekuwa na hela ina maana angekuwa jela huyu jamaa hatakiwi kuwa mbunge ila kwa sababu tanzania haina accauntability let chenge injoy the free air from the sorrounging
mkuu....Rage was set free by his appeal being in favour of him..... therefore granted innocent...
Hapana yule alitoka kwa msamaha wa rais, na pia nakumbuka wakati wanamuhoji kituo fulani cha redio yeye alisema, siku hiyo ya msamaha asubuhi aliitwa na bwana jela na kuambiwa umepata msamaha wa rais kwa hiyo leo utatoka.
Hakutoka kwa rufaa.
Chenge atalindwa tu. Na ndiyo maana kesi yake wameichelewesha ili kipindi cha uchaguzi kipite na apite bila pingamizi. Maana hukumu kama hii ingetolewa mwenzi mmoja kabla ya uchaguzi, ilikuwa ni sababu tosha ya kumuweka kando.
najua sauti yetu kama waJF haitasikia kwa watawala, lakini bunge la sasa lina wabunge makini na wengine ni member humu ndani, basi tafadhalini hebu pelekeni hoja binafsi juu ya status ya ubunge wa Chenge baada ya hukumu hii ili tujue ni kifungu kipi this time mafisadi watatumia ku save the neck of their ally!
Hivi wachangiaji wengi humu wanakimbilia kutype kabla ya kusoma? Icho kifungu (c) ukisoma utaona kuna comma.