Hati za Muungano ndio hizi?

Hata hati za muungano zikiletwa hamtakubali mtaamisha magoli! Mlianza bendera mkapewa, wimbo wa taifa mkapewa, vyote mnavyotaka mmepewa sasa hata hati ikija hamtokubali. Angalau sasa mmedai nchi yenu na hili tutawapa yaishe salama ndugu zetu. Hatutaki Muungano!!!

Mwanakijiji, hayataisha salama! Wakipewa nchi yao haitakua imetosha! Dai litakuwa Tanganyika iliwadhulumu na kuwafanya maskini na watadai walipwe. It will be interesting kuona kama na riba itadaiwa au la!
 
Wakifikia hapo ni kuwavurumishia mabomu mpaka visiwa vyote viyeyukie baharini.
 
Hata hati za muungano zikiletwa hamtakubali mtaamisha magoli! Mlianza bendera mkapewa, wimbo wa taifa mkapewa, vyote mnavyotaka mmepewa sasa hata hati ikija hamtokubali. Angalau sasa mmedai nchi yenu na hili tutawapa yaishe salama ndugu zetu. Hatutaki Muungano!!!

I like thatt MM. We don't want this fake UNION. Let them go
 
Mzee Mwanakijiji, kuwapa Zanzibar nchi yao ni kuvunja muungano!, huu ni uhaini!. Tutatakacho wapa ni haki ya kuujadili ni muungano wa aina gani wanautaka na sio kuuvunja!.

ilikuwapo ussr na ikavunjika, sembuse muungano huu wa wala urojo na sembe?

time will come when things will fall apart.

msijiapize kabisa kwamba muungano hautavunjika. mnajidanganya.
 
Mwanakijiji, hayataisha salama! Wakipewa nchi yao haitakua imetosha! Dai litakuwa Tanganyika iliwadhulumu na kuwafanya maskini na watadai walipwe. It will be interesting kuona kama na riba itadaiwa au la!

watasema na Bandari ya Salama ni yao. hawa watu wa ajabu sana.
 
Hata hati za muungano zikiletwa hamtakubali mtaamisha magoli! Mlianza bendera mkapewa, wimbo wa taifa mkapewa, vyote mnavyotaka mmepewa sasa hata hati ikija hamtokubali. Angalau sasa mmedai nchi yenu na hili tutawapa yaishe salama ndugu zetu. Hatutaki Muungano!!!

Nchi si walishapewa kupitia mwafaka wa CUF na CCM. Wanachotaka sasa sio talaka rejea bali ni full talaka!
 
Mwanakijiji, hayataisha salama! Wakipewa nchi yao haitakua imetosha! Dai litakuwa Tanganyika iliwadhulumu na kuwafanya maskini na watadai walipwe. It will be interesting kuona kama na riba itadaiwa au la!

Na kweli madai kama haya yataibuliwa na akina Masanja na Maganga waliozamia kule watakuwa walengwa wa kwanza kabisa. Ni busara kuhakikisha majadiliano ya amani na uwazi yakafanywa. Kama wengi watataka Zanzibar yao basi wapewe kwa masharti ya kutoleta chokochoko baadae. Vinginevyo tutaleka mambo ya Sudan na South Sudan.
 
M-zenji wa kawaida mawazo yake ni kwamba muungano ni kama ndoa kati ya zenji na bara... kibaya ni uvumi kuwa zenji ndo imeolewa.....hilo ndo tatizo, labda tuwaambie wao ndo wameowa!!
 
Pasco unaposema kuwapa nchi yao una maana gani? kwani tuliwapora au kuwanyang'anya kinguvu? Mbona muungano ulishavunjika kitambo au wewe hujui kuwa zanzibar ni nchi yenye majeshi,bendera na wimbo wa taifa? Ni muungano gani wa nchi mbili unaolalia(egemea) upande mmoja,yaani kwamba wao waamie huku wajenge popote pale wafanye biashara,kazi waoe,wajenge misikiti,waendeshe migahawa,baa lakini sisi haturuhusiwi hata kuabudu kwa uhuru,kumiliki shamba au nyumba hata kuajiriwa kule ni shughuri,sasa huu ni muungano wa nama gani?
Wanadai Zenj-bar ilikuwa ktjj bara Arabu kikasukumwa na upepo kuja Afrika na wanaodai kuuvunja Muungano ni Wamanga, wamahra, waarabukoko na baadhi ya washirazi lakini sio Dini sasa uwape Unguja na Pemba wakati Bakhresa, Mzee Yusuf, Hadija Kopa wapo bara nani umpe hicho kisiwa?
Hapewi mwarabu asilani atarudisha Utumwa na Utwana km wanabisha wajibu kwa nini wabantu wanatuita Punda na wao Farasi? (PUNDA hapandi MUSCAT)
 
Mzee Mwanakijiji, kuwapa Zanzibar nchi yao ni kuvunja muungano!, huu ni uhaini!. Tutatakacho wapa ni haki ya kuujadili ni muungano wa aina gani wanautaka na sio kuuvunja!.

Pasco siamini ulichokiandika kuwa una uwezo wa kuwaamulia Wazanzibari hata sisi Watanganyika kuhusu Muungano. Tatizo la muungano kivyangu ni kuwa mimi sikuwa sehemu ya maamuzi ya kuungana kwa hiyo ni sawa kabisa sijui na labda ni kweli sistahili kujua hata makubaliano hayo. Nilichoshudia ni kero za muungano zisizoisha na vurugu zisizo na maelezo kutoka kwa wenye muungano wao kuukomalia.

Kwa kweli napenda muungano usiwepo kabisa kwa kuanzia; ili tukiona tafrani ya bila kuishi bila muungano tutie akili ya kuuhitaji muungano upya. Mbona tumefanya hivyo kwa EAC. Kimaisha huzika mbegu ardhini ndipo huchipua na kuzaa kwa wingi. Tuuzike muungano kama una faida utachipua tu.
 
Jana nilikutana na hii https://www.jamiiforums.com/katiba-mpya/271339-prof-shivji-ametumwa-na-wazanzibari.html#post3965455

Kama kweli Serikali ya Tanganyika ina nia njema na Zanzibar na kuamini juu ya misingi ya Muungano wenye maslahi ya pamoja na fursa sawa (win - win situation) na kwamba Zanzibar inafaidika na mfumo wa Muungano uliopo ! SUALA:

Je, Serikali ya Tanganyika iko tayari katika kufuata mfumo na utaratibu huo huo iliyouasisi kwa kuona Zanzibar ambayo ni mbia na mshirika wake - inafutika, na badala yake iingie ndani ya Serikali ya Muungano kama vile ilivyo sasa Tanganyika ndani ya Serikali ya Muungano? Yaani tuwe na Serikali ya Tanganyika na ile ya Muungano badala ya kuwa na Serikali ya Zanzibar na ile ya Muungano.

Na kwamba Makao Makuu ya Serikali ya Muungano yawe Zanzibar?

Na kwamba Tanganyika ipate 4.5% katika mgao wa mambo ya Muungano kama inavyopata sasa Zanzibar?

Na kwamba Tanganyika kwa kipindi cha miaka 48 isiwe na: Polisi yake, usalama, usafiri wa anga, bandari, leseni za viwanda, ushirikiano wa kimataifa, utafiti, takwimu, ushuru wa bidhaa, kodi ya mapato, biashara za nje, simu, posta, elimu ya juu, mafuta na gesi asilia, uraia, uhamiaji, Mahakama ya rufaa, mambo ya nje, mikopo ya nje, sensa ya watu na baraza lake la mitihani - na kwamba yote haya yawe chini ya mamlaka ya Zanzibar? Kwa nini hamkubali tubadilishane kwa utaratibu huo muliouweka?

Kuna yeyote kati yetu ambaye amewahi kufikiri huu Muungano kama huyu Abdul 28?

Tunaichukuliaje changamoto aliyoitoa hapa? Kuwa Tanganyika ichukue nafasi ya Zanzibar katika Muungano wa Tanzania na Zanzibar ichukue nafasi ya Tanganyika kama ilivyo katika Muungano wa Tanzania.

Gonga link https://www.jamiiforums.com/katiba-...ji-ametumwa-na-wazanzibari-2.html#post3965820

Je changamoto hii wewe msomaji inakufanya upunguze jazba na kufikiria upya "Muungano wa aina hii tulionao" au unapata hasira zaidi na kuona Muungano wenyewe ni kero?

Kero huondolewa au hutatuliwa? Au ni jambo jema kuzipuuza kero na kutegemea zitajitatua zenyewe?
 
Hata hati za muungano zikiletwa hamtakubali mtaamisha magoli! Mlianza bendera mkapewa, wimbo wa taifa mkapewa, vyote mnavyotaka mmepewa sasa hata hati ikija hamtokubali. Angalau sasa mmedai nchi yenu na hili tutawapa yaishe salama ndugu zetu. Hatutaki Muungano!!!

Dawa ya hawa wasiokubali (wabishi) ni Maji washa washa na Majeshi toka Bara. Muungano hatuuvunji ng'o...
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji , kuwapa Zanzibar nchi yao ni kuvunja muungano!, huu ni uhaini!. Tutatakacho wapa ni haki ya kuujadili ni muungano wa aina gani wanautaka na sio kuuvunja!.
Wanabodi,
Leo sikukuu ya Muungano, nafanya mapitio ya baadhi ya mabandiko ya muungano.

Japo waasisi wa muungano wetu huu adhimu ni Nyerere na Karume, muungano ni kama ndoa, kuna mtu ana proposes, mwingine anakubali, ndoa inafungwa. Kwenye muungano wetu huu adhimu, aliye proposes ni Nyerere, Karume akakubali. Nia ya Nyerere ni kwenda kwenye serikali moja. Wito kwa viongozi wetu, kama nia ya kweli ni kudumisha muungano, twende kwenye serikali moja. Tumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kuyaishi maono yake!. Nawatakia Muungano Mwema.

Paskali
 
Back
Top Bottom