Asante, Wililiki kwa charge sheet.
Kilichofanyika leo, ni kuandaa hati ya mashitaka kwa mtindo wa zimamoto hivyo kulipua lipua tuu ili kutimiza matakwa ya kisheria ya kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24 tangu kukamatwa.
Kisheria, kwa charge sheet hiyo, pale hakuna kesi, kwanza ni bailable na pili its nothing!.
Angalizo, mabingwa wa kuchakachua kesi wa polisi toka polisi makao makuu, wameshatua mjini Arusha leo, kutengeneza kesi ya msingi, hivyo klesi itakapotajwa tena, serikali, itabadilisha hati ya mashitaka kwa kuwageuzia kibao Chadema kuwa ndio waliosababisha vifo vile, msishangae kama itageuzwa muder case 'unbailable!' jamaa kushikiliwa na polisi, by the time wanaachiwa, mabingwa wa kufanya mambo, watakuwa wameshafanya mambo, wakitoka tuu, sio wale wale waliongia, bali wengine kabisa!
Kusema kweli, kuna wakati huwa namkumbuka spika Sitta, asingekubali, wabunge wa Bunge lake wadhalilishwe namna hii kwa sababu za kipuuzi zisizo na kichwa wala miguu!.