Hati ya mashtaka waliosomewa chadema hii hapa

Hati ya mashtaka waliosomewa chadema hii hapa

naamin tunakoelekea sipo, ipo siku tutashindwa kwan uanaweza fanya watu wachache kuwa wajinga kwa muda mfupi na sio wote kwa muda wote.
 
Na polisi nao washtakiwe kwa kuua!
wanaJF hii hati ya mashtaka ni defective(mtanisamehe kwa kuchanganya lugha) kwanza wakili wa serikali alieiandaa anajua kabisa hawa watu hawana hatia au ni mbumbumbu wa sheria.Unamshitakije mtu kwa unlawfull assembly wkt tayari walipewa kibali cha kukutana na kufanya mkutano? Pili ni ngumu kuthibitisha pasipo mashaka watu wote waliotajwa kama waliandamana manake kumkuta mtu barabarani na kumkamata si uthibitisho alikuwa anandamana hapo kuprove ni ngumu sana.tatu dr Slaa alikamatwa hotelini kwake sasa utasemaje kafanya unlwfully assembly wkt alihutubua mkutano halali ulioruhusiwa? pia breach of peace imesababishwa na police wenyewe manake hao wanachadema walishava vitambaa vyeupe kuonyesha amani na hawakufanya vurugu yoyote hadi polisi walipoanza kuwatibulia na pia haipo wazi hawakutii amri gani ya kamanda wa polisi ya kutohudhuria kwenye mkutano au kuandamnana kwani unapoenda kwenye mkutano unapita anagani au unatembea sasa kama walitembea wakiwa wanaelekea kwenye mkutano nayo ni makosa? kwani walifunga barabara na kuzuia shughuli za kawaida kuendelea Arusha? hii kesi ni ya kiupuuzi tu na hata hati ya mashtaka imeandaliwa kizushi haina msingi wowote.nadhani Mabere marando aatafanya fasta hiyo kesi ifutwe haina msingi wowote kisheria waziachie mahakama ziendeshe mashauri mengine ya maana.Wakili Maranado atatoa pingamizi la hiyo charge sheet mapema tu kesi ifutwe mchakato wa kutafuta demokrasia ya kwei uendelee.
upuzi mtupu nadhani hata huyo wakili wa serikali anafanya kazi kisiasa na sio kama mtetezi wa haki za msingi za binadamu sijui kasoma chuo ghani huyo.
 
Asante, Wililiki kwa charge sheet.
Kilichofanyika leo, ni kuandaa hati ya mashitaka kwa mtindo wa zimamoto hivyo kulipua lipua tuu ili kutimiza matakwa ya kisheria ya kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24 tangu kukamatwa.

Kisheria, kwa charge sheet hiyo, pale hakuna kesi, kwanza ni bailable na pili its nothing!.
Angalizo, mabingwa wa kuchakachua kesi wa polisi toka polisi makao makuu, wameshatua mjini Arusha leo, kutengeneza kesi ya msingi, hivyo klesi itakapotajwa tena, serikali, itabadilisha hati ya mashitaka kwa kuwageuzia kibao Chadema kuwa ndio waliosababisha vifo vile, msishangae kama itageuzwa muder case 'unbailable!' jamaa kushikiliwa na polisi, by the time wanaachiwa, mabingwa wa kufanya mambo, watakuwa wameshafanya mambo, wakitoka tuu, sio wale wale waliongia, bali wengine kabisa!

Kusema kweli, kuna wakati huwa namkumbuka spika Sitta, asingekubali, wabunge wa Bunge lake wadhalilishwe namna hii kwa sababu za kipuuzi zisizo na kichwa wala miguu!.

Pasco, kwa charge hii tayari Mwendesha mashitaka amejifunga bao badala ya kuokoa! Ikiwa watabadilishiwa mashitaka watakuwa wamejifunga bao la pili na ndipo tutajua kuwa Polisi wanahujumu Vyama vya Upinzani kwa kushinikizwa na Serikali.
 
simshangai kishongo, kabila lao washawahi kudai uhuru wa watu wa mlima wao tu kutoka kwa wakoloni, wanajijua hao
 
wanaJF hii hati ya mashtaka ni defective(mtanisamehe kwa kuchanganya lugha) kwanza wakili wa serikali alieiandaa anajua kabisa hawa watu hawana hatia au ni mbumbumbu wa sheria.Unamshitakije mtu kwa unlawfull assembly wkt tayari walipewa kibali cha kukutana na kufanya mkutano? Pili ni ngumu kuthibitisha pasipo mashaka watu wote waliotajwa kama waliandamana manake kumkuta mtu barabarani na kumkamata si uthibitisho alikuwa anandamana hapo kuprove ni ngumu sana.tatu dr Slaa alikamatwa hotelini kwake sasa utasemaje kafanya unlwfully assembly wkt alihutubua mkutano halali ulioruhusiwa? pia breach of peace imesababishwa na police wenyewe manake hao wanachadema walishava vitambaa vyeupe kuonyesha amani na hawakufanya vurugu yoyote hadi polisi walipoanza kuwatibulia na pia haipo wazi hawakutii amri gani ya kamanda wa polisi ya kutohudhuria kwenye mkutano au kuandamnana kwani unapoenda kwenye mkutano unapita anagani au unatembea sasa kama walitembea wakiwa wanaelekea kwenye mkutano nayo ni makosa? kwani walifunga barabara na kuzuia shughuli za kawaida kuendelea Arusha? hii kesi ni ya kiupuuzi tu na hata hati ya mashtaka imeandaliwa kizushi haina msingi wowote.nadhani Mabere marando aatafanya fasta hiyo kesi ifutwe haina msingi wowote kisheria waziachie mahakama ziendeshe mashauri mengine ya maana.Wakili Maranado atatoa pingamizi la hiyo charge sheet mapema tu kesi ifutwe mchakato wa kutafuta demokrasia ya kwei uendelee.
upuzi mtupu nadhani hata huyo wakili wa serikali anafanya kazi kisiasa na sio kama mtetezi wa haki za msingi za binadamu sijui kasoma chuo ghani huyo.

Sijawahi kuona HATI FEKI kama hii maishani..... shame on you.

Njia pekee hapa ni kufuta kesi isiyo na tija. Nguvu ya dola haiwezi kushinda nguvu za hoja/umma. Hawa watu waachiwe na walioua WASHTAKIWE kwa OCAMPO MARA MOJA.
 
Baada ya kuisoma kwa umakini hati ya mashtaka ya viongozi wanaoshitakiwa wa Chadema pamoja na watu wengine zaidi ya 20 nimetafakari na nimeona nitoe mchango wangu hapa JF.

Kwanza kabisa wana-Chadema wa mkoani Arusha walikuwa wanatekeleza haki yao ya kimsingi kabisa waliyopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara ya 20(1) ya KATIBA ya jamhuri ya Muungano wa tanzania inampa Mtanzania yeyote haki ya kuwa huru, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani. Ibara hii inasema hivi;

"Kila mtu anastahili kuwa huru, bila kuathiri sheria za nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo."


Sasa tuiangalie hati ya mashtaka. CDM wanashtakiwa kwa kosa moja la Unlawful Assembly Contrary to Sections 75 and 74 of the Penal Code, Cap. 16 Volume 1 of the Revised Edition, 2002 read together with Section 45 of the Police Force and Auxiliary Services Act, (PFAS) Cap. 322 of the Revised Edition, 2002.

Hebu tuviangalie vifungu hivi kwa undani tukianza na kimoja baada ya kingine;

Kifungu cha sheria namba 74 (Penal Code):

"When three or more persons assemble with intent to commit an offence or, being assembled with intent to carry out some common purpose, conduct themselves in such a manner as to cause persons in the neighborhood reasonably to fear that the persons so assembled will commit a breach of the peace or will, by that assembly needlessly and without any reasonable occasion, provoke other persons commit a breach of the peace, they are an unlawful assembly"


Kifungu hiki cha sheria kinakataza watu ambao maandamano/wao unaonekana kuleta hofu, kuvuruga amani au kuwashawishi/kuchochea vurugu wakati wa maandamano hayo. Ni wazi kuwa CDM walishatangaza kufanya maandamano ya amani na kuwa wamepewa kibali cha kufanya maandamano hayo. Nia ya maandamano hayo yalikuwa ni kupinga ufisadi wa Kikwete na Serikali yake na kuutangazia umma kuwa matokeo yaliyotangazwa ya urais hayakuwa halali. hakuna mahala popoye CDM walimchochea au kumshawishi mtu kuleta vurugu. Hivyo basi ni kazi yao kuithibitishia Mahakama kuwa CDM walichochea watu kufanya vurugu na kutishia amani ya watu.


Kifungu cha sheria namba 75:

"Any person who takes part in an unlawful assembly is guilty of an offence and is liable to imprisonment for one year"

Kifungu cha sheria namba 45 (PFAS):

"Any assembly or procession in which three or more persons attending part neglect or refuse to obey any order for dispersal given under the provision of subsection (4) of section 43 or section 44, shall be deemed to be an unlawful assembly, within the meaning of section 74 of the Penal Code"

Kifungu hiki kinaeleza kuwa ikitokea mkusanyiko/maandamano ya watu zaidi ya watatu yanafanyika na kwamba maandamano hayo yameshindwa kutii amri ya kuzuia yasifanyike chini ya kifungu namba 43 kifungu kidogo cha (4) cha sheria za Polisi (PFAS) au kifungu cha 44, basi maandamano hayo yatakuwa ni kinyume na sheria/batili kama ilivyotafsiriwa kwenye kifungu namba 74 cha makosa ya jinai.

Kifungu namba 43(4) (PFAS):

"The officer in charge of Police may stop or prevent the holding or continuance of any assembly or procession in a public place which has been convened, collected, formed or organized otherwise than in accordance with the notification under subsection (1)…………give or issue such orders as he may consider necessary or expedient, including orders for the dispersal of any such assembly or procession as aforesaid"


Kifungu hiki kinasema kwamba Ofisa anyehusika wa Polisi (kwa tafsiri yangu) anaweza kuzuia maandamano/mkusanyiko wowote katika eneo la wazi/ umma ambayo yamepangwa kufanyika bila kibali kinachohitajika kama ilivyoelezwa kwenye kifungu namba 43(1). Pia Ofisa huyo anaweza kutoa amri ikiwa ni pamoja na maandamano hayo kufanyika.

Kifungu namba 43(1):


"Any person who is desirous of convening, collecting, forming or organising any assembly or procession in any public place shall, not less than forty eight hours before the time when the assembly or procession is scheduled to take place, submit a written notification of his impending assembly or procession to the police officer in charge of the area specifying;
(a0 the place and time at which the meeting is to take place;
(b) the purpose in general of the meeting


Kifungu hiki kinasema kwamba mtu yeyote anayetaka kufanya maandamano ya umma anatakiwa kutoa notisi/taarifa ndani ya muda usiopungua masaa 48 kabla ya maandamano/mkutano huu kufanyika, kuonesha ni wapi mkutano huo utafanyika na lengo/dhumuni lamkutano huo. Hivyo basi kwa maana ya vifungu hivi viwili 43(4) na 43(1), CDM walikuwa na haki/uhalali wa kufanya mkutano ule kwasababu kuu 2 kwamba walishatoa notisi (kwa mujibu wa Dr. Slaa) inayoonesha wapi mkutano ungefanyika (viwanja vya NMC) na dhumini la mkutano huo (kupinga ufisadi wa serikali ya Kikwete)...kazi kwao hao waliowafungulia mashtaka kupinga ukweli huu

Kifungu namba 43(2):

"Where a person submits a notification in accordance with subsection (1), he may proceed to convene, collect, form or organize the assembly or procession in question as scheduled unless and until he receives an order from the Police Officer in charge of the area directing that the assembly or procession shall not be held as notified"

Kifungu hiki kinaeleza ya kwamba mtu akishatoa nitisi ya kufanya maandamano kama ilivyoelezwa kwenye kifungu kidogo (1) basi anaweza kuendelea na mkutano/maandamano hayo isipokuwa tu kama akipokea amri kutoka kwa Polisi anayehusika ikimtaka asifanye maandamano hayo.

Kifungu namba 43 (3):

"A Police Officer to whom a notification has been submitted pursuant to subsection (1) shall not give a stop order under subsection
(2) in relation to the notification unless he is satisfied that the assembly or procession is likely to cause a breach of the peace or to prejudice the public safety or to the maintenance of public order or to be used for any unlawful purpose"

Kifungu hiki kinafafanua kuwa Afisa wa Polisi ambaye amepokea notisi ya maandamano hayo HARUHUSIWI KUZUIA maandamano/mkutano huo ISIPOKUWA/HADI HAPO atakapojiridhisha kuwa mkutano/maandamano hayo yatasababisha uvunjaji/ukosefu wa amani au kukosekana kwa usalama kwa jamii au kwamba mkutano/maandamano hayo yanafanywa kwa madhumuni mabaya/kutaka kuvunja sheria.

Kwa vifungu hivyo hapo juu 43(2) na 43(4) Polisi wana kazi kubwa ya kudhibitisha kuwa CDM walikuwa na nia ya kusababisha machafuko kwenye mkutano/maandamano yao kwani wao (CDM) wana vibali vyote vilivyotolewa na jamhuri kuruhusu mkutano huo), kitendo cha IGP Said Mwema kutoa agizo la maandamano hayo kusitishwa mara moja kwa sababu za 'ki-intelijensia' sijui aliangalia sheria gani na yeye ni mwanasheria aliyebobea, sina hakika kama alikuwa akifahamu lengo la CDM au kama alioneshwa makaratasi yao.

Kifungu cha namba 44 (PFAS):

"The officer in charge of Police may stop or prevent the holding or continuance of any assembly or procession in any place whatsoever if, in the opinion of such officer the holding or continuance, as the case may be, of such assembly or procession breaches the peace or prejudices the public safety or the maintenance of peace and order may, for any of the purposes aforesaid, give or issue such orders as he may consider necessary or expedient, including orders for the dispersal of any such assembly or procession."

Kifungu hiki kinaeleza kuwa Ofisa in charge wa Polisi anaweza kuzuia maandamano/mkutano usifanyike mahala popote kama ataona kuwa endapo mkutano huo utafanyika basi utavunja/kuvuruga usalama na amani iliyopo. katika sheria za ushahidi kuna kitu kinaitwa "Incumbet Probatio quodi sit non que negat (he who alleges must prove) hivyo basi hapa ni kazi yao polisi kuja kutoa ushahidi ni sababu zipi zilipelekea wao kudhani kuwa endapo wangeruhusu maandamano hayo kufanyika basi usalama na amani vingekuwa hatarini.

KAZI KWAO POLISI CHADEMA SISI TUENDELEZE MAPAMBANO WATANZANIA WAPENDA HAKI TUSIOGOPE VIONGOZI WETU WAKO MAHALI SALAMA KATIKA MUDA MUAFAKA. PIA TUSISAHAU KUWA TUNA WATU MAKINI WALIOBOBEA KATIKA FANI HII KAMA MABERE NYAUCHO MARANDO NA TUNDU LISSU, HAWA NINA IMANI KAZI HII WATAIFANYA BARABARA.
Stand to be corrected.
 
Hii kali lakini iko siku kitaelewekaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa:spider:
 
Back
Top Bottom