Hatari!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatari!!

Discussion in 'JF Doctor' started by Janja PORI, Aug 18, 2011.

 1. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  jamani naomba wataalamu mnisaidie Na mtoto ana Miaka 3 hajajua ongea je kuna hatari ya yeye kuwa Bubu na je kilema cha ububu ni cha kurisi? Au genetics transimision?
   
 2. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #2
  Aug 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dr Riwa yupo najua atakuja kusaidia hili. Mie mwanangu alichelewa sana kuongea nahisi kutokana na kukaa na dada wa nyumbani muda wote hivyo hakutani na watoto wenzake, nlichoamua kufanya ni kumpeleka chekechea hii imenisaidia sana sasa hivi ana 4yr anaongea vizuri sana na alianza akiwa na 2yrs.
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Aug 18, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Laura unanitafutia kesi hivooo...mie sina jibu la kila swali au usahuri kwa kila tatizo. Ila kwa kuchangia ni kuwa....mara nyingi 'ububu' husababishwa na kutosikia. Mtoto akiwa kiziwi, hajawahi kusikia sauti yeyote, basi hawezi kusema zaidi ya ile bee beee bee na kutoa ishara.

  Natumai mpaka mwanao anafika miaka mi3 utajua tu kama anasikia au la, mwanao anasikia? kama anasikia basi si bubu, ana tatizo jingine tuu.

  Maswali machache kabla sijachangia zaidi...
  - Je, mwanao alilia mara tu baada ya kuzaliwa? au walimgeuza geuza na kumpiga piga na kumpitisha mpira puani ndio akalia? alilazwa kwa siku kadhaa hospitalini baada ya kuzaliwa akihitaji msaada wa mashine ya kupumulia?
  Kwa sababu mtoto anapochelewa kulia baada ya kuzaliwa, basi anachelewa kupumua mwenyewe na hivyo kuchelewa kupata damu yenye oxygen ya kutosha kwenye ubongo na kuathirika. Athari hizi za ubongo huchelewesha makuzi yake kiakili na wakati mwingine hata kimwili.

  - Je, mtoto wako amechelewa katika makuzi, mfano alichelewa kukaza shingo? alichelewa kukaa, kutambaa, kusimama, kutembea n.k?
  Kama ni hivyo kuna uwezekano mkubwa alipata athari nilizosema hapo juu.

  - Je, mtoto wako hana matatizo ya ulimi mfano ulimi mkubwa, au umevimba na kujaa mdomoni? Je ana kinyama kimeshikilia ulimi ukikagua chini ya ulimi (Tongue tie)?
  Tongue tie ni vigumu kunotice kama mama hamuwa makini, kanashikilia ulimi kwa chini basi mtoto anachelewa kuongea, huwa kinakatwa kwa operation hospitali..

  Nijibu niendelee..
   
 4. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #4
  Aug 18, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Janja Pori nadhani maswali ya Dr Riwa umeyaona hebu mpe majibu tuone anatusaidiaje. Kusema kweli nikiona mtu ameleta tatizo hapa JF naamini kabisa anasaidiwa kama mimi ulivyonisaidia. Ila nitakuwa member mbya kwelikweli sijawahi hata kushukuru. Nisamehe.
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,529
  Trophy Points: 280
  thank u dr. riwa.
   
 6. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  Riwa mtoto amekua vizur na mtundu mjanja na wakati wa kuzaliwa alilia kama kawaida tu ulimi nadhan upo fiti
   
 7. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Basi kama hana worry yeyote kati ya hizo nilizotaja hapo (kwa sababu kwa hao wanahitaji special care ili kukua hasa kiakili), then tumshukuru mungu hana tatizo kubwa...na inawezekana ni delay tu ya kawaida. Japokuwa si kawaida mtoto wa miaka mi3 kuwa hajaanza kusema, lakini kuna wakati inatokea watoto wanabehave tofauti na zole expected trends za development.
   
 8. L

  Laura Mkaju Senior Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa Dr Riwa amesema haoni tatizo lolote, mie nashauri kama kuna chekechekea maeneo ya karibu na kwako mpeleke akachanyike na wenzake ili aongeze speed kidogo kule atakutana na watoto wenzake. Naamini kabisa kwa michezo ya watoto ilivyo atakuwa vizuri tena mwambie mwalimu wake kabisa mtoto amelepekwa ili ajifunze kuongea itasadia.
   
 9. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mng'atishe sungusungu mdomoni
   
Loading...