Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni

Hatari za kuweka picha za mtoto mtandaoni

I am off to bed. Tufanye mmeshinda. Ila soma baadhi ya comments humu utaelewa nachosema. Kuna watu wanawaona wengine malimbukeni kisa wanafanya kila ambacho wao hawapendi. Sasa huko si ndo kunaitwa kujudge watu? Kwanini umuite mtu mwingine limbukeni kisa anaishi si vile wewe unataka. Endeleeni na topic yenu
 
Sijasema mimi niko sahihi. Nimesema tuache kuhukumu. Kipi unachodhani ni sahihi. Ningehukumu ningeanza kwa kukosoa thread kwa kusema kitu sahihi ni hiki. Bali nimekuwa neutral kwa kusema it is good not to judge people. That is just a sobher statement. Si reason kwa emotions.

Na hakuna aliye hukumu kwenye uu Uzi mwenye hayo mamlaka ni Mungu tu sisi hapa tunatoa mawazo yetu na hayayajalenga kumhukumu mtu only mitazamo tu we ubase kwenye kuhukumu tu why??? Umekimbilia huko hizo ndo emotions zenyewe zinazokufanya uhisi watu wakitoa michango tofauti na wako ufikiri wanahukumu hapo upo kihisia zaidi kuliko reality
 
Unapoanzisha uzi uweke na facts na evidence. otherwise keep your opinion to yourself.
 
Na hakuna aliye hukumu kwenye uu Uzi mwenye hayo mamlaka ni Mungu tu sisi hapa tunatoa mawazo yetu na hayayajalenga kumhukumu mtu only mitazamo tu we ubase kwenye kuhukumu tu why??? Umekimbilia huko hizo ndo emotions zenyewe zinazokufanya uhisi watu wakitoa michango tofauti na wako ufikiri wanahukumu hapo upo kihisia zaidi kuliko reality
Tufanye upo sahihi. Good night
 
Khaaaa!!Kwahiyo watu wasiwe proud na watoto wao kwasababu tu wanaweza kuharibika?! Kwamba mtu asiwe proud kwasababu kuwa proud hamna maana?!

Kweli tunatofautiana. Utaachaje kuwa proud na kitu unachokipenda?! Mtoto wako mwenyewe uache kusikia fahari jinsi alivyo na afya, jinsi alivyo mjanja, jinsi alivyo na akili, mzuri n.k kisa tu anaweza akaja kuwa mbaya ukubwani?! Unajua hata kitu kinachochangia mtoto kukua vizuri kihisia, kisaikolojia na kiakili ni ufahari anaonyeshwa na wazazi wake?!

Ufahari unaouona online ndo ule ule wa nyumbani na mitaani, tofauti ni kwamba unakuwa shared na wengi. Au hujawahi kukuta mzazi akielezea mtoto wake alivyo hivi au vile, ama watu wakishare ndani ya nyumba vitu vya kijanja na vya akili alivyofanya mtoto wakati mmoja akiwa hayupo. Au hata kwa mawasiliano ya simu kwa waliopo mbali?! It's the same thing sema tu kwa upana zaidi.

Binafsi kama nyumba kubwa sioni ubaya wowote wa mtu kuwa proud na mtoto wake. Kama wewe una aibu na wakwako jipe all kind of excuses, hata nje usitoke nae ukiogopa kesho akianza kuvuta sigara utajificha wapi.

Lizzy yakupasa utambue kila mwanadamu anapenda kusifiwa. namna ya kutafuta sifa hizo ndipo tunapotofautiana. Mimi naamini unaweza kuwa proud na mwanao bila ya kumuanika ktk mitandao. kupata mtoto tu sio kigezo cha kumuanika kwenye mitandao ili upate sifa. unaweza kupata sifa mzuri kwamtoto huyo kutokana na uwezo wake au vipaji alivyonavyo.

Kwani kizuri hakihitaji sifa coz by nature tayari ni kizuri, acha proud zikufate na sio uzitafute. wahenga walisema kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.

Suala la kumuanika mtoto mitandaoni ni tofauti na maongeziya nyumbaniya kumsifu mtoto. kwani nyumbani mpaka unaanza kumsifu mtoto ni kwamba kunaissue imetokea na imeshuhudiwa na hao utakaowasifia. kinachofqnyika hapo ni kuwakumbusha tu na matukio mengine dhidi ya mtoto huyo. na kiukweli hapo utakua unafanya vyema.

After all mtakayoyaongea hapo huisha mwa muda mfupi tu na wala haiwezi kuwa ni record inayoweza kutumiwa vibaya ili kukuumiza kihisia.

Hiyo ni tofauti na kumuanika mitandaoni huku ukisubiria misifa kwa wengine hata wasiomtambua mtoto huyo. Ukimuanika tu mtandaoni unakua attention seeker.

Ok. acha tu tutofautiane kimtazamo. after all you know what you do. mwisho wa siku wote tunatafuta fraa. kuwa huru, fanya yako.

Wish you all the best.
 
Last edited by a moderator:
Nianze kwa kukuuliza wewe mzazi; unapoweka picha ya mtoto wako kila hatua tangu akiwa mchanga hadi anaanza kutembea na kuanza shule, alikuomba au ulipata ruhusa yake?


Ingekuwa wewe umepigwa picha bila idhini yako halafu ukaikuta kwenye mtandao utafurahi?


Najua unampenda mtoto wako na ana haki zake za msingi pamoja na kuheshimiwa faragha yake popote alipo. Haiwezekani chochote anachofanya ukiweke kwenye mtandao.


Naomba kueleza madhara yanayoweza kutokea kwa kuweka picha za mtoto wako au wa mwenzako kwenye mitandao hasa mitandao ya kijamii kama facebook , instagram na mingineyo.


Kwanza fahamu kuwa kampuni karibu zote za mitandao ya kijamii zimesajiliwa Marekani, chache zimesajiliwa Ulaya na Asia, lakini karibu zote zinatumia sheria na sera za mataifa hayo.


Katika mataifa hayo wanasisitiza mtoto asijiunge kwenye mitandao ya kijamii hadi atakapofikisha miaka 13, wengine miaka 15 au 16 .


Kampuni zote za mawasiliano zina utaratibu wa kuhifadhi kila kitu kinachotokea kwenye shughuli zao za kila siku kwenye chombo maalumu cha kuhifadhi taarifa za mtandao (server). Kwa hiyo ukiweka picha za mtoto zinahifadhiwa huko hata kama utazifuta.


Hapo awali, nilisema mtoto anahitaji faragha yake, unaporusha picha za mtoto wako kwenye hii mitandao au mawasiliano yoyote, unaingilia faragha yake na huko mbele anaweza kukushtaki wewe au wengine walioingilia faragha yake.


Mtoto anatakiwa kufunzwa kuanzia mdogo kabisa kuhusu faragha yake, nini cha kusema au kutoa na nini asiseme au asitoe. Hii ni pamoja na kwenye mitandao ya kijamii, simu na huduma nyingine za mawasiliano .


Umeshawahi kuona wanasiasa wanaweka picha za watoto wao au ndugu zao wa karibu kwenye mitandao hasa ya kijamii ? unajua ni kwa nini ?


Kwa sababu kila anachofanya yeye kinamwathiri mtoto wake au watu wake wa karibu kwa ubaya au uzuri. Ni rahisi kuweka rehani faragha za watoto na ndugu zake.


Kama ni mtoto wa kike anaweza kuanza kufuatiliwa na ‘mabazazi’ kwa sababu ya picha tu. Watatafuta anapoishi, shule anayosoma na usishangae siku moja akabakwa.

Kwa hisani ya mwananchi tunapata elimu

Hoja yangu:
Kwanini hii tabia imezuka sana wanandoa siku hiyo hiyo mama anaugulia maumivu badala ya baba kumhangaikia mama na mwanae yeye anafuta kamera iko wapi tena siku hizi mchina amerahisisha anamfotoa mtoto na kupost kwenye wall yake ili iweje? kwamba watu wajue na wewe ni kudume cha mbegu au una kizazi? matokeo yake ndo wazazi mnapotofautiana na marafiki zenu mnawatukana mpaka watoto, kuna wengne sijui mtandao gani yule dada anauza pichu anamtukana mtoto wa mwenzaje eti baboon hivi mnahisi watoto wanajisikiaje? unamharibia mtoto future yake bila kujua, ukifikiri ni fahari kuweka picha ya mwanao sijui facebook, twitter, instagarma na kwingne huko ni ushamba na ujinga, labda siku hizi kwa kuwa imekuwa issue sana kupata mtoto but is not fair

Nawasilisha hoja


Ahsante kwa kutuelimisha
 
Huwa nawaona kama malimbukeni tu leo kuna mwingine kapost anampeleka clinic hivi kuzaa katoto kamoja imekuwakero sasa wazazi wetu walituzaa kuanzia 7 na kuendelea hawakutafuta sifa za kijinga kama hivyo sijui nini kimeingia hapa yani mtu ana katoto kamoja mfano kajala au h mama au zamaradi kutwa utawakuta wanapost watt wao kwenye mitandao utadhani wamezaa kkoo
 
Huwa nawaona kama malimbukeni tu leo kuna mwingine kapost anampeleka clinic hivi kuzaa katoto kamoja imekuwakero sasa wazazi wetu walituzaa kuanzia 7 na kuendelea hawakutafuta sifa za kijinga kama hivyo sijui nini kimeingia hapa yani mtu ana katoto kamoja mfano kajala au h mama au zamaradi kutwa utawakuta wanapost watt wao kwenye mitandao utadhani wamezaa kkoo

Mmmmnnnnhhhh una mtoto weye....????yani hilo tu linakukera????
 
Ni Tanzania pekee ambapo watu ambao ni ignorant wanafikiri wanaweza wakawaambia wengine how to live their life. Watu hawaelewi nini maana yakuwa tolerant kwa wengine as longer hawakubugudhi katika kuvuta pumzi. Watu wako very judgemental na maisha ya wengine wakati maisha yao yanawashinda. Wazungu hawanaga time ya kudiscuss ujinga huu. Watu wako blinded na opinion zao na wanajiona wanachofikiria wao ndo bora kuliko wanachofikiria wengine.
Hoja yako ni nini? nani amekubugudhi katika kuvuta pumzi? nani amekuhukumu? huna hoja kaa kimya soma za wengine, hakuna aliyehukumu mwenzake hapa watu wanaenda kwa hoja kama unaona hakuna facts, zitafute hhuko leta hapa watu wafanye arguement msome Viol na Nyumba kubwa wanavyotoa hoja kulingana na mitaizamo yako sio wewe unatoa povu hapa, et wazungu hawadiscus kwani sisi tunaishi kwa kuiga hao wazungu ebo!
 
Na hakuna aliye hukumu kwenye uu Uzi mwenye hayo mamlaka ni Mungu tu sisi hapa tunatoa mawazo yetu na hayayajalenga kumhukumu mtu only mitazamo tu we ubase kwenye kuhukumu tu why??? Umekimbilia huko hizo ndo emotions zenyewe zinazokufanya uhisi watu wakitoa michango tofauti na wako ufikiri wanahukumu hapo upo kihisia zaidi kuliko reality
Ana stress huyo yeye peke yake ndo kaona kwamba kuna jajimenti mbona wengine wanatoa hoja na maada inasonga mbele kwa kuwa na mitizamo tofauti watu wanaelimika kwa pande zote mbili za maada, hana hoja huyo
 
Hoja yako ni nini? nani amekubugudhi katika kuvuta pumzi? nani amekuhukumu? huna hoja kaa kimya soma za wengine, hakuna aliyehukumu mwenzake hapa watu wanaenda kwa hoja kama unaona hakuna facts, zitafute hhuko leta hapa watu wafanye arguement msome Viol na Nyumba kubwa wanavyotoa hoja kulingana na mitaizamo yako sio wewe unatoa povu hapa, et wazungu hawadiscus kwani sisi tunaishi kwa kuiga hao wazungu ebo!
Sawa akili ndogo. Ndo topic zenu hizi ngoja mi nirudi huko kwenye siasa:becky:
 
te te te...sure you know how to mind your business...and what are you doing in this thread? econometrics...????
Hivi unabishanaje na huyo ambaye hana hoja eti anaiga na anafanya reference kwa wazungu kwa kuwa wameendelea si ujinga huu
 
Sawa akili ndogo. Ndo topic zenu hizi ngoja mi nirudi huko kwenye siasa:becky:
Mmmh! hili tu dogo umeshindwa kupambanua unataka kila mtu afanye arguement kama unavyotaka huko siasani utarudi sasa hivi, uwasalimie huko
 
Mmmh! hili tu dogo umeshindwa kupambanua unataka kila mtu afanye arguement kama unavyotaka huko siasani utarudi sasa hivi, uwasalimie huko
Wewe umejoin humu ndani 2013 una post kwenye mahusiano na mapenzi zaidi ya 1600 ambazo ni 98 percent ya post zako zote. Mimi nipo Jamii Forum toka 2008. Ukijumlisha post zangu zote hazifiki 300. Sipotezi muda kijinga jinga f.a.l.a wewe. Unakaa hapa utadhani unapata pesa. Sishindi hapa jamii forums. Huyo dada anayekusupport ana hasira na mimi nilimpa punch za maana last time kwenye topic ya eti waliojiajiri wamefulia. Sasa mtu mwenye thinking ya aina hiyo nitaongea naye nini. Na wewe ni wale wale upo upo tu.:becky::becky:
 
Na nyieeee kila kitu sheeda ....Basi na hao ambao mitandao imeanzia kwao wasingekuwa wanaweka ...wangewangojea wanao wakiwa wakubwa ndio wawaombe tusingeona picha za mtoto wa mzungu hata mmoja mitandaoni...


Kwanza ujue mitandao ni kumbukumbu nzuri ya kutunza soft copy...Hata Nyumba ikiungua Albums zikiungua au ukipoteza picha au flash ikiliwa na virus ukitafuta pics ktk mtandao utaipata tuu...

Waafrica tumezidi kwa kuzusha mambo....Ulimwengu wa Digital huu unatakiwa kubadilika kadri mazingira yanavyobadilika...Na changamoto zake unatakiwa kujifunza kukabiliana nazo na kubadilika nazo....





Duh.
Kweli Mkuu siku hizi mtu mko nyumba moja badala ya kumsalimia hapo unakwenda Facebook unampa salam
Mtu na Mkewe badala ya kusifiana nyumbani wanakwenda Facebook, umependeza.

Hii ni shidaaa kweli. hasa miaka hii
 
Hahahahahaaa unaenda kumsifia facebook wakati umemuacha ndani, kumbe hata akipika chakula kitamu unaenda kumsifia facebook kwa faida ya nani? na ukichapiwa wa kumlaumu nani wakti umemsifia mwenyewe, na wakikorofishana hapo sisemi

Wakiudhiana sasa post zao na status zao huko mitandaoni sasa...
 
Pana aliyekuwa mchawi na mmoja wa chama cha siri huko nchini kenya alieza jinsi walivyokuwa wakitumia picha zinazo postiwa mitandaoni kutimiza adhma zao.

Pia hata waombaji hutumia picha za watu katika maombi halikadhalika pamoja na hataari zote tajwa hilo waganga au wachawi kuzitumia picha vibaya inawezekana.
 
Back
Top Bottom