Mkuu Barbarosa unajua asili ya jina lako? Tuache hilo kwa sasa, ni kweli Edward akiondoka CCM atakuwa adui wa dola isipokuwa jua kitu kimoja dola yenyewe haipo pamoja katika hili, ni dola iliyogawanyika na mgawanyiko upo kwa ndani, ni ngumu kujua nani wa kumuamini.
Kuhusu foreigh powers (Uchina, Marekani na Ulaya) hawa wana maslahi yao na bado hayatishiwi kwa Lowasa na UKAWA kuingia madaraki. These powers would only act against the move kama maslahi yao yatatishiwa. Hawaipendi CCM kwa sababu ni CCM wanaipenda kwa sababu inalinda maslahi yao. Hata hivyo mahusioano yao si mazuri kama uanavyotaka kutuaminisha kwa mfano walisimamisha misaada kwa budget hivi karibuni CCM kamasi zikawatoka.
Hili la dola kukaa kimya ndio itakuwa inapiga hesabu zake, je zitakuwa na tija - time will tell ila siasa lazima hesabu kama dola inavyopiga hesabu ana the other side inapiga hesabu vivyo hivyo. Siasa ni kama mchezo wa chess kuna moves na counter moves mkuu.
Acha kuongopa Hapa!
Misri sasa hivi imerudi kule kule ilikotoka, si ajabu kubaya zaidi! Jeshi lile lile la Mubaraka ndiyo limechukuwa nchi tena, hakuna Demokrasia yoyote ile kwanza Arab Spring revolution yote imefeli vibaya mno! Mpaka leo hii hakuna Raisi wa kuchaguliwa na Jeshi ndiyo linaaamua kila kitu ambalo halichaguliwa na mtu yoyote yule!
Halafu isitoshe unalinganisha vitu visivyolingana huwezi kulinganisha Urusi au sijui Misri na TanZania, hizo nchi zote zilikuwa zinaongozwa kidekta na kulikuwa hakuna uhuru wowote ule si wa kuabudu, wa habari au hata kupiga kura sasa TanZania hatuko hivyo hapa kwetu kuna kila aina ya uhuru leo hii Slaa au sijui Mbowe anasimama jukwaani na kumwita Raisi wa JMT mwizi na fisadi na anashuka jukwaani anapanda gari lake anarudi nyumbani kwake au hata kwenda baa kunywa bia na hakuna anayemuhoji kitu na analalal usingizi anasex na Mke wake bila bugdha kama watz wengine tu, magazeti yanaandika yanavyotaka kuhusu CCM na Raisi wa JMT mpaka wanaandika kwamba raisi wa JMT kauza nchi kwa Wachina kwa sababu mtoto wake alishikwa na madawa ya kulevya Uchina na hakuna kitu kinatokea kwa hawa wanaoandika hivi, Uchaguzi unafanyika Upinzani wakishindwa wanakwenbda Mahakamani rejea Igunga na wanashinda mgombea wa CCM anatenguliwa na Mahakama, Upinzani wanafanya Mikutano bila ya shida na humo wanatukana na kushutumu Serikali rejea Mwanza na saa nyingine hata ushahidi hawana lkn wanalala vizuri tu bila ya shida kwanza wengine hata walinzi hawana sasa kuna Demokrasia zaidi ya hiyo?
Kumbuka Raisi wa JMT ana Absolute Power akiamua hayo yote niliyoyataja anaweza kuyakataza, anaweza kuamua kukifuta CHADEMA kesho na kumweka Slaa ndani kwa kumwita tu (raisi) fisadi na sheria hiyo ipo lkn halifanyiki...
Mkuu Barbarossa, nimeshindwa kupita kimya hapa, naomba maana ID yako,
Upande mmoja unasema rais ana absolute power, nakubaliana na wewe 100%, upande wa pili unasema kuna demokrasia, hapo nachanganyikiwa na logic yako! Haiwezekani kwenye mfumo wa kidemokrasia raisi akawa na absolute power, huu ni mfumo wa kidikteta sema CCM inajua namna ya kuutumia ionekane kama kuna demokrasia, hatutaki demokrasia ya namna hiyo ambapo raisi akiamua anaweza kufungia chombo cha habari, anaweza kukuweka kizuizini bila bila kupitia the due process of law, tunapambana na CCM kwa vile ndiye mlinzi wa mfumo huu ambao hatuwezi kwenda popote bila kuuvunja kwanza.
Kila nchi ina mazingira yake, ni kweli Misri, USSR ya 1917 na Tanzania zina mazingira tofauti ila nakubaliana na mkuu Lushenisti kuwa mabadiliko si kitu cha haraka haraka na kinachokuja kwa amani. Kwenye development studies kuna theory ya maendeleo inaitwa "Unit and struggle of the opposite" kama sikosei. Kwenye hili la the Arab spring kufeli I beg to differ,
Let us live the Arab spring discussion for anather day
Kama nia nikushika dola kwa kutumia watu wahalifu,! Mi sidhani kama watanzania wanaweza kukubaliana na wazo Hilo. Namimi sidhani kama tumefika huko
Lowassa angekuwa na connection kali ndani ya chama asingekatwa...

Nilikuwa najaribu kumjibu mtu aliyetaka kulinganisha Mapinduzi ya Urusi na Misri ndiyo nikasema hizo nchi mbili huwezi kulinganisha na TanZania kwani kama ni demokrasia angalau sisi tumewazidi sana (misri ya kabla ya Arab spring na Urusi ya Karne ya 20) lkn SIJASEMA kwamba TanZania ni nchi ya kidemokrasia kwa 100% na kwanza sidhani kama kuna nchi kama hiyo!
Blac Kid katika jamvi la weledi hoja hujibiwa kwa hoja, hoja dhaifu huangushwa na hoja yenye nguvu Barbarosa amejenga hoja yake, ameipanga, kama wewe unaamini na kujua kuwa hoja yake ni dhaifu basi jenga hoja yenye nguvu na si kufanya haya uliyoyafanya, umetukana halafu hujasema kitu. Eleza unachokifahamu wewe kuhusu demokrasia, eleza kwa nini unadhani hakuna demokrasia na demokrasia gani ungeitaka wewe maana kuna demokrasia za aina nyingi. Pengine demokrasia anayoizungumzia Barbarosa si ile unayoitaka wewe, mi naona hicho ndio kingekuwa kipimo bora kabisa cha kupima akili za mwanajamvi mwenzako kuliko kuhamaki na kujionesha namna ulivyo na uwezo wako wa kujenga na kuhimili hoja za watu wengine
Siasa ya tanzania imekosa mashiko. Hivi ni kweli ukawa wameamua kumpokea lowassa out of nowhere. Pumba tupu.
Lowasa anataka Urais kupambana na Umasikini kama umeshamsikia hiyo ndo ajenda yake kubwa, kwakuwa CCM wanapenda umasikini na ujinga ili waendelee kutawala, hiyo imemfanya Lowasa atafute watu wengine wenye malengo ya kuundoa umasikini na ujinga wa watanzania na si wengine ni UKAWA, siku Lowasa anajiunga UKAWA itakuwa ndo mwanzo wa Zama nyingine katika taifa letu, bila CCM kuwa Chama Tawala. Lowasa akiwa Rais atapigana kufa na kupota ku prove kuwa yaliynenwa juu yake si kweli, na watanzania tutanufaika sana na utawala wake.
Haya nitajie huko kwenye Demokrasia unakokuongelea halafu pia tukueweke kwenye lens kama tulivyoweka demokrasia ya TanZania kwenye lens pia!
apana ccm iondoke tu yaani neno ccm jamani liondoke aa
Kama nia nikushika dola kwa kutumia watu wahalifu,! Mi sidhani kama watanzania wanaweza kukubaliana na wazo Hilo. Namimi sidhani kama tumefika huko
Mkuu umeokwa povu sana, ushauri wa bure tu dont take politics serious utakufa na kihoro wenzio wanacheka pembeniLowasa yupi unyemzungumzia hapa? Je ni yule yule Lowasa ambaye yeye mwenyewe amesema ametumia maisha yake yote CCM, yule yule aliyesema yeye hatoki CCM na asiyempenda ahame chama? Lowasa gani mnayemzungumzia hapa? Ni yule yule mliyemtuhumu humu humu jamvini kamlisha sumu Mwakyembe, ni yule yule mliyeleta data zake humu jamvini na kumuita Richard of Monduli? Au kuna Lowasa mwingine ambaye yeye anakerwa sana na umasikini wa watanzania kiasi anataka kujitolea maisha yake kuwaokoa watanzania? Yuleyule au kuna mwingine ndugu zangu?
Nadhani ni mwandishi wa kimarekani Cristoper Dikens kama sijakosea jina, wakati Marekani ikijiandaa kuishambulia Iraq ili kumuondoa Sadam madarakani mandishi huyu aliandika makala "The perils of victory" Kwa Kiswahili unaweza kusema hatari za ushindi. Kwenye makala hii alitahadharisha mambo ambayo yangetokea baada ya ushindi wa kijeshi wa marekani dhidi ya Sadam. Alitabiri karibu kila kilichotokea baadaye kuanzia the cilivil war hadi kugeuka kwa Iraq kuwa a save heaven kwa magaidi.
Si lengo langu kuijadili makala ile, nimechukua kichwa cha makala ile vile kinawiana sana na yanayoelekea kutokea kwenye siasa za Tanzania kwa sasa. Kuna fununu kwamba kada wa CCM Mh Edward Lowassa anaelekea ku hama chama chake na kujiunga na chama kikuu cha upinzani (CDM) na labda akapitishwa kugombea uraisi kupitia UKAWA.
Uchambuzi wangu finyu unaniambia uwezekano wa Lowassa kushinda uraisi kupitia UKAWA ni mkubwa. Kwa nini! Wengi wanafikiria juu wa watu walioko nyuma yake lakini sidhani kama hilo ndilo lenye umuhimi wa kwanza. Kuna mambo kadhaa yanayompa Lowassa na UKAWA nafasi nzuri ya kuiangusha CCM.
CONNECTIONS ZA LOWASSA NDANI YA SYSTEM NA CHAMA Kushinda uchaguzi ni zaidi ya kuungwa mkono na watu, ni zaidi ya kupigiwa kura za kutosha. Uchaguzi ni kama vita na unapojipenyeza kwenye ngome ya adui yako na kujua anachopanga kufanya hakika una nafasi nzuri zaidi ya kushinda. Lowassa ana watu ndani ya system na CCM. Kuna watakaotoka naye iwapo atatoka (wana CCM) na kuna watakaobaki na kuendelea kumtumikia kichini chini wakiwa CCM, kuihujumu CCM toka ndani. Watu wake ndani ya system watasaidia sana kukabili juhudi wa system kuuhujumu upinzani. CCM na system iliyoko nyuma yake italazimika kupigana vita mbili kwa wakati mmoja, vita na upinzani wa wan je upande mmoja na upande wa pili itakuwa vita dhidi ya upinzani wa ndani. War on two fronts is the last thing strategist would wish for.
RASILIMALI FEDHA Ni wazi kuwa nyuma ya Lowassa kuna massive financial resources kulinganisha na kile ambacho CDM/UKAWA inaweza ku mobilize bila Lowasa. Rasilimali fedha ni muhimu sana kushinda uchaguzi, huu ni mchakato ghali sana ambapo uwezo wa kifedha una nafasi yake katika kuleta matokeo.
ORGANISATION Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni, 4u movement ilikuwa the best organised campaign within CCM, ilikuwa movement iliyoazima mbinu nyingi za kibiashara kufanya siasa, kosa kubwa lilikuwa ni kutokuweka msisitizo wa kutosha kwenye siasa yenyewe, siku nikiwa na nafasi nitalieleza hili kwa kina. Sasa organisation hii ikijumlishwa naya UKAWA itakuwa ni kikosi mahiri kabisa na tutaona mambo mapya kwenye kampeni za kisiasa. Sioni namna gani CCM inaweza kutengeneza timu ya kushindana na hii hapa.
WATU Hili wa watu nimelipa kipaumbele cha mwisho, Yes Lowasa ana watu wa kutosha (watu wa kawaida) japo si wengi kama anavyotaka kutuaminisha, jambo kubwa hapa watu hawa wengi wao si undecided voter bali ni wapiga kura wa CCM, watu wa Lowasa wana double effect iwapo wataipigia kura UKAWA, kwanza watoongeza kura za UKAWA na pili watapunguza kura ambazo kwa kawaida CCM inakuwaga imeshajihakikishia.
JE LOWASA NA CHADEMA/UKAWA WANA AGENDA MOJA?
Lowasa anautaka uraisi kwa gharama yeyote na UKAWA wanataka kuchukua dola. Hapa they both have something in common ila ukienda mbele zaidi utagundua wanaachana. Siamini kama Lowasa anataka madaraki ili kuleta mabadiliko chanya kwa Tanzania na Watanzania, kama ni hivyo basi hilo ni la mwisho katika vipaumbele vyake. Namuona kama mtu anayeendeshwa zaidi na ego yake na maslahi yake binafsi yale ya marafiki zake. Upande wa pili kuna element ndani ya UKAWA/CDM strong enough elements zilizodhamiria kuleta mabadiliko chanya kwa Tanzania/watanzani. Ni wazi kuwa pande hizi mbili kila moja inamjua mwenzia fika, ndoa hii iwapo itafungwa haiongozwi na mapenzi bali maslahi fulani fulani ya pande hizi mbili, mengine yenye manufaa kwa Tanzania na mengine yasiyo na manufaa kwa Tanzania. Of course siasa ni mchezo wa mahesabu makali na average brains zinaweza zisielewe most of the policial moves, siasa haziongozwi na hisia za mapenzi au chuki, zinaongozwa na maslahi ya mudu mrefu.
NINI HATARI YA USHINDI WA UKAWA? CDM/UKAWA wanaamini wataweza kudhibiti Lowassa baada ya kumtumia kuchuka dola, hili si jambo rahisi sana kwa kaliba yake Lowasa ninayemfahamu. Uwezo wake wa kujua bei za watu na staili yake ya kufanya siasa isiyo na jambo la kuonea aibu kufanya iwe baya kiasi gani inatoa picha tofauti. Naona hatari ya Lowasa kuununua uongozi wa juu wa CDM/UKAWA na akaishia yeye kuwaendesha badala ya wao kumuendesha. Hili likitokea tutaona muendelezo wa uozo ule ule tuliouona ndani ya serekali ya CCM na watu watajiuliza ilikuwa ni kwa manufaa gani waliiondoa CCM madarakani? Mbona majizi yale yale yaliyotamalaki chini ya utawala wa CCM bado yanaendelea kubaka rasilimali zetu chini ya utawala wa UKAWA? Huo utakuwa mwisho wa kisiasa wa baadhi ya vyama ndani ya UKAWA, nadhani muathirika namba moja atakuwa CHADEMA.
Hatari hii ikiwa kweli tutasema not all is lost: kwanza itakuwa ngumu sana kupitisha mambo bungeni kwa msimamo wa chama, for sure no matter what happens UKAWA ikishinda hatutaona chama kimoja kikiwa na udhibiti wa bunge kama ule iliokuwa nao CCM. Hii ni habari njema sana kwa wapenda mabadiliko. Pili: Baada ya kuiondo CCM madarakani, itakuwa kazi nyepesi sana kuvingo vyama vitakavyofuatia, CCM ni chama dola, chama kilichotuletea uhuru, chama chenye mizizi iliyojikita chini sana, hao wengine watakuwa wepesi sana kuwaondoa na tutaendelea kubadilisha vyama hadi tupate watawala sahihi. Hakutakuwa na chama kimoja kinachohodhi madaraka kama ilivyo CCM sasa!
HITIMISHO Kama hitimisho, iwapo Lowassa atahamia UKAWA kuna uwezekano mkubwa wa kuongoa CCM madarakani japo kuna hatari kubwa ya uozo wa CCM kujirudia chini ya utawala huo mpya. Hata hivyo bado naona it is a risk worth taking! Kuiondoa CCM madarakani itakuwa hatua ya kwanza, tutakuwa tumeondoa kikwazo kikubwa kabisa cha kwanza hivyo vingine tutaendele navyo hatu kwa hatua.
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ya-mafanikio-chadema-ukawa-and-lowassa-5.htmlShida iko hapa Watu wa CHADEMA/Lowasa siku zote wanawaza yaliyoikuta KANU ndiyo yataikuta CCM kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa maana tuna mazingira tofauti (Kenya na TanZania)!
Hivyo basi kitu pekee ambacho Bw.Lowasa na watu wake wanaweza kufanya ni kutumia fedha nyingi walizo nazo au kwa kifupi kununua washabiki ili wawachague na hapa ndipo tatizo litakapokuja kwa maana ni watu ambao hawasukumwi na sababu za Kiitikadi ideology, imani ya kidini, au kiethnic bali wanasukumwa tu kupewa pesa sasa mtu wa hivi siyo hatari sana na anaweza kukugeuka wakati wowote ule na hapo ndipo Dola ya CCM itakapocheza kwani mfumo wa fedha TanZania uko chini ya Serikali na unaweza kudhibitiwa wakati wowote!
Ngoja nikuulize swali dogo tu kwa mfano Serikali wakisema kesho Bw.Lowasa ana kesi ya kujibu kuhusu Richmond hivyo anatakiwa afike mahakamni Bw.Lowasa atafanya nini? Unafikiri kuna Mtz kutoka Karagwe au Tunduru atakayeingia barabarani kupinga kushitakiwa kwa Lowasa na awe tayari kuumia na kufa hata baada ya kuona wenzake wachache walioumizwa na Polisi?
Kuhusu Marekani, Uchina na Ulaya nilichomaanisha ni kwamba TanZania ni kipenzi cha Wazungu na mpaka sasa hivi hivyo kama Serikali ikimkamata Bw.Lowasa na kumfungulia mashitaka Wazungu au Wachina hawawezi kuingilia swala la escrow Wazungu waligoma kwa sababu fedha zao ndio zilizoibwa na walizitaka lkn siyo kwa sababu ya fedha za Mtz!
Hivyo kwa kifupi Bw.Lowasa hana uwezo wa kuwa Raisi wa JMT nje ya CCM na kama anaamini hivyo atakuwa siyo intelligent man kama mnavyomdhania kwanza hata watu hana kwa maana kama angekuwa nao tungeona maandamano nchi nzima pale tu alipokatwa jina lkn mimi nilikuwepo mitaani hata hao waliokuwa wanamshabika walivyosikia amekatwa wote wakahamia kwa Magufuli na kuendelea kunywa bia!
Sasa hii ni tofauti na Kenya, Raila baada ya Kibaki kutangazwa mshindi tayari Wajaluo wote wakaingia barabarani, sasa ni kwa nini?
Ni sababu ya ethnicity ambayo Bw.Lowasa hana zaidi ya fedha ambazo hata nyingi siyo zake na usifikiri CCM hawajui chanzo cha hizo fedha wanajua na swali ni Je, hawa wanaotoa hizo fedha wako tayari kugombana na Serikali na mfuomo wake wote?
Shida iko hapa Watu wa CHADEMA/Lowasa siku zote wanawaza yaliyoikuta KANU ndiyo yataikuta CCM kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa maana tuna mazingira tofauti (Kenya na TanZania)!