Hatari ya mafanikio - CHADEMA/UKAWA & Lowassa


Blac Kid katika jamvi la weledi hoja hujibiwa kwa hoja, hoja dhaifu huangushwa na hoja yenye nguvu Barbarosa amejenga hoja yake, ameipanga, kama wewe unaamini na kujua kuwa hoja yake ni dhaifu basi jenga hoja yenye nguvu na si kufanya haya uliyoyafanya, umetukana halafu hujasema kitu. Eleza unachokifahamu wewe kuhusu demokrasia, eleza kwa nini unadhani hakuna demokrasia na demokrasia gani ungeitaka wewe maana kuna demokrasia za aina nyingi. Pengine demokrasia anayoizungumzia Barbarosa si ile unayoitaka wewe, mi naona hicho ndio kingekuwa kipimo bora kabisa cha kupima akili za mwanajamvi mwenzako kuliko kuhamaki na kujionesha namna ulivyo na uwezo wako wa kujenga na kuhimili hoja za watu wengine
 
Mpaka Leo hakuna aliyechukua form ya Uraisi Chadema ikiwa ni Siku ya mwisho
 

Lowasa yupi unyemzungumzia hapa? Je ni yule yule Lowasa ambaye yeye mwenyewe amesema ametumia maisha yake yote CCM, yule yule aliyesema yeye hatoki CCM na asiyempenda ahame chama? Lowasa gani mnayemzungumzia hapa? Ni yule yule mliyemtuhumu humu humu jamvini kamlisha sumu Mwakyembe, ni yule yule mliyeleta data zake humu jamvini na kumuita Richard of Monduli? Au kuna Lowasa mwingine ambaye yeye anakerwa sana na umasikini wa watanzania kiasi anataka kujitolea maisha yake kuwaokoa watanzania? Yuleyule au kuna mwingine ndugu zangu?
 

Haya nitajie huko kwenye Demokrasia unakokuongelea halafu pia tukueweke kwenye lens kama tulivyoweka demokrasia ya TanZania kwenye lens pia!
 
Haya Libya, Misri, Iraq, Yemen walikuwa na mawazo kama yako lakini sasa wamejifunza wanajuta. Kwa hiyo unataka kutuambia nasisi watanzania tujaribu mawazo hayo ili tuje pata tabu ya maisha kwetu na familia zetu? ?

Nchi zote ulizozitaja walitumia bunduki,sisi tutatumia sanduku la kura.Kenya,Nigeria,Malawi n.k walivipiga chini vyama tawala mbona hawakujuta?Acha ujinga.
 
Wacha kudanganya watu na kuwatia woga. Siku hizi hakuna ubabe wa hovyo kiasi hicho na ndio maana wengi waliofanya hivyo wametoka madarakani na kustaafia The Hague kumalizia uzee wao.
Fikra za kizamani achana nazo


Nitajie huyo aliyetoka mfumo wa kama CCM halafu akaenda The Hague! Hivi hata unajua The Hague ni nini na kwanini hata ilianzishwa? Unafikiri kila nchi inapelekwa the Hague basi ingekuwa hivyo kungejaa huko Tha Hague!
Mbona Kagame anapiga risasi live wapinzani kila siku na hayuko The Hague? Na anakula bata na wazungu kila siku tena ni hivi majuzi wazungu wamemteua kuwa Kiongozi mwenye Utawala Bora Duniani
 
 
Ila nilichojifunza hapa faida ni nyingi kuliko hasara


Lowassa anafaida nyingi ndani ya ukawa kuliko hasara lazima tuwe risk takers ili taifa hili liweze badilika
 

Mkuu Barbarosa unajua asili ya jina lako? Tuache hilo kwa sasa, ni kweli Edward akiondoka CCM atakuwa adui wa dola isipokuwa jua kitu kimoja dola yenyewe haipo pamoja katika hili, ni dola iliyogawanyika na mgawanyiko upo kwa ndani, ni ngumu kujua nani wa kumuamini.

Kuhusu foreigh powers (Uchina, Marekani na Ulaya) hawa wana maslahi yao na bado hayatishiwi kwa Lowasa na UKAWA kuingia madaraki. These powers would only act against the move kama maslahi yao yatatishiwa. Hawaipendi CCM kwa sababu ni CCM wanaipenda kwa sababu inalinda maslahi yao. Hata hivyo mahusioano yao si mazuri kama uanavyotaka kutuaminisha kwa mfano walisimamisha misaada kwa budget hivi karibuni CCM kamasi zikawatoka.

Hili la dola kukaa kimya ndio itakuwa inapiga hesabu zake, je zitakuwa na tija - time will tell ila siasa lazima hesabu kama dola inavyopiga hesabu ana the other side inapiga hesabu vivyo hivyo. Siasa ni kama mchezo wa chess kuna moves na counter moves mkuu.
 

Umeandika kwa kujiamini sana Mr Hero, siasa is very dynamic, haijanyooka kihivyo
 
Kama nia nikushika dola kwa kutumia watu wahalifu,! Mi sidhani kama watanzania wanaweza kukubaliana na wazo Hilo. Namimi sidhani kama tumefika huko
 
Mwandishi wa story hii amesahau kuwa, one of the best move ambayo itafikiwa na serikali ya ukawa ni kuunda chama kipya cha siasa kwa umoja wao. Kitu ambacho kingekuwa ni kigumu ktk utawala huu wa CCM
 
Itakuwa hakuna kilichofanyika km maslahi yk binafsi atakuwa hana nia ya watanzania bali yy binafsi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…