Hatari ya barakoa used kwa Watoto

Munnahumuu

Member
Feb 6, 2018
34
17
Habarini za usiku huu wakulungwa, ni mwenyeji JF tangu 2016 lakini huu ndo uzi wangu wa kwanza.

Kama somo tajwa la hapo juu, naiona hatari kwa Barakoa zilizotumika na zinavyotupwa hovyo na kuzagaa mitaani. Kwa watoto hasa wanafunzi darasa la kwanza hadi la tatu wale wa day na wengineo wa rika hizo kitaani.

Nafikiri hawa hawaelewi chochote na nimeshuhudia watoto siyo mara moja wanaziokota na kuzivaa wawapo kwenye michezo ya kitoto ama wanapokuwa wanatoka mashuleni. Nashauri wazazi tuwe aware juu ya hili.

Serikali pia kupitia kitengo cha Dada Ummy na bwana Waitara,kipindi hiki cha tension ya mifuko ya plastic naomba jumlisheni na hili jamani.

Ahsanteni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom