Kauli ya makamu mkuu huyo iliungwa mkono na wakuu hao wa wilaya ambao walitaka uongozi wa Udom usiwarudishe kirahisi wanafunzi hao ili wajifunze kwanza kuwa walichofanya hakikuwa kizuri."Tena mkianza kuwarudisha rudisheni wana-CCM, hao wa Chadema achana nao maana ndio wanaoanzisha vurugu na uvunjifu wa amani hawana shukrani hao hata siku moja na wala hawajui kutoa fadhila zaidi ya kulalamika kila kitu,'' alisikika akisema mmoja wa wakuu hao wa wilaya.Hivi hawa wakuu wa Wilaya zetu zimo kweli jamani? hiyo ni pointi yakuongea na wenzio wakusikileze? inamaanisha chuo ni cha waccm tu na sio vyama vingine? Tusiingize mambo yasiasa, kwenye haki. Huyo atakuwa kilaza na inabidi achunguzwe zaidi. refer MWANANCHI 27.6.2011