Wanafunzi UDOM wadaiwa kutengeneza mabomu-Siasa na elimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi UDOM wadaiwa kutengeneza mabomu-Siasa na elimu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JOHN MADIBA, Jun 27, 2011.

 1. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  ZINAPOCHANGANYA CHUKI+BIFU ZA KISIASA UONGO KAMA HUU HAUKOSEKANI
  MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idrisa Kikula amesema hawezi kushawishika kwa lolote katika kuwarudisha chuoni hapo wanafunzi kwa kuwa anazo taarifa kuwa baadhi walitengeneza mabomu ya kupambana na polisi.

  Profesa Kikula alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wakuu wa wilaya wa wilaya zote nchini ambao walitembelea chuo hicho kwa ajili ya kujifunza.

  Alisema kuwa hakuna kitu kitakachomshawishi kuwarudisha wanafunzi kwa kuwa anasimamia taaluma sio siasa kama ambavyo baadhi ya wabunge wanataka iwe.

  "Siwarudishi wanafunzi kwa shinikizo la kisiasa maana siku ya mgomo mimi niliweka rehani maisha yangu baada ya kuambiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa wanafunzi wasigome nikawafuata saa sita usiku nikawaambia Serikali inashughulikia madai yenu, lakini baadaye saa tisa usiku nikasikia wameandamana,'' alisema Profesa Kikula na kuongeza:

  "Hata hivyo, uchunguzi wetu ulibaini kuwa baadhi yao siku moja kabla walikwenda mjini kununua petroli ambayo walitaka kutengeneza mabomu ya kupambana na polisi.

  "Sasa, kwa hali hiyo mnadhani ingekuwaje lazima tufanye uchunguzi wa kina kabla ya kuwaruidisha.''

  Kauli ya makamu mkuu huyo iliungwa mkono na wakuu hao wa wilaya ambao walitaka uongozi wa Udom usiwarudishe kirahisi wanafunzi hao ili wajifunze kwanza kuwa walichofanya hakikuwa kizuri.

  "Tena mkianza kuwarudisha rudisheni wana-CCM, hao wa Chadema achana nao maana ndio wanaoanzisha vurugu na uvunjifu wa amani hawana shukrani hao hata siku moja na wala hawajui kutoa fadhila zaidi ya kulalamika kila kitu,'' alisikika akisema mmoja wa wakuu hao wa wilaya.

  Mwanzoni mwa mwezi, uongozi wa chuo hicho uliwafukuza wanafunzi zaidi ya 9,000 wa Chuo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano baada ya kufanya maandamano yaliyomtaka baadhi ya mawaziri wajiuzulu.

  Waliwataja kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani , Shamsi Vuai Nahodha wajiuzulu kwa madai ya kuwadanganya.

  Wanachuo hao walikuwa wakishinikiza kupelekwa katika mazoezi ya vitendo pamoja na kununuliwa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na kompyuta.

  Wabunge wa Bunge la Muungano ambao wanaendelea na mkutano wao mjini Dodoma wamekuwa wakipiga kelele mara kwa mara wakitaka wanafunzi hao warudishwe chuoni hapo kwa madai kuwa walichokuwa wakidai ilikuwa ni haki yao.

  Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alisema Serikali ilikosea kutowapeleka katika mazoezi ya vitendo wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwa hiyo ni haki yao ya msingi.

  Mukama aliwaomba radhi wanafunzi hao kwa upungufu huo na kutaka waipe Serikali mwaka mmoja ili ibadili mfumo unatumika kwa sasa.
  ..................KUNA UKWELI HAPA AU BIFU ZA CCM NA CDM.............
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145

  Hapo penye red pananitisha sana kwa kuwa hizo ni kauli za chuki na ubaguzi,siamini kama kweli kuna kiongozi mwenye akili timamu anaweza kutamka matamshi kama haya!!
   
 3. JOHN MADIBA

  JOHN MADIBA JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 30, 2011
  Messages: 251
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  "Tena mkianza kuwarudisha rudisheni wana-CCM, hao wa Chadema achana nao maana ndio wanaoanzisha vurugu na uvunjifu wa amani hawana shukrani hao hata siku moja na wala hawajui kutoa fadhila zaidi ya kulalamika kila kitu,'' alisikika akisema mmoja wa wakuu hao wa wilaya.
  KWA KAULI HIZI ZA VIONGOZI WASERIKALI TUTAFIKA KWELI NGUGU ZANGU
   
 4. tozi

  tozi Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tunaomba jina la mkuu wa wilaya aliyetoa tamko tukamnyonye mavi,warudishwe ccm akimaanisha kuwa watarudi kwa kuonesha kadi au?huyo najua atakuwa Nnape ndiye mkuu wa wilaya mwenye akili matope kuliko wote,na wakifanya vile wajiandae kufunga chuo kizima maana hilo lazima tuliashughulikie hatutajali kufukuzwa,na wajue chadema hapa ndo wenye chuo kwa maana kuwa waliandamana zaidi ya asilimia 80% sasa hao wote watawafukuza?
   
 5. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  Hii kauli ni kiboko, duh.....! Hivi hawa wakuu wa wilaya na mkoa ndio wanaotoa hela za kuwasomesha wanafunzi tanzania au ni kufilisika kimawazo. Hii kauli ikemewe kwa vitendo inadhalilisha haki ya watanzania na ni jibu tosha kuwa tanzania ipo mikononi mwa mabeberu weusi. Sasa tujiulize ni amani ipi wanaongelea hawa manjemba. Hapa ninapata shida kuwaelewa kama hawa wakuu wa wilaya na mkoa ni wa ccm au ni wawatanzania wote. Hii ni kuidhalilisha taaluma ya Tanzania na ujumbe wa wanafunzi umefika sasa ufanyiwe kazi. Hivi wanafunzi wote wakiamua kugoma tanzania nzima watarudisha wanafunzi wa ccm tu au watafanya nini?
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wakuu wa wilaya na ma-RC ni watu hatari katika mfumo wa uongozi wa nchi hii. Ila wajue kuwa hizo nafasi ziko ICU...anytime watakuwa mitaaani wakitafuta vibarua. Hata wajikombe vipi kwa CCM haitasaidia.
   
 7. i

  ichawinga Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii ni kweli kabisa unajua bifu la CHUKUA CHAKO MAPEMA(C.C.M)na hawa ndg zet wapambanaji linapelekea hata mambo muhimu katika jamii kuingiliwa, sasa jiulize elimu ya vitendo wanavyodai udom na chakudema vinaingiliana vp ndg yangu hawa jamaa we ngoja mwisho wao umefika!
   
 8. i

  ichawinga Member

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 9. i

  ichawinga Member

  #9
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 10. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Siko kutetea maslahi ya chama chochote mimi daima kwangu Tanzania mbele,na si vinginevyo,ila kauli ya Mkuu huyo wa Wilaya ni moja ya vitu ambavyo najiuliza sana mpaka mtawala huyu anachaguliwa kuwa Mkuu wa wilaya nani alifanya uthibitisho juu ya uadilifu, uungwana, ustaarabu, usikivu, uvumilivu, unyeyekevu,staha,elimu,busara, ukali na upole wa tija na hata ucheshi juu ya umma [kwa ujumla vetting].

  Ni nini kiko ndani ya huyu mtwala mpaka anatamka maneno hayo kuwa hao wa chama kingine hawana shukrani.Yani hawa ndio ninaosema bado wanaamini CCM ndio Nchi na yoyote yule anayepinga CCM ni msaliti kwa nchi.Jamani kwangu mimi natambua mchango wa CCM kwa TAIFA hili lakini hainipi uhalali wa kuamini bila CCM hakuna TANZANIA.

  Kwanini wanataka Kizazi cha Dotcom Generation [DG] hao wanachuo waamini kuwa bila CCM vijana hao hawana maisha.Thubutu hiyo ni dhambi mbaya na kamwe viongozi wa haiba hiyo ya Mkuu huyo wa wilaya wasipewe nafasi kamwe kupandikiza chuki.Hao ndio wanasababisha chuki kubwa dhidi ya CCM.

  Huyu mkuu wa Wilaya hastahiki kuwepo hapo,kamwe hicho kiti ni uchochezi kwake na usaliti wa kwa huyo anayemwakilisha yaani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya raia wake [yani wanafunzi] .Matamshi yake ni sawa kuwa yametamkwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano japo hahusiki yeye kama yeye,lakini anahusika kwa watu wake kutumia vibaya kofia yake.Japo hata kwa hakika Rais wa Nchi na nguvu yake yote ya ukuu wa dola maneno hayo hayawezi yakatoka mdomoni mwake,, pamoja na kuwa ni kada mahususi wa chama cha mapinduzi aliyebobea bado nina hakika kwa kujua staha asingeweza kulopoka hayo haliyofanya mwakilishi wake.

  Hayo madudu ndio kilio cha wananchi,pata picha wangekuwa ni watu wawili tu ama watano ambao wako ndani ya himaya yake ya ukuu wa wilaya na hakika,angewaamlisha wakuu wa vyombo vya dola kutenda yale ambayo sasa hivi yangekuwa mengine kwa wahusika hao.

  Kamzalilisha Rais,busara zilizofikiwa kuamua kufunga chuo wakati huo zilikua njema, ila zinaleta aibu pale inapokuja kuonekana kuna watu nyuma yake wenye maneno ya uchochezi tena wakiwa ni watendaji wa Serikali.Maneno haya yangesemwa na upinzani kwa waelewa tungeona ni mbinu [Technical] lakini zinapotamkwa na mtu ndani ya Serikali yenye dola Wananchi wanaipokea taarifa hiyo tofauti sana ukizingatia vuguvugu hili la ujio wa uelewa wa umma dhidi ya siasa za Tanzania.
   
 11. SOKON 1

  SOKON 1 JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,115
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Msomi anayezungumza pumba nashindwa kumwelewa Pro Kikula kama kuna manafunzi walitaka kuchoma moto hawapeleke mahakamani ni sio kubwabwanya. Pili huyo mkuu wa wilaya nadhani hiyo nafasi wamepeana kindugu haiwezekani awe na uwezo mdogo wa kufikiria.
   
 12. b

  buyegirhyme Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli Kikula una matatizo, kama unao ushahidi wa hao waliotaka kutengeneza mabomu, wafungulieni mashtaka mahakamani, huwezi kudanganya watu wazima kwa kuja kwako usiku kuzuia mgomo kwa madai kuwa matatizo yetu yanashughulikiw a, tulipogoma mwezi disemba mwaka jana mliahidi pamoja na mawaziri lakini hamkuweza kutimiza kwa takribani miezi sita, je mngeweza ndani ya muda wa wiki mbili kabla ya Mitihani ya mwisho(UE)? Naona husimamii taaluma, bali unashinikizwa na siasa hasa za chama tawala, mnakifanya chuo chetu uwanja wa malumbano ya kisiasa, na ninasikitika kuwa mgomo wetu umehusishwa na shinikizo kutoka chadema kitu ambacho si kweli, tunadai haki yetu ya msingi ambayo wa[NENO BAYA] wachache walioshiba wanadai siyo lazima, sio lazima mtu wa digrii kwenda mafunzo kwa vitendo? lazima huyo anaedai kusimamia taaluma akubaliane nami kuwa mafunzo kwa vitendo ni muhimu kwa ngazi yetu, si kitu ambacho mwanafunzi anasubiri shinikizo la chama chochote ili achukue hatua za kudai haki yake! katika mgomo na maandamano ya amani hakuna mali iliyoharibiwa kuonesha busara zetu kama wasomi, au mnataka tuvunje majengo ndipo msikie madai yetu? Kwa kweli msipo weka mambo sawa katika chuo chetu sasa hivi ingali bado mapema; hapo mbeleni kitawashinda na ndoto za kubeba wanafunzi zaidi ya 40,000 kwa mkupuo mtazijutia, kwani mtatoa wataalamu bomu, na hata sifa ya chuo pia haitakwenda kokote kule. Acheni danadana katika kushughulikia mambo ya msingi! Mfano ni pale mlipo wa-suspend wanafunzi wa mwaka wa pili International Relations na wengine kadhaa ambao wengine majina yao mliyaandika kwa a.k.a kitu kisicho rasmi kuonesha jinsi gani msivyo makini katika kazi zenu, mkadai hao wamehusika katika kuchochea vurugu, mgomo usio halali na mengineyo...hapa pia mlifanya jambo lisilo la msingi, na pia natatizika na umakini wenu katika uchunguzi wenu. Msipotatua tatizo sasa, jueni kuwa wanafunzi watarudi na kurudia migomo vilevile, chuo kitadidimia hata zaidi na pia mtaonekana mmeshindwa kazi! Hatufanyi siasa katika chuo chetu bali taaluma, japokuwa moja ya taaluma tunazosomea ni Taaluma ya Siasa! Vivi Tanzania, Viva Africa!
   
 13. b

  buyegirhyme Member

  #13
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ivi ni kweli uyo mkuu wa wilaya yupo serious au!!!!!kama kweli serikali inadai inaondoa siasa vyuoni hiki anachofanya uyu ni nini??????siamini kama viongozi wengine hasa wa chuo wanaliona hili afu wapo kimya 2,,kwa kweli tz hakuna tunapo elekea kwa staili hii..,viongozi wa udom nao badala ya kusolve hi ishu mapema ili kurudisha wanafunzi chuoni kuendelea na masomo wanang'ang'ana kutoa shutma mpya kila siku,,je kwa hili soko la ushindani tunatarajia kufanya nini kama nchi?????!!!!!!!!!!!!!!!


  "siwarudishi wanafunzi kwa shinikizo la kisiasa maana siku ya mgomo mimi niliweka rehani maisha yangu baada ya kuambiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa wanafunzi wasigome nikawafuata saa sita usiku nikawaambia Serikali inashughulikia madai yenu, lakini baadaye saa tisa usiku nikasikia wameandamana,'' alisema kikula
  kwani umeambiwa ni majambazi ss unajihami na nini, kama mnacho fanya ni haki, ua mlikua mnajihami mkijua ni kweli hamtoi haki zao
   
 14. P

  PascalFlx Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]
  MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idrisa Kikula amesema hawezi kushawishika kwa lolote katika kuwarudisha chuoni hapo wanafunzi kwa kuwa anazo taarifa kuwa baadhi walitengeneza mabomu ya kupambana na polisi.

  Profesa Kikula alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na wakuu wa wilaya wa wilaya zote nchini ambao walitembelea chuo hicho kwa ajili ya kujifunza.

  Alisema kuwa hakuna kitu kitakachomshawishi kuwarudisha wanafunzi kwa kuwa anasimamia taaluma sio siasa kama ambavyo baadhi ya wabunge wanataka iwe.

  “Siwarudishi wanafunzi kwa shinikizo la kisiasa maana siku ya mgomo mimi niliweka rehani maisha yangu baada ya kuambiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa wanafunzi wasigome nikawafuata saa sita usiku nikawaambia Serikali inashughulikia madai yenu, lakini baadaye saa tisa usiku nikasikia wameandamana,’’ alisema Profesa Kikula na kuongeza:

  “Hata hivyo, uchunguzi wetu ulibaini kuwa baadhi yao siku moja kabla walikwenda mjini kununua petroli ambayo walitaka kutengeneza mabomu ya kupambana na polisi.

  “Sasa, kwa hali hiyo mnadhani ingekuwaje lazima tufanye uchunguzi wa kina kabla ya kuwaruidisha.’’

  Kauli ya makamu mkuu huyo iliungwa mkono na wakuu hao wa wilaya ambao walitaka uongozi wa Udom usiwarudishe kirahisi wanafunzi hao ili wajifunze kwanza kuwa walichofanya hakikuwa kizuri.

  “Tena mkianza kuwarudisha rudisheni wana-CCM, hao wa Chadema achana nao maana ndio wanaoanzisha vurugu na uvunjifu wa amani hawana shukrani hao hata siku moja na wala hawajui kutoa fadhila zaidi ya kulalamika kila kitu,’’ alisikika akisema mmoja wa wakuu hao wa wilaya.

  Mwanzoni mwa mwezi, uongozi wa chuo hicho uliwafukuza wanafunzi zaidi ya 9,000 wa Chuo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano baada ya kufanya maandamano yaliyomtaka baadhi ya mawaziri wajiuzulu.

  Waliwataja kuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani , Shamsi Vuai Nahodha wajiuzulu kwa madai ya kuwadanganya.

  Wanachuo hao walikuwa wakishinikiza kupelekwa katika mazoezi ya vitendo pamoja na kununuliwa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na kompyuta.

  Wabunge wa Bunge la Muungano ambao wanaendelea na mkutano wao mjini Dodoma wamekuwa wakipiga kelele mara kwa mara wakitaka wanafunzi hao warudishwe chuoni hapo kwa madai kuwa walichokuwa wakidai ilikuwa ni haki yao.

  Wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alisema Serikali ilikosea kutowapeleka katika mazoezi ya vitendo wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kuwa hiyo ni haki yao ya msingi.

  Mukama aliwaomba radhi wanafunzi hao kwa upungufu huo na kutaka waipe Serikali mwaka mmoja ili ibadili mfumo unatumika kwa sasa.
  [TABLE="class: contentpaneopen, width: auto"]
  [TR]
  [TD]
  By Habel Chidawali, Dodoma

  Source: Wanafunzi Udom wadaiwa kutengeneza mabomu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 15. Mfatiliaji

  Mfatiliaji Senior Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Udom(yawning)..
   
 16. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Tengenezeni mengi,mtugawie na sisis.Wakati umefika wa kudai haki.
   
 17. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  sasa ndo wakati wa serikali kuwa sikivu kama inavyojisifia kila siku, Nawaomba serikali walifanyie kazi lile wazo la mgombea wa UPDP mh. Dovutwa la kujenga kiwanda cha silaha Dar kwa sababu tayari kuna vijana UDOM washaonyesha vipaji ktk field hiyo tusiache hivyo vipaji vikapotea silaha is good bussiness. Serikali iwasiliane na Prof Kikula atawapa their where abouts
   
 18. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Tengenezeni mengi mtugawie na sisi,Wakati wa kudai haki umefika.
   
Loading...