Hata wao walishindwa kuzuia tabasamu lao!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,017
Reaction score
142,861
Kuna mambo huwa hayazuiliki. Huwa yanakuja tu au yanatokea tu kiasili.

Mapema leo wakati Mchungaji Msigwa anasalimiana na Mheshimiwa Lissu, maafande wa Magereza walishindwa kuzuia tabasamu kwenye nyuso zao.

Achana na maneno yangu. Picha huongea maneno zaidi ya elfu. Jionee mwenyewe.

IMG_0289.jpeg

Naamini hao maafande kisirisiri wanamkubali sana Lissu.
 
Kuna mambo huwa hayazuiliki. Yanakuja tu au yanatokea tu kiasili.

View attachment 3634933

Wanamkubali Sanaa!Asili haiongopi.
 
Achana na maneno yangu. Picha huongea maneno zaidi ya elfu. Jionee mwenyewe.
Lakini swali muhimu zaidi ambalo hukuliuliza, na wengi itabidi waliulize, huyo "Msigwa" amefikafikaje hapo na kuwa katika hali hiyo.

Hata kaka yake Lissu au Heche na wengine wote hawajawahi kuwa na fursa kama hiyo.
Tafakari sana.
 
Ukimsikiliza huyo bwana jela aliyekua anapigwa cross examination na TAL leo , utabaini kuna namna nafsi inamsuta na sio kwamba anapenda ila ni mfumo mbovu ambao amejikuta yumo na hawezi kujinasua.

Mfano ile kauli yake "nikiruhusu watu waje wamuone nitalaumiwa"

Anaulizwa kwani sheria inazuia watu au wewe ndio unaogopa lawama , maana yake ni bwana jela yupo ofisini na gwanda zake ila ni ni kama picha tu mkuu na mtoa maelekezo yuko mbali pengine hata ana mwaka hajakanyaga gerezani kuona wafungwa na mahabusu wanaishi vipi wakati huyo bwana jela anakuwepo ila hana sauti na haruhusiwi kupinga lolote atakaloambiwa.

Madhara ya mfumo mbovu uitwao" maelekezo kutoka juu" ndio umemnyima hata mhadhiri wa UDOM dhamana majuzi kwa kosa la uongo ambalo halina tija yoyote mtu akiamua kutumia mabavu na maelekezo unawekwa nyuma ya nondo kinyume cha sheria.

Tuukatae mfumo huu , mimi naukataa leo kesho na hata kesho kutwa.
 
Kuna mambo huwa hayazuiliki. Yanakuja tu au yanatokea tu kiasili.

Mapema leo wakati Mchungaji Msigwa anasalimiana na Mheshimiwa Lissu, maafande wa Magereza walishindwa kuzuia tabasamu kwenye nyuso zao.

Achana na maneno yangu. Picha huongea maneno zaidi ya elfu. Jionee mwenyewe.

View attachment 3634933

Naamini hao maafande kisirisiri wanamkubali sana Lissu.
Wanamkubali Sana, sema ndio wako kazini
 
Mi kinacho niuma Mungu ametupa mtu makini kama Lissu mwenye sifa kibao tunashindwa kumtumia dah!
Nimeyasoma haya maneno yako. Nikafikiria niandike kitu gani kujibu maneno yako haya mazito.
Nimekaa dakika tatu hivi, nimeshindwa kupata maneno yenye uzito kulingana na haya yako.
Acha niweke kiporo; huenda kuna siku tutakutana tena mkuu 'Nuzulati', humu humu jukwaani, nikiwa na maneno sahihi ya kujibu haya yako.
 
KITUKO KILICHOTOKEA MAHAKAMANI.

Wakati Mkuu wa Gereza yaani BWANA JELA ambae ni Andrew Shabani Ntamamilo alipohojiwa na Mhe. Tundu Lissu kuhusu Kuwazuia kabisa Mawakili kama Vile Deogratias Mahinyila, Dickson Matata lakini pia viongozi wakuu wa Chama akiwemo John Heche, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu wa Chama, John Mnyika na Amani Golugwa ambao ni mashahidi katika kesi ya Uhaini wamekataliwa kuingia Gerezani Ukonga.

Majibu ya Mkuu wa Gereza amesema yeye hajawazuia. Mhe. Lissu akasema basi watakuja kuanzia kesho. Akasema SITAWARUHUSU waingie kwasababu kesi bado iko mahakamani.

Jaji Amir Mruma ndio akaanza kumuhoji kuna amri yoyote ya Mahakama kuwa watu hawa hawapaswi kuja kumtembelea Tundu Lissu? Akasema kwa kiburi tena kuwa SITAWARUHUSU.

Jaji akavua miwani na kumuuliza unataka tufike huko. Uko serious kweli? Akiwa amekasirika sana. Maaskari Magereza walioko nyuma niliokaa nao karibu wamekimbilia nje kucheka.

Baada ya Jaji kukasirika Bwana Jela akaanza kuomba radhi kwa Jaji. Majaji wote watatu wametikisa vichwa vyao na kuonesha wanashangaa mambo haya yanawezekanaje kwenye Taifa lenye sheria na taratibu.

Kesi hii imeendelea tena kutuonesha watawala wa nchi hii wakoje. Ukisikia majibu ya Mkuu wa Gereza unajiuliza kiburi anakitoa wapi?

Ngoja tusubiri maamuzi ya Majaji mwisho wa kesi hii utakuwaje lakini naamini kila mtu anashuhudia uhalisia wa mambo ulivyo katika Taifa letu.

Tuendelee kusubiri lisaa likamilike turudi kuendelea.

Wanachama leo ni wengi mno. Mahakama imetapika. Yupo Makamu Mwenyekiti John Heche, Yupo Katibu Mkuu, Mnyika. Mama Suzan Lyimo, Mwenyekiti BAZECHA, Yupo Boniface Jacob Mwenyekiti Kanda ya Pwani, Dua Lyamzito, Katibu Mkuu BAVICHA, Pamela Massey, Katibu Mkuu Bawacha. Mzee Azaveli Lwaitama, Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama na wanachama wengine mbalimbali.

Tutaendelea kuwaleteeni live moja kwa moja mwenendo wa kesi hii kutokea Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es salaam.

Screenshot_20260722-221237.png
 
View attachment 3634965
Mahakama mfukoni 😄😄
 
Back
Top Bottom