kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,293
- 12,593
Kwa mara ya kwanza leo nimemsikia kwa masikio yangu mfanyabiashara aliyeondolewa kando ya barabara akisifia usafi ulioaza kujitokeza kandokando ya barabara zetu.
Nilikuwa na rafiki yangu aliyekuwa anauza matikiti ya kukata vipande pale Banana Ukonga jirani na taasisi ya Hali ya Hewa akisifia sana namna sehemu hiyo inavyoonekana sasa baada ya wauza miwa, mananasi na matikiti kufurushwa na Mh. Mkala. "Ni ubishi wetu tu lakini kweli tulikuwa tunayachafua mazingira", alisikika ex mmachinga akisema. nikamuuliza sasa uko wapi na unafanya nini, akasema amerudia kazi yake ya udereva maana leseni ya udereva anayo lakini aliitia mfukoni afanye umachinga.
Nina uhakika kuwa kosa lilikuwa ni serikali kuacha kuwaambia vijana mapema kuwa hapo hapana kwa biashara, sio vijana. Na hata leo vijana wako tayari kuondoka kama watapewa muda wa kumalizia bidhaa zao walizonazo mikononi. Hata wao wanafahamu kuwa walipo sipo ila walikuwa wakisikilizia tu, hatimaye wakajenga mazoea na kuvutia wengine.
Mitaa ikiwa safu CCM isiwe na mashaka 2025.